Kutayarisha na kudhibiti Klipu

Unaweza kutayarisha klipu ya sehemu ndogo ya video au mtiririko mubashara na kuituma kwa wengine kwenye mitandao ya kijamii au kupitia mawasiliano ya moja kwa moja, kama vile barua pepe au SMS. Klipu hupatikana kwa umma na zinaweza kutazamwa na mtu yeyote aliye na uwezo wa kufikia klipu ambaye pia anaweza kutazama video halisi. Unaweza kupata klipu ulizotayarisha na klipu zilizotayarishwa kutokana na video zako, kwenye ukurasa wa maktaba ya Klipu Zako. Watayarishi wa video wanaweza kudhibiti klipu zinazotayarishwa kutokana na video zao katika Studio ya YouTube.

Kumbuka: Mipangilio ya kutengeneza klipu za video huwa imewashwa kwa chaguomsingi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuizima.

Klipu za YouTube

Kutayarisha na kutuma klipu

Klipu zina urefu wa kati ya sekunde 5 hadi 60 na huchezwa kwa kurudiwa bila kukoma kwenye ukurasa wa kutazama wa video halisi.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video unayotaka kuitayarishia klipu.
  3. Chagua Menyu ''kisha  Tayarisha klipu
  4. Ipe Klipu yako jina (lisizidi herufi 140).
  5. Teua sehemu ya video ambayo ungependa kutayarishia klipu. Unaweza kuongeza (urefu usiozidi sekunde 60) au kupunguza (urefu usiopungua sekunde 5) urefu wa sehemu uliyochagua kwa kuburuta kitelezi.
  6. Bofya TUMA KLIPU.
  7. Teua chaguo la kushiriki klipu:
    • Pachika: Unaweza kupachika video husika kwenye tovuti.
    • Mitandao jamii: Unaweza kutuma Klipu yako kwenye mtandao jamii kama vile Facebook au Twitter.
    • Nakili kiungo: Unaweza kunakili kiungo cha Klipu yako ili ukibandike mahali pengine.
    • Barua pepe: Unaweza kutuma Klipu yako ukitumia programu chaguomsingi ya barua pepe kwenye kompyuta yako.

Kumbuka: Unaweza kupata klipu ulizotayarisha kwenye maktaba ya Klipu.

Kufuta klipu uliyotayarisha

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye sehemu ya Maktaba.
  3. Gusa Klipu zako.
  4. Tafuta klipu unayotaka kufuta kisha uchague Menyu ''.
  5. Gusa chaguo la "Futa klipu".

Kumbuka: Kufuta klipu kunaiondoa kwenye YouTube. Watumiaji walio na idhini ya kufikia URL ya klipu na watayarishi ambao wanamiliki video halisi iliyotumiwa kutayarisha klipu, hawataweza kufikia klipu hiyo tena.

Kuwazuia watazamaji kutayarisha klipu ya maudhui yako

Unaweza kuzuia hadhira yako dhidi ya kutayarisha na kushiriki klipu za video yako.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, bofya Mipangilio.
  3. Chagua Chaneli kisha Mipangilio ya Kina.
  4. Kwenye Klipu, batilisha uteuzi Ruhusu watazamaji watayarishe klipu ya maudhui yangu.

Kumbuka: Unaweza pia Kuweka watumiaji kwenye orodha ya “Watumiaji waliofichwa” ya chaneli yako ili uwazuie kutayarisha klipu za video au mitiririko yako mubashara. Unaweza pia Kuweka maneno kwenye orodha yako ya maneno yaliyozuiwa ili uyazuie yasitumiwe kwenye majina ya klipu za video na mitiririko yako mubashara.

Kudhibiti klipu za video zako

Unaweza kudhibiti Klipu zilizotayarishwa kutokana na video zako katika Studio ya YouTube.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, bofya Maudhui.
  3. Chagua jina au kijipicha cha video.
  4. Kwenye Menyu ya kushoto, bofya Klipu .
  5. Unaweza kutazama, kucheza, kutuma, kuficha na kuripoti Klipu zako.

Kudhibiti sehemu ya "Klipu maarufu za jumuiya"

Unaweza kuonyesha klipu maarufu za video zako kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. Klipu hizi zinaweza kutayarishwa na wewe au watazamaji wako. Zikishawekwa kwenye kichupo chako cha Ukurasa wa kwanza, klipu hizo huonekana kwa umma na kupangwa kulingana na umaarufu na jinsi zilivyotayarishwa hivi majuzi.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, bofya Kuweka mapendeleo .
  3. Chini ya “Sehemu zinazoangaziwa,” bofya Weka Sehemu .
  4. Washa au zima   ”Klipu maarufu za jumuiya.” 
  • Kidokezo: Unaweza kuweka rafu kwa kuiburuta juu na chini.

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)

Sioni jinsi ya kutengeneza Klipu kwenye YouTube.

Ili utengeneze klipu kutoka kwenye video au mtiririko mubashara katika YouTube, ni lazima:

  • Uwe umeingia katika akaunti.
  • Utengeneze Klipu kutoka kwenye chaneli inayotimiza masharti na ambayo imejumuishwa. Chaneli pia inaweza kuzima kipengele cha kutengeneza Klipu kwenye maudhui yake.

Huwezi kutengeneza klipu kutoka kwenye:

  • Video zenye urefu wa chini ya dakika 2
  • Video zinazolenga watoto
  • Mitiririko mubashara bila DVR
  • Mitiririko mubashara yenye urefu wa zaidi ya saa 8
  • Maonyesho ya kwanza yakiwa bado yanaendelea
  • Video zilizobuniwa kutoka kwenye chaneli za habari

Je, ni nani anayeweza kuona klipu nilizotayarisha?

Klipu hupatikana kwa umma na zinaweza kutazamwa na kutumwa na mtu yeyote anayeweza kufikia Klipu ambaye pia anaweza kutazama video halisi. Watayarishi wanaomiliki video halisi wanaweza kufikia Klipu zote zilizotayarishwa kutoka kwenye video hiyo, katika ukurasa wa Maktaba na katika Studio ya YouTube na wanaweza kutazama na kutuma Klipu za video hiyo. Klipu inaweza pia kuonekana kwenye mifumo mahususi ya utafutaji, ugunduzi na takwimu inayopatikana kwa watazamaji na watayarishi kwenye YouTube.

Kwa nini klipu nilizotayarisha hazipatikani tena?

Iwapo video halisi itafutwa au kuwekwa kuwa ya faragha, basi Klipu za video hiyo hazitapatikana. Iwapo video itabainishwa kuwa haijaorodheshwa, basi Klipu za video hiyo bado zitapatikana.

Iwapo video ya asili inakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, basi Klipu zilizotengenezwa kutoka kwenye video hiyo zitaondolewa.

Nilitengeneza klipu kutoka kwenye mtiririko mubashara na haifanyi kazi.

Klipu zitaonekana baada ya mtiririko mubashara kukamilika na kupakiwa kama video. Huwezi kubuni Klipu kutoka kwenye mitiririko mubashara bila DVR au mitiririko mubashara mirefu kuliko muda wa DVR. Pata maelezo kuhusu jinsi ya Kuwasha DVR kwenye mitiririko mubashara.

Iwapo mtiririko mubashara utadumu zaidi ya muda wa DVR, klipu zozote ambazo ziko nje ya muda wa DVR hazitaweza kuchezwa hadi mtiririko huo mubashara ukamilike na video husika ichapishwe.

Je, ninaweza kutayarisha Video Fupi kutokana na Klipu?

Ndiyo, unaweza kuandaa mseto wa klipu iwapo video chanzo ya klipu pia imetimiza masharti ya kuandaa mseto. Zana zote za kuandaa mseto unazoweza kupata kwenye video unaweza pia kuzipata kwenye klipu yoyote ya video hiyo, pata maelezo zaidi hapa.

Watayarishi wanaomiliki video chanzo ya klipu wanaweza kugeuza klipu nzima kuwa Video Fupi, pata maelezo zaidi hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14818020851025651528
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false