Ikiwa ungependa kubadilisha au kughairi safari yako ya ndege, wasiliana na kampuni ya usafiri wa ndege au wakala wa usafiri mtandaoni moja kwa moja upate usaidizi. Google haiwezi kukusaidia moja kwa moja kubadilisha au kukatisha safari.
Hakikisha umesoma sera ya kukatisha safari ili ufahamu makataa yoyote ya kukatisha safari, ada unazoweza kutozwa na kama utarejeshewa pesa. Baadhi ya mashirika ya ndege sasa yanatoa nafasi za kubadilisha nauli.
Kwa kawaida, barua pepe za kuthibitisha ulizopokea baada ya kuweka nafasi ya safari yako ya ndege zitakuwa na namba ya uthibitisho na anwani ya mawasiliano ya shirika la ndege au ya wakala wa usafiri. Pia unaweza kupata maelezo zaidi katika maelezo ya safari husika kwenye google.com/travel.