Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha, kubadilisha, kudhibiti na kuchuja orodha zako za video kwenye Studio ya YouTube ili kushirikisha hadhira yako.
Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.
Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android
Kuweka video kwenye orodha
- Fungua programu ya Studio ya YouTube .
- Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
- Chagua video ambayo ungependa kuweka kwenye orodha.
- Gusa Badilisha .
- Gusa Weka kwenye orodha kisha uchague orodha ambako ungependa kuiweka.
- Gusa Nimemaliza.
- Gusa Hifadhi.
Kuondoa video kwenye orodha
Ili uondoe video mahususi kwenye orodha, fuata hatua hizi:
- Fungua programu ya Studio ya YouTube .
- Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
- Chagua video ambayo ungependa kuondoa kwenye orodha.
- Gusa Badilisha .
- Gusa orodha kisha uache kuteua kisanduku kilicho karibu na jina la orodha mahususi.
- Gusa Nimemaliza.
- Gusa Hifadhi.
Kubadilisha mipangilio ya orodha (mada, maelezo)
Unaweza kubadilisha mada, maelezo, faragha na mpangilio wa video katika orodha ukitumia programu ya Studio ya YouTube.
- Fungua programu ya Studio ya YouTube .
- Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
- Katika kichupo cha Orodha, chagua orodha ambayo ungependa kubadilisha.
- Gusa Badilisha .
- Badilisha mipangilio ya orodha kisha uguse Hifadhi.
Kufuta orodha
- Fungua programu ya Studio ya YouTube .
- Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
- Katika kichupo cha Orodha, chagua orodha ambayo ungependa kufuta.
- Gusa Badilisha .
- Gusa FUTA ORODHA, kisha uchague Sawa.