Mapendekezo ya kujibu maoni yanategemea majibu yanayotolewa sana na watayarishi yanayoonekana kwenye YouTube. Tumia mapendekezo ya kujibu maoni ili ujibu maoni kwa haraka na kwa urahisi zaidi kwenye Studio ya YouTube, programu ya YouTube pamoja na ya Studio ya YouTube katika simu.
Kwa sasa, mapendekezo ya kujibu maoni yanapatikana katika lugha zifuatazo kwenye Studio ya YouTube, programu ya YouTube pamoja na ya Studio ya YouTube katika simu:
|
|
|
|
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya lugha yako.
Kutumia mapendekezo ya kujibu maoni
Kutumia mapendekezo ya kujibu maoni
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Jumuiya
.
- Pata majibu yanayopendekezwa chini ya maoni.
- Chagua pendekezo na ubadilishe ipasavyo.
- Chagua Jibu.
Mapendekezo yaliyoboreshwa ya kujibu maoni
Unapotumia mapendekezo ya kujibu maoni, huenda baadhi ya mapendekezo yakawa yameboreshwa. Mapendekezo yaliyoboreshwa ya kujibu maoni hutumia AI zalishi ili kutayarisha majibu ya maoni ya hiari, unayoweza kubadilisha katika toni na muundo unaopenda.
Mapendekezo yaliyoboreshwa ya kujibu maoni yanapatikana katika lugha zote zinazotumika kwenye maoni ya YouTube. Unaweza kuona mapendekezo ya kujibu maoni katika lugha zaidi ya moja iwapo una historia ya kujibu katika lugha nyingi.
Kutuma maoni kuhusu mapendekezo yaliyoboreshwa ya kujibu maoni
Kwa kuwa haya ni mapendekezo ya kiotomatiki, wakati mwingine tunaweza kukosea. Unaweza kututumia maoni kuhusu pendekezo mahususi lililoboreshwa la kujibu maoni au kukiwa na pendekezo lililoboreshwa la kujibu maoni kwenye maoni yasiyofaa.
- Kando ya pendekezo la maoni, chagua Zaidi
.
- Chagua Je, kuna tatizo?