Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha, kubadilisha, kudhibiti na kuchuja orodha zako za video kwenye Studio ya YouTube ili kushirikisha hadhira yako.
Kutayarisha orodha
Ili uunde orodha mpya,
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Katika kona ya juu kulia, bofya UNDA Orodha mpya.
- Weka jina la orodha.
- Tumia kisanduku kunjuzi kuchagua mipangilio ya uonekanaji wa orodha yako.
- Bofya TUNGA.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha podikasti kwenye Studio ya YouTube hapa chini au tembelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi.
- Majina ya orodha hayapaswi kuzidi herufi 150
- Majina ya orodha hayawezi kuwa na herufi zisizoruhusiwa ("<", ">", na kitenganishi cha mstari "\u2028")
- Maelezo ya orodha hayapaswi kuzidi herufi 5,000
- Maelezo ya orodha hayapaswi kuwa na herufi zisizoruhusiwa ("<", ">" na kitenganishi cha mstari "\u2028")
Kudhibiti orodha
Ili udhibiti orodha yako,
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Bofya kichupo cha Orodha.
- Bofya Menyu iliyo karibu na orodha ambayo ungependa kusasisha.
- Chagua Badilisha kwenye YouTube. Orodha yako itafunguka katika kichupo kipya.
- Ili upange video kwenye orodha, buruta na udondoshe video kwenda juu na chini ili upange upya .
- Ili ushiriki orodha, nenda kwenye maelezo yako ya orodha na uchague Shiriki . Kisha, uchague unakotaka kushiriki orodha.
- Ili uweke washiriki, nenda kwenye maelezo yako ya orodha na ubofye Zaidi Shirikiana .
- Ili uweke video kwenye orodha, nenda kwenye maelezo ya video zako na uchague Zaidi Weka video. Unaweza kuweka video kutoka sehemu ya utafutaji, URL au maktaba yako.
Kubadilisha jina au maelezo ya orodha
Ili usasishe maelezo ya orodha yako,
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Bofya kichupo cha Orodha.
- Bofya Maelezo karibu na jina au maelezo ya orodha yako kisha usasishe jinsi unavyotaka.
- Bofya HIFADHI.
Kidokezo:
- Majina ya orodha hayapaswi kuzidi herufi 150
- Majina ya orodha hayawezi kuwa na herufi zisizoruhusiwa ("<", ">", na kitenganishi cha mstari "\u2028")
- Maelezo ya orodha hayapaswi kuzidi herufi 5,000
- Maelezo ya orodha hayapaswi kuwa na herufi zisizoruhusiwa ("<", ">" na kitenganishi cha mstari "\u2028")
Kuchuja orodha
Ili upate orodha kwa urahisi, tumia kichujio kufanya utafutaji wako uwe mahususi zaidi:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya Kushoto, chagua Maudhui.
- Bofya kichupo cha Orodha.
- Tumia upau wa kuchuja kisha uweke maneno muhimu ili upate na uchuje orodha zako kulingana na jina.
Kubadilisha orodha iwe podikasti
Ili ubadilishe orodha iliyopo iwe podikasti,
- Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui Orodha.
- Wekelea kiashiria juu ya orodha unayotaka kuifanya iwe podikasti.
- Bofya Menyu Ifanye iwe podikasti.
- Kagua maelezo ya podikasti yako na uweke kijipicha cha mraba mdogo cha podikasti. Maelezo ya podikasti yanajumuisha jina, maelezo na anayeweza kutazama podikasti yako kwenye YouTube.
- Bofya Nimemaliza ili uthibitishe mabadiliko uliyofanya.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu kuchapisha na kusambaza podikasti kwenye YouTube, angalia makala yetu ya Kituo cha Usaidizi.
Kuondoa vipengele vya kuchapisha na kusambaza podikasti katika orodha
Ili kuondoa vipengele vya kuchapisha na kusambaza podikasti kutoka kwenye orodha yako,
- Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui Podikasti.
- Wekelea kiashiria juu ya orodha ya kucheza unayotaka kuondoa isiwe podikasti.
- Bofya kwenye Menyu karibu na podikasti unayotaka kuondoa vipengele.
- Chagua Badilisha isiwe podikasti.
- Bofya Ndiyo ili uthibitishe.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu kuchapisha na kusambaza podikasti kwenye YouTube, angalia makala yetu ya Kituo cha Usaidizi.