Ukurasa wako huunganisha maelezo ya uanachama, ofa na takwimu zilizowekewa mapendeleo ili kukusaidia kunufaika zaidi na YouTube Premium.
Fahamu manufaa yote utakayopata ukitumia Premium katika ukurasa wa Manufaa Yako ya Premium
Je, ni nini kimejumuishwa katika ukurasa wangu wa manufaa ya Premium?
- Orodha ya manufaa ya uanachama wa Premium, kama vile video bila matangazo, uchezaji wa chinichini, video ulizotazama nje ya mtandao na zaidi. Manufaa mapya huongezwa mara kwa mara, kwa hivyo angalia tena ili upate taarifa.
- Takwimu za matumizi zilizowekewa mapendeleo kama vile saa au dakika zilizotazamwa ili kuonyesha jinsi ulivyotumia uanachama wako wa Premium kadiri muda ulivyosonga.
- Matangazo na ofa mpya zinapatikana.
Pata ukurasa wako wa manufaa wa YouTube Premium
Ukurasa wako wa manufaa ya Premium unaweza tu kutazamwa kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi (isipokuwa vishikwambi).
Gundua manufaa yako kwa kutumia kompyuta au kivinjari cha kifaa cha mkononi au fuata hatua hizi kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi:
- Gusa picha yako ya wasifu .
- Gusa Manufaa yako ya Premium.