Hitilafu za kawaida za upakiaji

Ikiwa unakumbwa na matatizo ya kupakia video yako, chagua ujumbe kuhusu hitilafu unaouona kisha fuata hatua za utatuzi ili upate suluhisho la tatizo lako.

"Tumekumbwa na matatizo ambayo hayakutarajiwa"

Jaribu kusubiri kwa dakika chache, kisha pakia tena.

"Seva imekataa faili"

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea unapopakia faili lililo katika muundo usiyo sahihi. Hakikisha kwamba unapakia aina ya faili inayotumika.

"Hitilafu imetokea wakati wa kutuma data kupitia mtandao."

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea kivinjari chako kinapohitaji kusasishwa kufikia toleo la hivi karibuni. Vifuatavyo ni vivinjari tunavyokushauri utumie ili kupakia video:
Baada ya kusasisha kivinjari chako, jaribu kupakia tena.

"Uchakataji haujakamilishwa"

Huenda ujumbe huu kuhusu hitilafu ukatokea ikiwa faili ulilolipakia limefupishwa au si sahihi. Pia, unaweza kutokea kwenye mtandao wenye kasi ndogo ya kupakia. Jaribu kucheza video kwenye kifaa chako na uhakikishe unapakia aina ya faili inayotumika, kisha pakia tena. Endapo tatizo litaendelea, jaribu kupakia video yako kupitia mfumo tofauti.

"Hitilafu ya mtandao imetokea"

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea kivinjari chako kinapohitaji kusasishwa kufikia toleo la hivi karibuni. Vifuatavyo ni vivinjari tunavyokushauri utumie ili kupakia video:
Baada ya kusasisha kivinjari chako, jaribu kupakia tena.
"Imeshindwa kupakia. Hali ya kituo chako au mipangilio ya akaunti kwa sasa hairuhusu upakiaji."
Huenda ujumbe huu kuhusu hitilafu ukatokea ikiwa:

"Hitilafu ya usalama imetokea"

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea unapokuwa na mipangilio ya usalama isiyo ya kawaida kwenye kivinjari chako. Kuna uwezekano kuwa mipangilio hiyo inatokana na kinga mtandao, kingavirusi, kizuia vidadisi au programu nyinginezo zinazohusiana. Tunakushauri uzime kwa muda programu hii kisha jaribu kupakia tena.

"Imekataliwa (faili ni dogo sana)"

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea ukijaribu kupakia faili ambalo ni dogo zaidi ya KB 2. Hakikisha kwamba faili la video lina ukubwa wa angalau KB 2 kisha pakia tena.

"Imeshindwa (faili tupu la .mov)"

Ujumbe huu kuhusu hitilafu hutokea wakati muundo wa faili za QuickTime movie zinapohifadhiwa kuwa 'reference movie'. Ili uhakikishe kwamba video yako inageuzwa kwa usahihi, chagua "Save as a self-contained movie" kisha jaribu kupakia tena.

"Umefikisha kikomo cha kupakia cha siku. Unaweza kupakia video zaidi baada ya saa 24."

Ili tuhakikishe usalama kwenye YouTube, tumeweka kikomo cha idadi ya video zinazoweza kupakiwa na kituo ndani ya kipindi cha saa 24 kwenye kompyuta ya mezani, kifaa cha mkononi na YouTube API.
Vikomo vinaweza kutofautiana kulingana na nchi au eneo au historia ya kituo. Maonyo ya hakimiliki yanaweza kuathiri ustahiki wa historia ya kituo. Maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yataathiri idadi ya video utakazoweza kupakia.
Ikiwa utapokea hitilafu inayosema "Umefikisha kikomo cha kupakia cha siku" unapojaribu kupakia video kwenye YouTube, jaribu tena baada ya saa 24.

Sababu nyingine

Huenda ukapata ujumbe kuhusu hitilafu unapopakia faili iliyopo kwenye muundo ambao si sahihi. Hakikisha kwamba unapakia aina ya faili inayotumika. Pia, unaweza kujaribu kubadili kodeki au programu ya kuhariri video unayotumia.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9814003045976731684
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false