Mtayarishi anapotueleza kuwa video yake inajumuisha matangazo yanayolipiwa, tutaonyesha ufumbuzi mwanzoni mwa video. Matangazo yanayolipiwa yanajumuisha bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa, udhamini au mahusiano mengine ya kibiashara ambayo huenda yalishawishi maudhui yako.
| Aina ya matangazo yanayolipiwa | Ufafanuzi |
|
Kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui |
Video kuhusu bidhaa au huduma kwa sababu kuna uhusiano kati ya mtayarishi na mtengenezaji wa bidhaa au mtoa huduma. Video zilizotayarishwa za kampuni au biashara kwa lengo la kufidiwa au kupokea bidhaa au huduma bila malipo. Video ambapo chapa, ujumbe au bidhaa ya kampuni au biashara hiyo imejumuishwa moja kwa moja kwenye maudhui na kampuni imempa mtayarishi pesa au bidhaa bila malipo ili atengeneze video hiyo. |
|
Maudhui yaliyoidhinishwa |
Video zilizotayarishwa za mtangazaji au muuzaji na kujumuisha ujumbe unaoendana na maoni, imani au hali zinazohusu utumiaji wa bidhaa au huduma na mtayarishi. |
|
Udhamini |
Video ambazo gharama zote au sehemu ya gharama za utayarishaji zimelipwa na kampuni. Kwa jumla, udhamini unatangaza chapa, ujumbe au bidhaa za wengine bila kujumuisha chapa, ujumbe au bidhaa moja kwa moja katika maudhui. |
Kumbuka kuwa hata ukiwa na YouTube Premium, huenda bado ukapata ufumbuzi wa maudhui yaliyodhaminiwa yaliyowekwa moja kwa moja na watayarishi. Ikiwa wewe ni mtayarishi, pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, udhamini na maudhui yaliyoidhinishwa kwenye maudhui yako.