Kuanza kutumia akaunti zinazodhibitiwa

Wazazi wanaoamua kuwa mtoto wao aliye na umri chini ya miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi au eneo waliko) yuko tayari kutazama maudhui kwenye YouTube wanaweza kuweka mipangilio ya akaunti inayodhibitiwa. Akaunti zinazodhibitiwa zimeunganishwa kwenye Akaunti ya Google ya mzazi mwenyewe.

Mzazi anapoweka akaunti inayodhibitiwa, anachagua mipangilio ya maudhui ambayo inazuia video na muziki ambao watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 wanaweza kucheza. Pata maelezo zaidi kuhusu akaunti zinazodhibitiwa.

Jinsi ya kuweka mipangilio ya matumizi yanayosimamiwa kwa ajili ya mtoto wako kwenye YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Fungua akaunti inayodhibitiwa

Kabla ya kufungua akaunti inayodhibitiwa, hakikisha kuwa umemfungulia mtoto wako Akaunti ya Google.

Chagua mojawapo ya chaguo hizi ili kufungua akaunti inayodhibitiwa:

Chaguo la 1: Kwenye YouTube au YouTube Music katika kifaa cha mzazi

  1. Kwa kutumia Akaunti ya Google unayotumia ukiwa msimamizi wa akaunti ya mtoto wako, ingia katika mojawapo ya akaunti zifuatazo:

2. Nenda kwenye picha ya wasifu wako 

3. Chagua Mipangilio .

4. Chagua Mipangilio ya Wazazi.

5. Chagua mtoto wako kisha fuata hatua zinazofuata.

Chaguo la 2: Kwenye YouTube au YouTube Music katika kifaa cha mtoto

  1. Ingia katika programu kuu ya YouTube, programu ya YouTube Music au programu ya YouTube kwenye Televisheni Inayoweza Kuunganisha kwenye Intaneti au kifaa cha kutiririsha maudhui. Tumia Akaunti ya Google ya mtoto wako ambayo imeunganishwa na yako.
  2. Chagua ANZA kisha ufuate hatua zinazofuata.
    • Kumbuka: Utahitaji kuweka nenosiri lako la Akaunti ya Google ili kutoa ruhusa.

Chaguo la 3: Kwenye families.youtube.com katika wavuti

  1. Nenda kwenye families.youtube.com.
  2. Ingia katika Akaunti ya Google unayotumia ukiwa msimamizi wa akaunti ya mtoto wako.
  3. Chagua mtoto kutoka kwenye kikundi chako cha familia na ufuate hatua zinazofuata.

Chaguo la 4: Kwenye programu ya Family Link

  1. Ingia katika akaunti ya programu yako ya Family Link Family Link.
  2. Chagua mtoto wako.
  3. Chagua Vidhibiti kisha Vizuizi vya maudhui kisha YouTube kisha YouTube na YouTube Music.
  4. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini.

Anzisha hali ya matumizi yanayosimamiwa

Ili kuanza matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube:

  1. Sasisha programu: Iwapo mtoto wako anatumia kifaa cha mkononi, hakikisha kwamba programu zake zote za YouTube zimesasishwa.
  2. Ingia katika akaunti: Ingia katika akaunti ya mtoto wako kwenye YouTube kupitia vifaa vyote anavyotumia.

Kuna mipangilio na vidhibiti kadhaa vya wazazi vinavyopatikana kwa ajili ya matumizi yanayosimamiwa ya mtoto wako.

Vidokezo:

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5121367210917581339
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false