Kutiririsha video ya HDR kwenye YouTube

Unaweza kutiririsha video ya HDR kwenye YouTube Moja kwa Moja. HDR hukuruhusu uonyeshe rangi zinazorindima na halisi kwa watazamaji wako wanaotumia idadi inayoongezeka ya vifaa vinavyotumia HDR.

Ili utiririshe HDR kwenye YouTube Moja kwa Moja, unahitaji kutayarisha maudhui yanayooana ya HDR na utumie programu oanifu ya kusimba. Wakati huu, utiririshaji wa HDR kwenye YouTube unatumika tu kwenye kodeki ya video ya H.265 (HEVC).

Kutiririsha mubashara maudhui ya michezo ya video ya HDR

Ili utiririshe mubashara maudhui ya michezo ya video ya HDR, unahitaji:

  • Kucheza mchezo unaotumia kifaa cha HDR.
  • Kuwasha HDR kwenye mipangilio ya mchezo.
  • Kutumia skrini au TV inayotumia HDR.
  • Kutumia programu oanifu ya kusimba.

Kutiririsha mubashara maudhui mengine ya video ya HDR

Ili utiririshe mubashara maudhui mengine ya video ya HDR, unahitaji

  • Kutumia programu oanifu ya kusimba.
  • Kutumia kamera inayotumia video ya HDR yenye viwango vya rangi ya PQ au HLG. Angalia mwongozo wa kamera yako ili uone ikiwa viwango hivi vinatumika.

Kutazama mitiririko mubashara ya HDR

Watazamaji wataona mtiririko wako katika HDR kiotomatiki kwenye vifaa vinavyotumika. Watazamaji kwenye vifaa vingine wataona mtiririko wako katika Kiwango cha Kawaida Kinachobadilika. Vifaa vya HDR vinavyotumika vinajumuisha:

  • Programu ya YouTube kwenye TV za HDR.
  • Kutuma maudhui kwenye vifaa vya Chromecast Ultra vilivyounganishwa na TV za HDR.
  • Vifaa vya mkononi vya Android vyenye skrini ya HDR.
  • Kompyuta binafsi za Mac na Windows zinazotumia picha za HDR na skrini ya HDR. Watazamaji wataona mtiririko wako kwenye HDR ikiwa wameruhusu HDR katika mipangilio ya kompyuta yao.

Kumbuka Toleo tangulizi katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja litaonyesha rangi za HDR.

Jinsi ya kujua ikiwa unatazama katika HDR

Mitiririko ya HDR itaonyesha “HDR” katika menyu ya mipangilio ya ubora wa video, kwa kawaida hupatikana kwenye sehemu ya chini kulia ya skrini yako. Ikiwa kifaa chako hakitumii HDR, hutaona beji ya HDR na mtiririko utaonyeshwa kwenye SDR.

Kuweka mipangilio ya Mtiririko wa HDR kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja wa YouTube

Unaweza kutumia RTMP(S) au HLS ili kutiririsha katika HDR. Kumbuka kwamba utahitaji kuacha kuchagua mipangilio ya “Washa ubora mwenyewe”.

Ili uanzishe mtiririko wa HDR kupitia HLS, utahitaji kuweka itifaki ya ufunguo wako wa mtiririko kuwa HLS. Pata maelezo zaidi.

Programu oanifu za kusimba za RTMP

OBS

Ili uwashe HDR kwenye OBS (toleo la chini zaidi ni 30.1)
  1. Unapofungua OBS, kompyuta yako lazima iwe na angalau chanzo kimoja cha HDR. Ukiwa na skrini ya HDR, kwenye Windows 11, unaweza kuwasha HDR hata ikiwa video chanzo si HDR kupitia kipengele cha HDR ya Kiotomatiki.
  2. Kwenye Mipangilio, nenda kwenye Mtiririko na uchague YouTube RTMPS.
  3. Kwenye Mipangilio, nenda kwenye Kifaa kisha bofya Programu ya kusimba.
  4. Chagua programu yako ya kusimba ya maunzi ya HEVC. 
  5. Chini ya Mipangilio ya Programu ya kusimba, badilisha Wasifu wako kuwa Main 10 (wasifu chaguomsingi ni Main).
  6. Katika Mipangilio bofya Ya kina. Washa HDR na ubadilishe Muundo wa Rangi uwe P010 (4:2:0).
  7. Badilisha Nafasi ya Rangi iwe Rec 2100 PQ au HLG (Tunapendekeza HLG).

 

Programu oanifu za kusimba za HLS

Avermedia RECentral 4

AWS Elemental Live 

Mirillis Action!

Ili usimbe HDR ukitumia Mirillis Action!, tumia toleo la 4.12.2 au toleo jipya zaidi na mojawapo ya kadi zifuatazo za picha zinazooana.

  • NVIDIA GeForce GTX 10-series au toleo jipya zaidi.
  • AMD Radeon RX 5700 au toleo jipya zaidi.
  • Picha za toleo la 10 la Intel au toleo jipya zaidi.

Ili uweke mipangilio ya Mirillis Action! ifanye kazi na HDR ya YouTube Moja kwa Moja:

  1. Kuanzia kwenye Action!, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti yako ya YouTube.
  2. Nenda kwenye kichupo cha kurekodi video katika Action!
  3. Hakikisha kuwa ufunguo wako wa mtiririko unatumia itifaki ya HLS na uteuzi wa kipengele cha “Washa mipangilio unayoweka mwenyewe” uwe umebatilishwa (kwa chaguomsingi).
  4. Kwenye kichupo cha “Kutiririsha Mubashara”, chagua YouTube kama huduma ya kutiririsha maudhui.
  5. Action! itatayarisha upelekaji unaotawanya kiotomatiki unapoanza kutiririsha.

Unaweza kutayarisha na kudhibiti upeperushaji wako katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.

  1. Nenda kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
  2. Tayarisha au dhibiti mtiririko mubashara.
  3. Hakikisha kuwa ufunguo wako wa mtiririko umewekwa ili utumie HDR na uteuzi wa kipengele cha “Washa mipangilio unayoweka mwenyewe” uwe umebatilishwa (kwa chaguomsingi).
  4. Nakili ufunguo wako wa mtiririko.
  5. Kwenye Action!, chagua huduma Maalum ya kutiririsha maudhui.
  6. Chini ya “Seva au URL,” weka URL ifuatayo na ubadilishe STREAMKEY ukitumia ufunguo wako wa mtiririko wa YouTube:
    https://a.upload.youtube.com/http_upload_hls?cid=STREAMKEY&copy=0&file=
  7. Acha mipangilio ya tenganisha “Ufunguo wa mtiririko” bila kujazwa.

Kumbuka: Huenda Action! isioane na baadhi ya michezo ya zamani ya HDR.

Kumbuka: Unaweza tu kusimba katika miundo inayotumika katika kifaa chako.

OBS

Ili uwashe HDR katika OBS

  1. Unapofungua OBS, kompyuta yako lazima iwe na angalau chanzo kimoja cha HDR. Ukiwa na skrini ya HDR, kwenye Windows 11, unaweza kuwasha HDR hata ikiwa video chanzo si HDR kupitia kipengele cha HDR ya Kiotomatiki.
  2. Katika Mipangilio nenda kwenye Mtiririko na uchague YouTube HLS ( “onyesha yote” na uende chini kwenye orodha).
  3. Kwenye Mipangilio, nenda kwenye Kifaa kisha bofya Programu ya kusimba.
  4. Chagua programu yako ya kusimba ya maunzi ya HEVC. 
  5. Chini ya Mipangilio ya Programu ya kusimba, badilisha Wasifu wako kuwa Main 10 (wasifu chaguomsingi ni Main).
  6. Katika Mipangilio bofya Ya kina. Washa HDR na ubadilishe Muundo wa Rangi uwe P010.
  7. Badilisha Nafasi ya Rangi iwe Rec 2100 PQ au HLG (Tunapendekeza HLG).

Programu za kusimba za maunzi yanayooana

Masharti ya kawaida ya mipangilio ya programu ya kusimba

HDR ya YouTube Moja kwa Moja inahitaji kutumia tokeo la HLS. Yafuatayo ni masharti ya kawaida ya kuweka mipangilio ya programu ya kusimba katika kifaa chako:

Mipangilio ya HDR:

  • Kodeki ya Video: HEVC (unaweza tu kusimba katika miundo inayotumika katika kifaa chako)
  • Kina cha Biti: Biti 10
  • Misingi ya Rangi: BT.2020 (ni lazima ioane na chanzo chako)
  • Sifa za Uhamishaji: ST 2084 PQ au HLG, kulingana na inayozalishwa na chanzo chako.
  • Vizidishi vya Solo: Ung'aavu Unaobadilika wa BT.2020 (ni lazima ioane na chanzo chako)

Tokeo la HLS:

  • Muda wa Sehemu: Kati ya sekunde 1 hadi 4.
  • Muundo wa Sehemu: Sharti uwe TS (Mtiririko wa Usafirishaji).
  • Kipindi cha Baiti hakitumiki.
  • Ni sharti utumie orodha endelevu yenye sehemu zisizozidi 5 zinazosubiri kushughulikiwa.
  • Ni sharti utumie HTTPS POST/PUT.
  • Usimbaji kwa njia fiche hautumiki isipokuwa ukitumia HTTPS.
  • URL: Weka URL ifuatayo na ubadilishe STREAMKEY ukitumia ufunguo wako wa mtiririko wa YouTube. Kwa HDR, lazima utumie ufunguo wa mtiririko ambao una HLS kama itifaki ya kutiririsha na uteuzi wa mipangilio ya “Washa mipangilio unayoweka mwenyewe” uwe umebatilishwa (kwa chaguomsingi).
  • Ikiwa unatumia uingizaji (wa data) mbadala, URL ni: https://b.upload.youtube.com/http_upload_hls?cid=STREAMKEY&copy=1&file=
Cobalt

Programu za kusimba za Cobalt zinazotumia HDR ya HEVC zinaoana na HDR ya YouTube Moja kwa Moja. Angalia mwongozo wa bidhaa wa muundo wako mahususi wa Cobalt ili uone kama unaruhusu HDR ya HEVC.

Kuweka mipangilio ya Cobalt ya HDR ya HEVC

  1. Weka mipangilio ifuatayo kwenye programu ya kusimba ya Cobalt:
    1. Hali ya programu ya kusimba: HEVC (unaweza tu kusimba katika miundo inayotumika katika kifaa chako)
    2. Kina cha Biti: Biti 10
    3. Hali ya chroma: 4:2:0

  1. Kwenye ukurasa wa “Ya kina”, weka chaguo za aina ya ishara ya video ziwe za aina sawa ya HDR na kamera yako ya HDR au kifaa kingine cha kurekodi. HDR ya YouTube Moja kwa Moja inaruhusu mipangilio iliyoorodheshwa hapa pekee. Angalia mwongozo au mipangilio ya kamera yako ya HDR ili uone ikiwa inaoana na mipangilio hii ya Cobalt.
    1. Washa Aina ya Ishara ya Video: Imechaguliwa
    2. Kiwango Kamili cha Video: Washa ikiwa tu chanzo chako kinatoa video ya kiwango kamili.
    3. Misingi ya Rangi: Weka iwe BT.2020 (ni lazima ioane na chanzo chako)
    4. Sifa za Uhamishaji: Weka iwe ST 2084 PQ au HLG, kulingana na inayozalishwa na chanzo chako.
    5. Vizidishi vya Solo: Weka iwe Ung'aavu Unaobadilika wa BT.2020 (ni lazima ioane na chanzo chako.

  1. Inayofuata, weka tokeo la HLS kwenye YouTube. Nenda kwenye kichupo cha “Tokeo” na uweke mipangilio hii:
    1. Itifaki ya Tokeo: “HLS”
    2. Mahali Seva Inapotumika: Mbali
    3. Itifaki ya Uhamishaji: HTTP/S
    4. Pakia URL: https://a.upload.youtube.com/http_upload_hls?cid=STREAMKEY&copy=0&file=

Katika URL iliyo hapo juu, badilisha STREAMKEY ukitumia ufunguo wako wa mtiririko wa YouTube. Kwa HDR, lazima utumie ufunguo wa mtiririko ambao una HLS kama itifaki ya kutiririsha na uteuzi wa mipangilio ya “Washa mipangilio unayoweka mwenyewe” uwe umebatilishwa (kwa chaguomsingi).

  1. Washa Kijajuu cha Seva Pangishi: Kimebatilishwa
  2. Jina la Faili ya Msingi: “limechapishwa”
  3. Sehemu (sek): Namba yoyote kati ya 1 hadi 4
  4. Idadi ya Sehemu: Teua chaguo lolote
  5. Jina la Programu: Usilibadilishe

Telestream

Programu ya kusimba ya Mtiririko Mubashara ya Lightspeed kutoka Telestream inaoana na HDR ya YouTube Moja kwa Moja.

Fuata maagizo katika mwongozo wa watumiaji wa programu ya kusimba ili uweke mipangilio ya Chaneli ya HLS ukitumia mipangilio ifuatayo:

  • Muda wa Sehemu: Kati ya sekunde 1 na 4.
  • Muundo wa Sehemu: Sharti uwe TS (Mtiririko wa Usafirishaji)
  • Washa Kiwango cha Baiti: Si kweli
  • Aina ya Orodha: Inaendelea kuboresha
  • Vipengee: 5
  • Usimbaji fiche: Hamna
  • Mahali pa Tokeo: Tuma kwenye Mtandao wa Kuwasilisha Maudhui
  • Sehemu ya Kuchapisha: https://a.upload.youtube.com/http_upload_hls?cid=STREAMKEY&copy=0&file=

Katika URL iliyo hapo juu, badilisha STREAMKEY ukitumia ufunguo wako wa mtiririko wa YouTube. Kwa HDR, lazima utumie ufunguo wa mtiririko ambao una HLS kama itifaki ya kutiririsha na uteuzi wa mipangilio ya “Washa mipangilio unayoweka mwenyewe” uwe umebatilishwa (kwa chaguomsingi).

  • Mbinu ya HTTP: Ruhusu mbinu ya HTTP kisha uchague CHAPISHA

Ili uweke mipangilio ya HDR, unahitaji uweke mipangilio ya HEVC katika sehemu ya Programu ya kusimba ya kifaa chako ukitumia mipangilio hii:

  1. Ruhusu biti 10 kisha uwashe metadata ya HDR.
  2. Misingi ya Rangi: Weka iwe BT2020 (ni lazima ioane na chanzo chako).
  3. Sifa za Uhamishaji: Weka iwe SMPTE-ST-2084 (PQ) au ARIB-STD-B67 (HLG), kulingana na inayozalishwa na chanzo chako.
  4. Vizidishi vya Solo: Weka iwe BT2020NC (ni lazima kioane na chanzo chako).

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12854435678489707249
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false