Jinsi ya kutumia Muhtasari wa Kutangaza

Muhtasari wa Kutangaza hutoa maelezo muhimu zaidi ya hadhira na vipimo vya kituo ili kuwasaidia watayarishi wajiandae ipasavyo kwa ajili ya ufadhili wa kibiashara.

Angalia Muhtasari wako wa Kutangaza

Unaweza kuangalia Muhtasari wako wa Kutangaza kwenye Studio ya YouTube:

  1. Tumia kompyuta ili uingie katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya kichupo cha BrandConnect.
  4. Kwenye kadi ya Muhtasari wa Kutangaza, bofya ANGALIA MUHTASARI WA KUTANGAZA.

Data ya Hadhira na Kituo

Muhtasari wa Kutangaza una data muhimu zaidi ya hadhira na vipimo vya kituo kama vile, lakini si tu:

  • Bango la kituo na wasifu
  • Aina maarufu za hadhira na ununuzi
  • Demografia na takwimu kuu za kituo
  • Video za kampeni za kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui
  • Video maarufu kwa jumla

Vikundi vya watumiaji vinajumuisha vikundi vya watu wenye mambo mahususi yanayowavutia, makusudi na maelezo ya demografia, kama yanavyokadiriwa na Google.

Ili uweke mapendeleo kwenye kadi:

  1. Chagua '' Menyu.
  2. Bofya Badilisha.
  3. Panga kulingana na aina zinazofaa zaidi na maarufu zaidi au tumia upau wa kutafutia ili kupata aina nyingine za hadhira.
  4. Chagua hadi aina 5 zinazokufaa wewe na ufadhili wako wa kibiashara.
  5. Bofya "Hifadhi".

Kuweka Mapendeleo Kwenye Ripoti Yako ya Muhtasari wa Kutangaza

Baadhi ya kadi kwenye ripoti ya Muhtasari wa Kutangaza zinaweza kubadilishwa ili kukusaidia kuangazia vipengele vya kituo chako ambavyo vinaweza kuvutia biashara fulani.

Ili ubadilishe upendavyo kadi kwenye ripoti yako ya Muhtasari wa Kutangaza:

  1. Chagua'' Menyu
  2. Bofya Badilisha.

Si kadi zote zinaweza kubadilishwa. Ikiwa huwezi kubadilisha kadi husika, unaweza kuchagua kuondoa maelezo yasionekane kwenye ripoti. Ili kuondoa kadi kwenye ripoti:

  1. Chagua'' Menyu
  2. Bofya Ficha.

Unapobadilisha kadi inayojumuisha video, unaweza kuchagua hadi video 4 za kujumuisha. Kwa kadi zilizo na aina, unaweza kuchagua hadi aina 5 kwa kila kadi.

Kupakua ripoti na kushiriki na biashara

Ukimaliza kubadilisha ripoti, unaweza kukagua kwanza na kupakua Muhtasari wako wa Kutangaza.

Ili kukagua Muhtasari wa Kutangaza: Kwenye kona ya juu kulia, chagua ONYESHO LA KUKAGUA.

Ili kupakua Muhtasari wa Kutangaza: Kwenye kona ya juu, chagua PAKUA PDF.

Hakikisha kuwa uko tayari kushiriki data yako na biashara au mtu mwingine yeyote unayemtumia PDF.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13775280556525706521
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false