Vidirisha vya taarifa za uchaguzi

Vipengele vinavyohusiana na uchaguzi vinapatikana tu katika vipindi vya uchaguzi kwenye nchi au maeneo machache. Vipengele vinavyopatikana vinaweza kutofautiana kwenye kipindi mahususi cha uchaguzi.

Huenda vidirisha vya maelezo vikaonyeshwa unapotafuta au kutazama video zinazohusiana na wagombea wa uchaguzi, vyama au upigaji wa kura. Vidirisha vya maelezo pia vitaangazia matokeo ya uchaguzi mahususi yaliyotolewa kwenye vyanzo vingine visivyoegemea chama chochote.

Vidirisha vya maelezo ya wagombeaji

Katika kipindi cha uchaguzi, vidirisha vya maelezo ya wagombeaji vinaweza kuonekana katika sehemu ya juu ya matokeo yako ya utafutaji unapotafuta majina ya wagombeaji wanaotimiza masharti. Vidirisha hivi huangazia maelezo kuhusu wagombeaji, kama vile vyama vyao vya kisiasa na ofisi wanayogombea. Kwa baadhi ya uchaguzi, vidirisha vya maelezo pia vinaweza kuonyesha unapotafuta vyama vya kisiasa vinavyotimiza masharti.

Maelezo kuhusu wagombeaji na vyama hutolewa kwa vyanzo vilivyothibitishwa vya wengine visivyoegemea chama chochote. Pia, kuna kiungo cha kupata maelezo zaidi kuhusu mgombeaji au chama cha kisiasa kupitia huduma ya Tafuta na Google.

Chini ya  kidirisha cha maelezo, unaweza pia kugundua:

Vidirisha vya maelezo ya kupiga kura

Katika kipindi cha uchaguzi, vidirisha vya maelezo ya kupiga kura vinaweza kuonyeshwa katika sehemu ya juu ya matokeo yako ya utafutaji unapotafuta maelezo kuhusu jinsi ya kupiga kura Ili kukusaidia upate maelezo zaidi kuhusu taarifa mahususi ya kupiga kura, vidirisha hivi vitakuelekeza kwenye maelezo ya kupiga kura katika huduma ya Tafuta na Google ambayo yamekusanywa kutoka vyanzo vilivyothibitishwa vya wengine, visivyoegemea chama chochote au vikupeleke moja kwa moja kwenye vyanzo hivyo.

Vidirisha vya maelezo kuhusu uadilifu wa uchaguzi

Katika miezi inayoelekea uchaguzi, kidirisha cha maelezo kuhusu uadilifu wa uchaguzi kinaweza kuonekana ukitafuta maudhui yanayohusiana na uchaguzi au mchakato wa kupiga kura katika nchi uliko. Pia, vidirish hivi vinaweza kuonekana chini ya video zinazojadili uchaguzi mahususi. Vidirisha vya maelezo kuhusu uadilifu wa uchaguzi huwaunganisha watazamaji na maelezo kuhusu uadilifu wa mchakato wa uchaguzi katika uchaguzi mahususi. Vidirisha vya maelezo vitaunganisha kwenye vyanzo vingine visivyoegemea chama chochote.

Vidirisha vya maelezo kuhusu matokeo ya uchaguzi

Vidirisha vya maelezo ya matokeo ya uchaguzi vinaweza kuonekana katika sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji wako unapotafuta video zinazohusiana na uchaguzi mahususi wa kitaifa. Pia, vidirisha hivi vinaweza kuonekana chini ya video zinazojadili uchaguzi mahususi wa kitaifa. Vidirisha vya maelezo vinaweza kuelekeza kwenye vyanzo vya wengine visivyoegemea chama chochote.

Vidirisha vya maelezo kuhusu mada za uchaguzi

Vidirisha vya maelezo vinavyohusiana na mada za uchaguzi vinaweza kuonyeshwa katika sehemu ya juu ya matokeo yako ya utafutaji au chini ya video zinazohusiana. Vidirisha hivi huelekeza kwenye maelezo ya kuaminika kutoka vyanzo vya wengine visivyoegemea chama chochote, kama vile tume ya uchaguzi ya kitaifa. Pata maelezo zaidi kuhusu muktadha wa mada katika vidirisha vya maelezo.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Vidirisha vya maelezo ya wagombeaji

Maelezo ya vidirisha vya maelezo ya wagombeaji hutoka wapi?

Maelezo hayo hutolewa kwa washirika wa data kutoka kwa wahusika wengine, wasioegemea chama chochote. Washirika wa data wanaweza kutofautiana kulingana na uchaguzi na nchi au eneo.

Wagombeaji wapi hupata vidirisha vya maelezo?

Wagombeaji walio na maelezo yaliyotolewa kwa mshirika mwingine asiyeegemea upande wowote wanatimiza masharti ya kupata kidirisha cha maelezo. Kwa baadhi ya uchaguzi, vyama vya kisiasa ambavyo vina angalau mgombeaji mmoja anayetimiza masharti pia vimetimiza masharti ya kupokea kidirisha cha maelezo, kama yalivyotolewa na mshirika mwingine, asiyeegemea chama chochote.

Ninapotafuta mgombeaji, hakuna kidirisha cha maelezo. Kwa nini?

Huenda ukahitaji kubadilisha hoja yako ya utafutaji. Weka jina kamili la mgombeaji ili vidirisha vya maelezo na chaneli zilizobandikwa vionekane katika matokeo yako ya utafutaji. 

Kumbuka:

  • YouTube haiamui moja kwa moja wagombeaji au vyama vinavyoonyeshwa kwenye kidirisha. Badala yake, tunategemea vyanzo vingine vilivyothibitishwa kwa maelezo ya mgombeaji na chama.
  • Iwapo mgombea hana chaneli ya YouTube, bado atangaaziwa katika kidirisha cha maelezo. 
  • Iwapo chaneli ya mgombea au ya chama imeondolewa kwa kukiuka sera ya YouTube, huenda chaneli hiyo isionyeshwe kwenye matokeo ya utafutaji.
  • Visanduku vya maelezo ya wagombeaji vinapatikana tu kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi (Android na iOS) au kwenye kompyuta yako. 

Vidirisha vya maelezo ya kupiga kura

Maelezo kuhusu kupiga kura kwenye vidirisha vya maelezo yanatoka wapi?

Vidirisha vya maelezo ya kupiga kura kwenye YouTube huunganisha kwenye vipengele vya Google vya “Jinsi ya Kupiga Kura”. Maelezo kwenye huduma ya Tafuta na Google hutolewa kwa washirika wa data kutoka kwa wahusika wengine, wasioegemea chama chochote. Washirika hawa wa data wanaweza kutofautiana kulingana na nchi au eneo na uchaguzi.

Ninapotafuta maelezo kuhusu kupiga kura, hamna kidirisha cha maelezo. Kwa nini?

Huenda ukahitaji kubadilisha hoja yako ya utafutaji. Jaribu kutafuta "Jinsi ya kupiga kura."

Kumbuka, vidirisha vya maelezo ya kupiga kura vinapatikana tu kwenye:

  • Programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi (Android na iOS)
  • Kompyuta yako

Vidirisha vya taarifa kuhusu uadilifu wa uchaguzi 

Maelezo ya vidirisha vya maelezo kuhusu uadilifu wa uchaguzi hutoka wapi?

Maelezo hayo hutolewa kwenye vyanzo vya wahusika wengine huru. Washirika wa data wanaweza kutofautiana kulingana na uchaguzi na nchi au eneo.

Ninapotafuta au kutazama video kuhusu uchaguzi, hakuna kisanduku cha maelezo. Kwa nini?

Vidirisha vya maelezo kuhusu uadilifu wa uchaguzi vitaonekana tu kwenye utafutaji au video zinazohusiana na uchaguzi mahususi katika nchi au maeneo yanayofaa. Katika utafutaji, huenda ukahitaji kufanya hoja zako za utafutaji mahususi zaidi ili kidirisha cha maelezo kionekane.

Vidirisha vya maelezo kuhusu matokeo ya uchaguzi

Maelezo kuhusu vidirisha vya maelezo ya matokeo ya uchaguzi hutoka wapi?

Maelezo hayo hutolewa kwenye vyanzo vya wahusika wengine huru. Washirika wa data wanaweza kutofautiana kulingana na uchaguzi na nchi au eneo.

Ninapotafuta au kutazama video kwenye matokeo ya uchaguzi, hakuna kisanduku cha maelezo. Kwa nini?

Vidirisha vya maelezo ya matokeo ya uchaguzi vitaonekana tu kwenye utafutaji au video zinazohusiana na uchaguzi mahususi wa kitaifa katika nchi au maeneo yanayofaa. Katika utafutaji, huenda ukahitaji kufanya hoja zako za utafutaji ziwe mahususi zaidi ili kisanduku cha maelezo kionekane. Vidirisha havitaonekana tena baada ya uchaguzi kukamilika na matokeo kuthibitishwa.

Kumbuka, vidirisha vya maelezo ya matokeo ya uchaguzi vinapatikana tu katika baadhi ya nchi au maeneo na kwenye:

  • Programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi (Android na iOS)
  • Kompyuta yako

Vidirisha vya maelezo kuhusu mada za uchaguzi

Ni mada zipi nyingine za uchaguzi huonyesha vidirisha vya maelezo?

Vidirisha vya maelezo vinaweza kuonyeshwa katika sehemu ya juu ya matokeo yako ya utafutaji au chini ya video zinazohusiana kwenye mada za uchaguzi zinazoweza kuwa na maelezo ya kupotosha. Kumbuka kuwa, vidirisha vya maelezo vinavyoonyesha muktadha zaidi kuhusu mada za uchaguzi vinapatikana tu katika nchi au maeneo machache, kwenye mada fulani, kama vile:

  • Kupiga kura kwa njia ya barua nchini Marekani
  • Kupiga kura kielektroniki nchini Brazili
  • Kupiga kura kielektroniki nchini India
 Pata maelezo zaidi kuhusu muktadha wa mada katika vidirisha vya maelezo.

Maoni

Tunategemea vyanzo huru vya wahusika wengine ili kupata taarifa za uchaguzi. Iwapo utagundua maelezo yasiyo sahihi au ambayo hayapo yanayohusiana na vipengele vyovyote vilivyofafanuliwa hapa juu, tutumie maoni:

  1. Katika kona ya juu kulia ya kisanduku cha maelezo, chagua Menyu ''.
  2. Chagua Tuma Maoni. Dirisha litafunguka ambapo unaweza kuandika maoni yako.
  3. Andika maoni yako. Jumuisha maelezo mahususi, kama vile mgombeaji au chama kipi hakipo au kina maelezo yasiyo sahihi.
  4. Chagua iwapo ungependa kujumuisha picha ya skrini. Unaweza kuangazia maelezo yoyote kwenye skrini au uondoe taarifa zozote binafsi zinazoonyeshwa. Tunapendekeza ujumuishe picha ya skrini.
  5. Chagua Tuma.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10610716414309971467
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false