Kudhibiti chapa ya kituo chako

Weka chapa kwenye utambulisho wa chaneli yako ya YouTube kwa kusasisha picha yako ya wasifu, bango la chaneli na alama maalum ya video.

Kubadilisha picha yako ya wasifu

Badilisha picha yako ya wasifu katika Studio ya YouTube. Picha yako ya wasifu ni picha inayoonyeshwa kwa watazamaji katika chaneli, video na vitendo vyako vyenye maelezo yanayoonekana kwa umma kwenye YouTube.

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo kisha Wasifu.
  3. Bofya BADILISHA kisha uchague mchoro au picha kutoka kwenye kompyuta yako. Badilisha mipangilio iliyowekwa mapema ya rangi na ukubwa uliopunguzwa wa mchoro au ukubwa wa picha uliyopakia, kisha ubofye NIMEMALIZA.
  4. Bofya CHAPISHA. Inaweza kuchukua dakika chache kabla picha yako ya wasifu kusasishwa kwenye YouTube.

Kupunguza ukubwa wa picha yako ukitumia kibodi au teknolojia saidizi

Ili upunguze ukubwa wa picha yako kutoka kwenye kona

  1. Sogeza ili uchague kona ya picha yako.
  2. Tumia vitufe vya vishale ili upunguze ukubwa wa picha.

Hamisha mraba wote wa kupunguza ukubwa

  1. Sogeza ili uchague mraba wote wa kupunguza ukubwa.
  2. Tumia vitufe vya vishale ili ubadilishe mkao wa mraba wa kupunguza ukubwa.

Mwongozo wa picha ya wasifu

Ni sharti picha yako ya wasifu itii Mwongozo wetu wa Jumuiya na itimize vigezo vifuatavyo:

  • Faili ya JPG, GIF, BMP au PNG (usitumie GIF zilizohuishwa)
  • Ukubwa wa picha haupaswi kuzidi MB 15.
  • Picha itakayotekelezwa kwa pikseli 98 X 98.

Watayarishi wa YouTube

Picha ya bango lako huonekana kwenye mandharinyuma katika sehemu ya juu ya ukurasa wako wa YouTube.
  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo kisha Wasifu.
  3. Bofya BADILISHA kisha uchague picha. Ili ufanye manadiliko, chagua onyesho la kukagua na ubadilishe sehemu unayopunguza, kisha ubofye NIMEMALIZA.
  4. Bofya CHAPISHA.
Kumbuka: Picha ile ile ya bango hutumika kwenye skrini za kompyuta, simu na televisheni, lakini huonekana kwa njia tofauti kulingana na kifaa chako.

Chaneli Rasmi za Msanii

Picha yako ya bango hutumika tu kwenye kompyuta na vifaa vya mkononi. Ili usasishe bango hilo, fuata maagizo ya Mtayarishi wa YouTube yaliyo hapo juu.

Ili usasishe bango ulilonalo kwenye televisheni na katika YouTube Music:

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Wasifu.
  3. Bofya karibu na picha ya wasifu na uchague picha. Ili ufanye mabadiliko kwenye picha,
    • Chagua Toleo la kukagua kisha ubadilishe picha.
    • Bofya NIMEMALIZA.
  4. Bofya HIFADHI katika sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.

Mwongozo wa picha ya bango

Fuata mapendekezo haya ili bango lako litekelezwe ipasavyo:

  • Kipimo cha chini cha upakiaji: pikseli 2048 x 1152 yenye uwiano wa 16:9.
  • Katika kipimo cha chini, eneo salama la maandishi na nembo: pikseli 1235 x 338.
  • Kipimo kinachopendekezwa (hasa katika televisheni): pikseli 2560 x 1440.
  • Picha zinapaswa kutoshea kwenye skrini yote katika vifaa vikubwa lakini ukubwa wake utapunguzwa katika mionekano na vifaa fulani.
  • Usijumuishe vipengele vyovyote vya ziada vya faili (k.m. vivuli, kingo na fremu).
  • Ukubwa wa faili: Usizidi MB 6.

Jinsi ya kubadilisha ukubwa wa picha

Unaweza kutumia kihariri cha picha cha kompyuta yako au zana ya mtandaoni ya kubadilisha ukubwa wa picha ili upunguze ukubwa wa picha. Kwa mfano, unaweza kutumia Preview kwenye kompyuta ya Apple au Microsoft Photos kwenye Windows.

Weka alama maalum ya video yako

Unaweza kuwahimiza watazamaji wajisajili kwenye kituo chako kwa kuweka alama maalum ya video kwenye video yako. Unapoongeza alama maalum ya video, watazamaji wanaweza kujisajili moja kwa moja katika chaneli yako wanapotumia YouTube kwenye kompyuta.
  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo kisha Wasifu.
  3. Chagua muda wako wa kuonyesha:
    • Mwisho wa video: Alama maalum ya video itaonekana kwa sekunde 15 za mwisho wa video.
    • Muda maalum wa kuanza: Alama maalum ya video itaanza kuonekana muda utakaochagua.
    • Video yote: Alama maalum ya video itaonekana wakati wote kwenye video.
  4. Bofya BADILISHA na uchague picha. Badilisha ukubwa wa picha yako, kisha ubofye NIMEMALIZA.
  5. Bofya CHAPISHA.
Kumbuka: Alama maalum za video hazipatikani kwenye video zinazolenga watoto. Iwapo uliweka alama maalum ya video, lakini video yako sasa inalenga watoto, watazamaji hawataona alama maalum.

Mwongozo wa alama maalum ya video

Ni sharti alama yako maalum ya video itimize vigezo vifuatavyo:

  • Kima cha chini: pikseli 150x150.
  • Picha ya mraba isiyozidi MB 1 kwa ukubwa.

Upatikanaji

Alama maalum ya chaneli inapatikana katika mwonekano wa mlalo kwenye kompyuta na vifaa vya mkononi (huwezi kuibofya kwenye simu). Alama maalum za kituo hazionyeshwi kwenye vichezaji maalum visivyo na chrome vya YouTube au Adobe Flash.

Vipimo vya alama maalum ya video

Unaweza kupata vipimo katika ripoti ya Chanzo cha usajili kwenye Takwimu za YouTube.

Tazama jinsi ya kudhibiti uwekaji chapa wa kituo chako

Tazama video ifuatayo kutoka kwenye chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube kuhusu jinsi ya kusasisha picha yako ya wasifu, bango la chaneli na alama maalum ya video.

Customize Your Channel Branding & Layout: Add a Profile Picture, Banner, Trailer, Sections, & more!

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu