Jinsi ya kutumia Kuelekezwa Moja kwa Moja kwenye YouTube

Unaweza kuwaelekeza watazamaji wa mtiririko wako mubashara kwenye Onyesho la kwanza ili kuwahamasisha au kuwaelekeza kwenye mtiririko mubashara wa kituo kingine ili uwasaidie watayarishi wengine kukuza vituo vyao.

Mtiririko wako ukiisha, kucheza kiotomatiki kutawapeleka watazamaji wako kwenye Onyesho la kwanza au mtiririko mubashara utakaochagua.

Kumbuka: Ili uelekeze watazamaji wako kwenye mtiririko mubashara wa kituo kingine, kituo hicho kinahitaji kukupa ruhusa katika Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Kuelekezwa Moja kwa Moja

Kuwaelekeza kwingine watazamaji wa mtiririko wako mubashara

  1. Anzisha mtiririko mubashara.
  2. Bofya Hariri.
  3. Bofya Kuweka mapendeleo.
  4. Chini ya “Elekeza kwingine,” bofya Ongeza.
  5. Chagua Onyesho la kwanza au tafuta mtiririko mubashara wa kituo kingine.
  6. Mtiririko wako mubashara utakapoisha, utaona uthibitisho unaosema watazamaji wako wataelekezwa kwingine.

Kuwalekeza kwingine watazamaji wako wa Onyesho la kwanza

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Katika upande wa kushoto, bofya Video.
  3. Chini ya “Mahali pa kuwaelekeza kwingine watazamaji,” bofya Chagua.
  4. Chagua Onyesho lingine la kwanza au utafute mtiririko mubashara wa kituo kingine.
  5. Onyesho lako la kwanza linapoisha, watazamaji wako wataelekezwa kwingine.

Badilisha nani anayeweza kuelekeza watazamaji kwako

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Katika upande wa kushoto, bofya Mipangilio kisha Jumuiya.
  3. Chagua kwenye mipangilio ya ruhusa katika Mipangilio ya Kituo inayoweza kutumika kuelekeza kwingine maudhui. 

    • ‘Vituo ninavyovifuatilia vinaweza kuwaelekeza watazamaji kwenye maudhui yangu’ - Kwa chaguomsingi, kituo chochote unachofuatilia kinaweza kuelekeza kwenye maudhui yako, isipokuwa pale ambapo mipangilio ya wanaofuatilia kituo imewekwa kuwa ya faragha. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya wanaokufuatilia iwe ya umma

    • ‘Ruhusu mtayarishi yeyote aelekeze kwenye maudhui yangu’ - Kwa kuchagua mipangilio hii, mtayarishi yeyote anaweza kuelekeza kwenye maudhui yako. Mipangilio hii haiwezi kutumika na ‘Vituo ninavyovifuatilia vinaweza kuwaelekeza watazamaji kwenye maudhui yangu’ au orodha ya kuelekeza kwingine mwenyewe.

    • 'Vituo mahususi vinavyoweza kuwaelekeza watazamaji kwenye maudhui yangu’-  Ongeza mwenyewe vituo vilivyoidhinishwa kwenye kisanduku cha maandishi ambavyo vinaweza kuelekeza kwenye maudhui yako. Unaweza kuongeza hadi vituo 100 kwenye orodha hii, na inaweza kutumika na mipangilio ya ruhusa ya ‘Vituo ninavyovifuatilia vinaweza kuwaelekeza watazamaji kwenye maudhui yangu’.

  4. Bofya Hifadhi.

Kutimiza masharti

Kipengele hiki kinapatikana kwa watayarishi wanaoelekeza zaidi ya watu 1,000 wanaofuatilia na hawana maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Vidokezo

  • Weka mipangilio ya Onyesho lako la kwanza kabla hujaweka mipangilio ya mtiririko wako mubashara.
  • Kumbuka kuambia hadhira yako kuwa mtiririko mubashara utakapoisha, wasubiri sekunde chache ili skrini zao zipakie Onyesho la kwanza.
  • Bandika ujumbe wa gumzo la moja kwa moja kwenye ukurasa wa Onyesho lako la kwanza unaoelekeza watazamaji kwenye mtiririko wako mubashara.
  • Ruhusu wengine Wanaotiririsha mubashara kuelekeza kwenye mtiririko wako mubashara. Pata maelezo zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1151351990057272451
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false