Chanzo cha hadhira kisicho sahihi kwenye video zako

Chanzo cha hadhira kisicho sahihi ni shughuli yoyote kwenye chaneli yako ambayo haitoki kwa mtumiaji halisi au mtumiaji aliyevutiwa kihalali. Inaweza kujumuisha njia za ulaghai, bandia au zisizokusudiwa ili kuongeza mapato ya matangazo ya video, pamoja na nyinginezo.

Mifano ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi kwenye video inajumuisha:

  • Vyanzo vya uonekanaji wa matangazo vinavyolipiwa au vya kiotomatiki kutoka kwa wengine, ikiwa ni pamoja na huduma za “kuongeza watazamaji” na nyingine zinazodai kuwa mitandao halali ya matangazo, pamoja na nyinginezo.
  • Marafiki au watu unaowasiliana nao wanaoruhusu orodha za kucheza za video zako zicheze siku nzima, hivyo kusababisha kuongezeka kwa utazamaji matangazo kutokana na matangazo kucheza kwenye video hizo.
  • Kuwatangazia watazamaji wako kuwa wanapaswa kutazama au kubofya matangazo kwenye video fulani ili kuongeza utazamaji wa matangazo, hivyo kuongeza mapato ya matangazo.

Mifumo yetu inatathmini utazamaji wa video zako ili kubaini ikiwa ni sahihi au si sahihi, bila kujali chanzo cha watazamaji ni kipi na kimepatikanaje. Ni muhimu tushughulikie haraka chanzo cha hadhira kisicho sahihi ili kuhakikisha mfumo unaendelea kuwafaa watayarishi, watangazaji na watazamaji. Kwa kuendelea kulinda mifumo yetu ya utangazaji dhidi ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi, watazamaji wanaweza kuendelea kuwekeza kwa uhakika kwenye mfumo, hali ambayo inawasaidia watayarishi kuchuma mapato kupitia maudhui bora wanayotayarisha. 

Muda mwingine, watayarishi wanaweza kubaini kuwa chaneli zao zinaathiriwa na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi, hata kama hawaviongezi kwa makusudi. Hii humaanisha kuwa kuna muda ambapo watayarishi huenda wasifahamu kwamba shughuli wanazopokea zinatokana na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi.

Ingawa tunajitahidi kujaribu kuzuia hali hii, baadhi ya aina za vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vinaweza tu kutambuliwa na mifumo yetu baada ya kutokea. Kwa hivyo, marekebisho yanafanyika katika idadi ya utazamaji na mapato kwenye Takwimu za YouTube na AdSense katika YouTube. Unapoona marekebisho haya, inamaanisha kuwa mifumo yetu ya ulinzi dhidi ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi inafanya kazi kulinda mfumo, hata kama hukuzalisha au kuongeza vyanzo hivyo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha hadhira kisicho sahihi, angalia Mijadala ya Usaidizi ya Jumuiya ya YouTube.

Jinsi vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vinavyoathiri mapato yako

Ikiwa vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vitatokea kwenye chaneli yako, huenda ukaona:

  • Kupungua kwa idadi ya utazamaji na mapato. Huenda ukaona marekebisho kwenye Takwimu za YouTube ya kuondoa idadi ya utazamaji na hivyo mapato yanayohusiana na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi.  
  • Matangazo machache kwenye chaneli yako. Huenda tukaweka mipaka kwenye uonyeshaji wa matangazo kwa muda mfupi hadi mifumo yetu itakapobaini kupungua kwa hatari ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi, hali inayoweza kuathiri mapato hata kama idadi ya utazamaji iko vile vile.
  • Marekebisho kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Ikiwa tutabaini mapato yanayohusiana na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi baada ya kulipa au kukokotoa malipo yako, kiasi hicho kitapunguzwa kwenye salio lako la AdSense katika YouTube la sasa au la baadaye.
  • Kuchelewa kwa malipo. Huenda malipo yakachelewa kwa hadi siku 90 ili kutoa muda wa kutosha wa kuchunguza vyanzo vya hadhira na mapato yanayohusiana kwenye chaneli yako. Huenda mapato yakazuiwa, kurekebishwa au kupunguzwa yakibainika kuwa si sahihi.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vinavyoweza kuathiri mapato yako yaliyokadiriwa katika Takwimu za YouTube.

Vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vinapobainika, watangazaji hawatozwi au kurejeshewa pesa inapofaa na inapowezekana. 

Mapato yako ya AdSense katika YouTube yatakatwa kabla ya malipo ili kuondoa mapato yanayotokana na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi. Mapato yoyote ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi yataonekana kama kipengee tofauti katika Ukurasa wa malipo kwenye AdSense katika YouTube. 

Katika hali ambapo shughuli muhimu kwenye chaneli zinaonekana kuwa si sahihi, akaunti ya AdSense katika YouTube inayohusiana huenda ikasimamishwa au ikafungwa kabisa. Watayarishi watakuwa na chaguo la kukata rufaa akaunti zao za AdSense katika YouTube zinapofungwa. Hali ya ukiukaji inaweza pia kusababisha kipengele cha uchumaji wa mapato kizimwe kwenye akaunti zako zozote kwa mujibu wa sera zetu za uchumaji wa mapato wa chaneli katika YouTube. Iwapo unafikiri kuwa tumekosea, unaweza kukata rufaa. Ukiukaji huo ukibatilishwa, unaweza kutuma ombi la uchumaji wa mapato mara tu utakapotimiza masharti katika Studio ya YouTube.

Vidokezo vya kuzuia chanzo cha hadhira kisicho sahihi

Ikiwa vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vitatokea kwenye chaneli yako, kagua vidokezo hivi ili upate mbinu za kawaida za kukusaidia uzuie hali hii: 

  1. Epuka kushirikiana na wahusika usiowaamini unapotayarisha video zako na kukuza chaneli yako. Kwa mfano, ni vyema uepuke huduma zinazodai kukuongezea idadi ya utazamaji, alama za imenipendeza au usajili. Hata kama huduma za wengine zinapodai zinaongeza watazamaji halisi kwenye chaneli yako, huenda ikawa ni mchakato bandia, hivyo kusababisha vyanzo vya hadhira visivyo sahihi. 
  2. Usibofye matangazo kwenye video zako, hata wakati unafikiri inaweza kuwa SAWA kufanya hivyo. Mifumo yetu hutambua watayarishi wanapobofya matangazo kwenye video zao wenyewe. Hali hii ikijirudia kwa kipindi fulani, akaunti yako inaweza kufungwa ili kulinda watangazaji na mfumo wa watayarishi.
  3. Kamwe usimuhimize yeyote kubofya matangazo yako ili kukusaidia kuchuma mapato zaidi, hata wakati unafanya hivyo kwa lengo zuri au kutoa msaada.
Pata maelezo zaidi kuhusu vidokezo vya kuzuia chanzo cha hadhira kisicho sahihi kwenye Kituo chetu cha Usaidizi.

Nyenzo

Kumbuka: Aikoni za njano huwekwa kwenye video kulingana na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Haziwekwi kulingana na sera hii dhidi ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13145958065780833049
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false