Kuweka mipangilio ya mtiririko wa HLS

Kutiririsha HDR au kutumia kodeki ambazo hazitumiwi kwenye RTMP kwa kutumia itifaki ya uingizaji ya HLS (Utiririshaji wa Moja kwa Moja wa HTTP) kwenye YouTube Moja kwa Moja.

Kabla ya kuanza

Hakikisha kuwa programu yako ya kusimba inaruhusu RTMPS na kuwa unafahamu mambo ya msingi ya kutiririsha mubashara kwenye YouTube.

1. Angalia mipangilio iliyowekwa mapema ya HLS kwenye YouTube

Ikiwa programu yako ya kusimba ina mipangilio iliyowekwa mapema ya uingizaji (wa data) wa HLS kwenye YouTube, chagua mipangilio iliyowekwa mapema. Huenda ukahitaji kunakili na kubandika ufunguo wako wa mtiririko kama vile katika mitiririko ya RTMP. Sasa uko tayari kutiririsha.

Ikiwa programu yako ya kusimba haina uingizaji (wa data) wa HLS kwenye mipangilio iliyowekwa mapema kwenye YouTube, ruka hatua ya 2 ya “Weka URL ya uingizaji.”

2. Weka URL ya seva

  1. Nenda kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja wa YouTube kisha Tiririsha. Chini ya “Chagua ufunguo wa mtiririko,” bofya Tunga ufunguo mpya wa mtiririko, na uchague HLS kuwa itifaki ya utiririshaji.

Kumbuka: Ikiwa unataka kutiririsha katika HDR, ni sharti usiteue “Washa utatuzi unaofanya mwenyewe”.

  1. “URL ya mtiririko” wa uingizaji wa HLS itasasishwa. URL inapaswa kuanza na “https” badala ya “rtmp”. Nakili URL kwenye programu yako ya kusimba.
  2. Iwapo unahitaji uingizaji (wa data) mbadala, nakili “URL ya seva mbadala.” Ufunguo wa mtiririko tayari ni sehemu ya URL, hivyo huhitaji kunakili “Ufunguo wa mtiririko” kivyake.

Kumbuka: Chaguo la “Muda mchache zaidi wa kusubiri” huzimwa HLS inapochaguliwa. HLS ina muda mrefu zaidi wa kusubiri kwa sababu inatuma sehemu za video, badala ya mtiririko endelevu kama vile RTMP.

3. Kamilisha mipangilio ya HLS

Hakikisha kuwa unasasisha pia mipangilio hii ya HLS inayohitajika na YouTube Moja kwa Moja:

  • Muda wa Sehemu: kati ya sekunde 1-4, muda mchache wa sehemu unasababisha muda mchache wa kusubiri.
  • Muundo wa Sehemu: ni sharti uwe TS (Mtiririko wa Usafirishaji).
  • Kipindi cha Baiti hakitumiki.
  • Ni sharti utumie orodha ya kucheza endelevu yenye sehemu zisizozidi 5 zinazosubiri kushughulikiwa.
  • Ni sharti utumie HTTPS POST/PUT.
  • Usimbaji kwa njia fiche hautumiki isipokuwa ukitumia HTTPS.

Mipangilio ya programu ya kusimba

Kwa mipangilio ya programu ya kusimba, angalia mwongozo wetu wa jumla kuhusu mipangilio, kasi ya biti na ubora. Mipangilio ya ziada ya HLS ambayo ni tofauti na RTMP ni pamoja na:

  • Kodeki ya video: pia hutumia HEVC pamoja na H.264
  • Kodeki ya sauti: AAC, AC3 na EAC3

Mipangilio ya kina inayopendekezwa

  • Kasi ya sampuli ya sauti: KHz 44.1 kwa sauti ya stereo, KHz 48 kwa sauti inayozingira ya 5.1
  • Kasi ya biti ya sauti: Kbps 128 kwa stereo au Kbps 384 kwa sauti inayozingira ya 5.1

Programu za kusimba zinazotumia maudhui ya HLS

  • Programu za kusimba za Cobalt
  • Harmonic
  • Kitendo cha Mirillis: Kodeki ya video ya HEVC ikichaguliwa, uingizaji wa HLS utatumiwa kiotomatiki.
  • OBS
  • Telestream

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
331283793127151014
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false