Kudumisha usalama wako mtandaoni ni muhimu zaidi kwa kila kitu tunachofanya - ni wajibu wetu kuwa wazi kuhusu data tunayotumia huku tukikupa chaguo na udhibiti wa data hiyo.
Data unayotoa kwa Google na YouTube inatusaidia kuboresha hali yako ya utumiaji unapotumia huduma zetu. Unaweza kudhibiti mipangilio yako ya faragha ya YouTube kwa kutembelea Data yako kwenye YouTube au Akaunti yako ya Google.
Jinsi YouTube inavyoweza kutumia data iliyounganishwa na akaunti yako
Jinsi YouTube inavyoweza kutumia data iliyojumlishwa
Jinsi YouTube inavyokusaidia kudhibiti faragha na usalama wako
Jinsi YouTube inavyoweza kutumia historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta pamoja na jinsi unavyoweza kuidhibiti
Jinsi YouTube inavyotumia data ya mahali ulipo
YouTube hukadiria mahali ulipo kwa sasa kwa kutumia data ya mahali kwenye kifaa chako, anwani ya nyumbani au ya kazini uliyohifadhi kwenye Akaunti yako ya Google na anwani yako ya IP ili kukupa hali ya utumiaji inayokufaa zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu kuelewa na kudhibiti data ya mahali ulipo unapotafuta kwenye YouTube.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi data ya mahali inavyotumika kwenye Google, ikiwa ni pamoja na kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi kwenye YouTube. Pia, tembelea Data yako kwenye YouTube ili upate maelezo kuhusu jinsi YouTube inavyotumia data ya mahali ulipo.
Dhibiti aina ya data na shughuli zinazotumika kuweka mapendeleo kwenye matangazo
Unapotumia programu za Google, unaweza kudhibiti aina ya data na shughuli zinazoweza kutumika kuweka mapendeleo kwenye matangazo au unaweza kuzima mipangilio ya kuweka mapendeleo ya matangazo. Tunarahisisha kudhibiti data inayotumika kukuwekea mapendeleo ya matangazo kwenye Mipangilio ya Matangazo. Data hii inajumuisha kile tunachokadiria kuhusu mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako pamoja na unavyowasiliana na watangazaji wengine ambao wanashirikiana nasi kuonyesha matangazo, na taarifa ulizoweka kwenye Akaunti yako ya Google.
Unapoingia katika Akaunti yako ya Google, dhibiti jinsi matangazo yako yanavyowekewa mapendeleo au zima matangazo yenye mapendeleo kwenye Mipangilio yako ya Matangazo.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu Google Ads na data, nenda kwenye Kituo chetu cha Usalama.Jinsi YouTube inavyoweza kutumia taarifa zako binafsi
YouTube haiuzi taarifa zako binafsi
Jinsi YouTube inavyoweza kutumia maudhui, kama vile video na picha ulizochagua kupakia
Maudhui ambayo unaamua kupakia tu ndiyo yanayohifadhiwa na YouTube na kuunganishwa kwenye chaneli yako ya YouTube. Anayeweza kutazama maudhui haya ni kulingana na mipangilio ya faragha ya video uliyoichagua. Kulingana na mipangilio ya faragha ya video yako, maudhui ambayo umepakia yanaweza kuonyeshwa au kupendekezwa kwa watazamaji wengine. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya faragha ya video yako hapa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti na kuhariri maudhui kwa kutumia Studio ya YouTube kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi hapa.
Nini kinatokea kwa maudhui yako na data husika baada ya kufuta video
Ukichagua kufuta video kwenye YouTube, video hiyo itafutwa kabisa. Haiwezi kurejeshwa baadaye na video hiyo haitaweza kutafutwa tena kwenye YouTube. Data inayohusishwa na video hiyo, kama vile muda wa kutazama, bado itakuwa sehemu ya ripoti zilizojumlishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti na kuhariri maudhui kwa kutumia Studio ya YouTube kwenye kompyuta au katika kifaa cha mkononi hapa. Pata maelezo zaidi ya jinsi ya kufuta na kubadilisha videohapa.
Kinachofanyika unapofuta chaneli yako ya YouTube
Angalia Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia data kwenye YouTube na huduma zote za Google.