Hafla ya ziada kwenye Premium ni mitiririko mubashara na wasanii kwa waliojisajili kwenye Premium pekee. Ni fursa za wanachama wa YouTube Premium na YouTube Music Premium kushirikiana katika muda halisi na wasanii wanaoandaa mipasho ya video na gumzo la moja kwa moja. Hafla ya ziada kwenye Premium zinapatikana katika masoko yote ambapo YouTube Premium na YouTube Music Premium zimezinduliwa.
Ujumbe wa gumzo la moja kwa moja na maoni kwenye Hafla ya ziada kwenye Premium huonekana kwa wanachama wote wa YouTube Premium na YouTube Music Premium wanaoweza kufikia mtiririko mubashara. Hii inamaanisha kuwa ujumbe huu wa gumzo la moja kwa moja na maoni kwenye mitiririko hii mubashara huenda yakaonekana kwa wanachama wote waliopo na watakaojiunga katika siku za usoni wa YouTube Premium na YouTube Music Premium wanaoweza kutazama mitiririko mubashara iliyowekwa kwenye kumbukumbu.
Bado unaweza kuona ujumbe wako mwenyewe wa gumzo la moja kwa moja na kuwa na chaguo la kuufuta kwa kutembelea historia ya gumzo la moja kwa moja, hata kama wewe si mwanachama tena wa YouTube Premium au YouTube Music Premium. Unaweza pia kuona maoni yako mwenyewe na kuyafuta kwa kutembelea historia ya maoni yako, hata kama huna YouTube Premium au YouTube Music Premium.