Kufahamu mambo ya msingi kuhusu faragha kwenye programu za YouTube

Kudumisha usalama wako mtandaoni ni muhimu zaidi kwa kila kitu tunachofanya - ni wajibu wetu kuwa wazi kuhusu data tunayotumia huku tukikupa chaguo na udhibiti wa data hiyo.

Data unayotoa kwa Google na YouTube inatusaidia kuboresha hali yako ya utumiaji unapotumia huduma zetu. Unaweza kudhibiti mipangilio yako ya faragha ya YouTube kwa kutembelea Data yako kwenye YouTube au Akaunti yako ya Google.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia data iliyounganishwa na akaunti yako

YouTube hutumia data yako ili kuboresha hali yako ya utumiaji, kama vile kukukumbusha ulichotazama na kukupa mapendekezo na matokeo ya utafutaji yanayofaa zaidi. Shughuli na maelezo yako yanaweza pia kutumiwa ili kuweka mapendeleo ya matangazo yaliyo kwenye YouTube na Huduma nyingine za Google. Unaweza kudhibiti au kuzima shughuli ya data katika Data yako kwenye YouTube.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia data iliyojumlishwa

Ili kuboresha huduma zetu mara kwa mara, huwa tunatumia data ya YouTube iliyojumlishwa bila utambulisho ili kuboresha hali ya utumiaji kwa watumiaji wote. Kwa mfano, huwa tunatumia taarifa za uchunguzi ili kuelewa programu ya YouTube inavyofanya kazi, ili kurekebisha hitilafu na kuboresha kasi na utendaji.

Jinsi YouTube inavyokusaidia kudhibiti faragha na usalama wako

Kila wakati, tunahakikisha kuwa unaendelee kudhibiti faragha na usalama wako kwenye YouTube — iwe ni kukusaidia kudhibiti mipangilio yako ukitumia zana mahiri au kurahisisha matumizi ya mipangilio hiyo kwenye bidhaa zetu. Kwa mfano, tunatoa zana za kupunguza data kama vile kipengele cha kufuta kiotomatiki, kinachokupa chaguo la YouTube kufuta data yako kiotomatiki baada ya kipindi fulani. Unaweza kudhibiti data ya shughuli zako kwenye Data yako kwenye YouTube.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta, na jinsi unavyoweza kuidhibiti

YouTube hutumia historia ya mambo uliyotafuta na ya video ulizotazama ili kuboresha hali yako ya utumiaji, kwa mfano kukurahisishia kupata video ulizotazama hivi karibuni au kuboresha mapendekezo yako. Historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta inaweza pia kutumika ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Unaweza kuangalia au kufuta data ya historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta katika Data yako kwenye YouTube ili mapendekezo na matangazo yakufae zaidi. Ikiwa huna historia ya kutosha ya video ulizotazama hapo awali, vipengele vya YouTube vinavyotegemea historia ya video ulizotazama kukupa mapendekezo ya video, kama vile mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, huondolewa.
Tembelea Data yako kwenye YouTube ili udhibiti aina ya data ya shughuli inayohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Unaweza pia kuvinjari au kufuta shughuli zako kwenye YouTube.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia data ya mahali ulipo

YouTube inaweza kutumia maelezo ya mahali kama vile eneo uliko kwa ujumla, lililokadiriwa kutokana na Anwani yako ya IP ili kukuonyesha mapendekezo ya maudhui yanayokufaa yaliyo karibu nawe na matokeo ya utafutaji. Kwa mfano, ikiwa unatafuta habari au taarifa ya hali ya hewa kwenye YouTube, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha habari kuu na taarifa ya hali ya hewa ya eneo lako kwa ujumla. Pia, iwapo utachagua kupakia video, maelezo yako ya mahali ulipo, kama vile eneo lako kwa jumla unapopakia video au eneo ambalo umeweka lebo kwenye video pia linaweza kutumiwa kupendekeza maudhui yako kwa hadhira lengwa iliyo katika eneo lako.

Eneo kwa ujumla ni kubwa kuliko maili 1 ya mraba na lina angalau watumiaji 1,000. Eneo kwa ujumla la utafutaji wako halikutambulishi. Badala yake, eneo kwa ujumla husaidia kulinda faragha yako na kwa kawaida ni kubwa kuliko maili 1 ya mraba nje ya miji.

Unaweza kuangalia, kufuta, kuzima au kuchagua kufuta kiotomatiki Kumbukumbu ya Maeneo Yako katika Data yako kwenye YouTube.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi data ya mahali inavyotumika kwenye huduma za Google, ikijumuisha kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi kwenye YouTube.

Pata maudhui ya mahali ulipo kwa kuweka eneo kwenye utafutaji wako

Ikiwa unatafuta kitu mahususi na hupati matokeo ya utafutaji yanayofaa, jaribu kuweka eneo kwenye utafutaji wako, kama vile Hali ya hewa katika eneo la Chelsea.

Dhibiti aina ya data na shughuli zinazotumika kuweka mapendeleo kwenye matangazo

Unapotumia programu za Google, unaweza kudhibiti aina ya data na shughuli zinazoweza kutumika kuweka mapendeleo kwenye matangazo au unaweza kuzima mipangilio ya kuweka mapendeleo ya matangazo. Tunarahisisha kudhibiti data inayotumika kukuwekea mapendeleo ya matangazo kwenye Mipangilio ya Matangazo. Data hii inajumuisha kile tunachokadiria kuhusu mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako pamoja na unavyowasiliana na watangazaji wengine ambao wanashirikiana nasi kuonyesha matangazo, na taarifa ulizoweka kwenye Akaunti yako ya Google.

Unapoingia katika Akaunti yako ya Google, dhibiti jinsi matangazo yako yanavyowekewa mapendeleo au zima matangazo yenye mapendeleo kwenye Mipangilio yako ya Matangazo.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu Google Ads na data, nenda kwenye Kituo chetu cha Usalama.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia taarifa zako binafsi

Taarifa zako binafsi zinajumuisha maelezo kama vile jina na picha yako. Unaweza kuamua taarifa binafsi utakazoonyesha kwa watu wengine kupitia huduma za Google kwa kudhibiti taarifa binafsi kwenye Akaunti yako ya Google. Baadhi ya matangazo yanaweza kukupatia fomu ili utoe maelezo ya ziada kama vile anwani ya barua pepe na nambari ya simu, lakini taarifa hizi si za lazima na hazihitajiki ili uendelee kutumia YouTube.

YouTube haiuzi taarifa zako binafsi

Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. Tunatumia taarifa tunazokusanya ili kukupa huduma zinazokufaa, ikiwa ni pamoja na kukupa mapendekezo, kuweka mapendeleo kwenye matokeo ya utafutaji na kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Ingawa matangazo haya yanatusaidia kufadhili huduma zetu na kuzifanya zipatikane kwa kila mtu bila gharama za kifedha, hatuuzi taarifa zako binafsi.

Jinsi YouTube inavyoweza kutumia maudhui, kama vile video na picha ulizochagua kupakia

Maudhui ambayo unaamua kupakia tu ndiyo yanayohifadhiwa na YouTube na kuunganishwa kwenye chaneli yako ya YouTube. Anayeweza kutazama maudhui haya ni kulingana na mipangilio ya faragha ya video uliyoichagua. Kulingana na mipangilio ya faragha ya video yako, maudhui ambayo umepakia yanaweza kuonyeshwa au kupendekezwa kwa watazamaji wengine. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya faragha ya video yako hapa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti na kuhariri maudhui kwa kutumia Studio ya YouTube kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi hapa.

Nini kinatokea kwa maudhui yako na data husika baada ya kufuta video

Ukichagua kufuta video kwenye YouTube, video hiyo itafutwa kabisa. Haiwezi kurejeshwa baadaye na video hiyo haitaweza kutafutwa tena kwenye YouTube. Data inayohusishwa na video hiyo, kama vile muda wa kutazama, bado utakuwa sehemu ya ripoti zilizojumlishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti na kuhariri maudhui kwa kutumia Studio ya YouTube kwenye kompyuta au katika kifaa cha mkononi hapa. Pata maelezo zaidi ya jinsi ya kufuta na kubadilisha videohapa.

Kinachofanyika unapofuta chaneli yako ya YouTube

Unaweza kuchagua kufunga au kufuta kituo chako cha YouTube wakati wowote. Kufunga au kufuta kituo chako kutafuta maudhui yako kabisa, ikiwa ni pamoja na video, maoni, ujumbe na orodha zote za kucheza. Hutaweza tena kutoa maoni au kuchapisha maudhui.

Angalia Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia data kwenye YouTube na huduma zote za Google.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11623105684846668833
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false