Unaweza kutiririsha kwenye YouTube Moja kwa Moja kupitia RTMPS, kiendelezi salama cha itifaki maarufu ya kutiririsha video za RTMP. Ni RTMP kupitia muunganisho wa Usalama wa Mawasiliano Mtandaoni (TLS/SSL) na hutoa usimbaji fiche.
Kuanza
Hakikisha kuwa programu yako ya kusimba inaruhusu RTMPS na kuwa unafahamu mambo ya msingi ya kutiririsha mubashara kwenye YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha mtiririko mubashara ukitumia programu ya kusimba.
1. Kuangalia mipangilio iliyowekwa mapema ya RTMPS kwenye YouTube
Sasisha programu yako ya kusimba kuwa toleo jipya na uangalie mipangilio iliyojumuishwa ndani ya RTMPS kwenye YouTube.
- Ukiona mipangilio iliyowekwa mapema ya RTMPS kwenye YouTube, ichague. Huenda ukahitaji kuweka ufunguo wako wa mtiririko kutoka kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja pia. Sasa uko tayari kutiririsha.
- Iwapo programu yako ya kusimba haina mipangilio iliyowekwa mapema ya RTMPS kwenye YouTube, nenda katika “Weka mipangilio ya URL ya seva.”
2. Weka URL ya seva
Unaweza kupata URL ya RTMPS kutoka kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja. Kumbuka kuwa bado itakuonyesha URL ya RTMP kwa chaguomsingi, kwa hivyo hakikisha kuwa umepata URL ya RTMPS badala yake.
- Fungua Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
- Bofya kichupo cha Mtiririko au uratibu mtiririko mpya.
- Chini ya “Mipangilio ya mtiririko,” katika sehemu ya "URL ya Mtiririko", bofya aikoni ya kufunga ili kuonyesha URL ya RTMPS.
- Nakili URL ya Mtiririko.
- Bandika URL katika programu yako ya kusimba.
- Nakili ufunguo wako wa mtiririko wa YouTube kutoka kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja na uubandike katika programu yako ya kusimba.
Utatuzi
Hitilafu za SSL
Ukiona hitilafu kama vile "cheti kisicho sahihi cha SSL kilichotumwa na seva ya RTMP," jaribu yafuatayo:
1. Kuhakikisha kuwa URL ya seva ni sahihi
rtmps
, wala si rtmp
.2. Kubainisha nambari ya mlango
Iwapo URL inaonekana kuwa sahihi lakini bado unapata hitilafu ya SSL, jaribu kubainisha mlango wa 443 katika URL. Ufuatao ni mfano, lakini utahitaji kusasisha ili ilingane na URL ya Mtiririko unayopata kutoka kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja:
rtmps://exampleYouTubeServer.com:443/stream
Au, iwapo programu yako ya kusimba inakuruhusu ubainishe nambari ya mlango katika chaguo za mipangilio, tumia 443 hapo.
Muda wa muunganisho umekwisha
Ukiona hitilafu kama vile "imeshindwa kuunganisha kwenye seva — muda wa muunganisho umeisha," basi jaribu yafuatayo:
1. Kuhakikisha kuwa URL ya seva ni sahihi
Fuata hatua katika “Weka mipangilio ya URL ya seva” ili uhakikishe kuwa URL ya seva ni sahihi.
Itifaki na seva zinapaswa kuwa rtmps, wala si rtmp.