Video Fupi za YouTube ni njia ya mtu yeyote kugeuza wazo kuwa fursa ya kuwasiliana na hadhira mpya popote ulimwenguni. Unachohitaji ni simu mahiri na kamera ya Video Fupi iliyojumuishwa kwenye programu ya YouTube ili kutayarisha Video Fupi zilizo na urefu wa hadi dakika tatu. Zana mpya kabisa za utayarishaji wa Video Fupi hufanya kuwa mtayarishi kwenye YouTube iwe jambo rahisi, la haraka na la kufurahisha. Boresha Video zako Fupi za YouTube.
Kutayarisha Video fupi
✨MPYA✨ Kuweka VIUNGO🔗 kwenye VIDEO ZAKO FUPI🩳
Kutayarisha Video fupi ukitumia zana za YouTube za kutayarisha video za muundo mfupi hukuruhusu kurekodi klipu moja au zaidi zenye jumla ya hadi dakika tatu. Wakati unarekodi ukitumia Kamera ya Video Fupi, tumia upau wa shughuli katika sehemu ya juu ya skrini ili uone idadi ya sehemu ulizorekodi na urefu wa kila rekodi.
- Ingia katika programu ya YouTube
.
- Gusa Buni
kisha uchague Video fupi.
- Shikilia Rekodi
au uiguse ili uanze kurekodi kisha uiguse tena ili uache.
- Kumbuka: Unaweza kubadilisha urefu katika kona ya juu kulia.
- Ukimaliza kurekodi, unaweza:
- Kuweka muziki, kuweka madoido au kutumia madoido mengine ili kuboresha rekodi yako.
- Kugusa Tendua
ili uondoe klipu ya video uliyorekodi au kugusa Rejesha
ili uiweke tena.
- Kugusa Funga
Futa au Hifadhi kisha uondoke. Kuhifadhi rasimu katika hatua hii kutahifadhi mabadiliko yoyote uliyofanya.
- Gusa Nimemaliza
. Ukiwa hapa, unaweza:
- Kukagua video yako.
- Kuweka sauti, kipengele cha kusoma maandishi kwa sauti na madoido mengine.
- Kugusa Rudi nyuma
ili urudi kwenye skrini ya kurekodi.
- Gusa Endelea ili uweke maelezo kwenye video yako.
- Kwenye skrini hii, weka jina (lisizidi herufi 100) kisha uchague mipangilio, kama vile faragha ya video.
- Gusa Onyesha zaidi
ili uone maelezo ya ziada.
- Kumbuka: Mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video kwa watayarishi walio na umri wa kati ya miaka 13 hadi 17 ni ya faragha. Iwapo una umri usiopungua miaka 18, mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video hubainishwa kuwa ya umma. Kila mtu anaweza kubadilisha mipangilio hii ili afanye video yake iwe ya umma, ya faragha au ambayo haijaorodheshwa.
- Gusa Onyesha zaidi
- Kupata maoni: Gusa kitufe cha Pata maoni ili upate uchanganuzi wa kivutio cha video yako, kasi na mengineyo.
- Gusa Chagua hadhira
“Ndiyo, inalenga watoto" au "Hapana, hailengi watoto" ili uchague hadhira yako. Pata maelezo zaidi kuhusu video zinazolenga watoto.
- Kwenye skrini hii, weka jina (lisizidi herufi 100) kisha uchague mipangilio, kama vile faragha ya video.
- Gusa Pakia Video fupi ili uchapishe Video yako fupi au Hifadhi rasimu ili uihifadhi kama rasimu uichapishe baadaye.
Kutayarisha Video fupi ukitumia kipengele cha 'Tumia AI kuhariri'
JINSI YA: Kutumia AI kuhariri kwenye Video Fupi za YouTube
Kumbuka: Kwa sasa kipengele hiki hakipatikani katika maeneo yote.
Kipengele cha Tumia AI kuhariri hukusaidia kugeuza video ghafi kuwa video iliyoboreshwa yenye muziki na madoido, hivyo kukupa rasimu bora ya kwanza unayoweza kubadilisha upendavyo. Unaweza kutumia kipengele cha Tumia AI kuhariri kupitia YouTube Create na Kamera ya Video Fupi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia kipengele cha Tumia AI kuhariri kwenye YouTube Create.
- Ingia katika programu ya YouTube
.
- Gusa Buni
kisha uchague Video fupi.
- Katika kona ya chini kushoto, gusa Weka
.
- Chagua video au picha ambazo ungependa kuweka.
- Kumbuka: Unaweza tu kupakia hadi dakika 3 katika vipengee vya jumla na kiwango cha chini cha sekunde 5.
- Gusa Tumia AI kuhariri.
- Chagua muundo wa kuhariri kwenye violezo vinavyopatikana.
- Gusa Endelea.
- Subiri video iliyohaririwa itayarishwe.
- Kagua video iliyotayarishwa. Kagua kisha uguse Endelea.
- Kumbuka: Unaweza kufanya mabadiliko ya ziada ukitumia zana zetu za kuhariri au kubadilisha muziki.
- Ukimaliza, endelea kupakia video yako.
Kuhifadhi Video yako fupi kama rasimu
Unaweza kuhifadhi Video yako fupi kama rasimu kabla ya kuipakia na urudi baadaye ili uihariri.
Hamna kikomo cha idadi ya rasimu unazoweza kuhifadhi kwa wakati mmoja. Kumbuka kuwa rasimu huhifadhiwa kwenye kifaa chako na si kwenye chaneli yako ya YouTube. Ukifuta programu ya YouTube au ukibadilisha kifaa chako, utapoteza rasimu zako.
Ili upate rasimu zako katika programu ya YouTube:
- Gusa Tayarisha
Video fupi.
- Tayarisha Video yako fupi
gusa Endelea.
- Katika kona ya chini kulia, gusa Rasimu.
- Kutoka hapa unaweza kuchagua rasimu ili uihariri au uifute kutoka kwenye kifaa chako.
Kuchagua kijipicha
Jinsi ya KUCHAGUA ✨Vijipicha✨ vya Video zako Fupi
Unaweza kuchagua fremu kwenye Video yako fupi ili itumike kama kijipicha kabla na baada ya kupakia Video zako Fupi. Kumbuka kuwa unaweza tu kubadilisha kijipicha chako kwenye programu ya YouTube na si kwenye Studio.
Ifuatayo ni jinsi ya kuchagua kijipicha cha Video yako fupi:
- Gusa Tayarisha
Video fupi.
- Rekodi Video yako fupi kisha uweke maelezo ya video.
- Nenda kwenye skrini ya mwisho ya kupakia
gusa Hariri
kwenye kijipicha cha video yako.
- Chagua fremu ya kutumia kama kijipicha chako.
- Kidokezo: Unaweza kuweka maandishi na madoido kwenye kijipicha chako. Ukimaliza kuhariri, huwezi kurudi kwenye mabadiliko uliyofanya hapo awali ili uhariri chochote.
- Gusa Nimemaliza.
Ili uhariri kijipicha baada ya kupakia Video fupi:
- Ingia katika programu ya YouTube
.
- Nenda kwenye ukurasa wa chaneli yako
Video zako
.
- Gusa Zaidi
kwenye Video fupi ambayo ungependa kuhariri
Hariri
.
- Chagua fremu ya kutumia kama kijipicha chako.
- Kidokezo: Unaweza kuweka maandishi na madoido kwenye kijipicha chako. Ukimaliza kuhariri, huwezi kurudi kwenye mabadiliko uliyofanya hapo awali ili uhariri chochote.
- Gusa Nimemaliza.