Google kwa Mashirika Yasiyolenga Faida hutuma jarida lenye taarifa kuhusu fursa, mipango na miradi mahususi ya mashirika yasiyolenga faida. Si lazima uwe na akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyolenga Faida ili upokee majarida, mtu yeyote anaweza kujisajili. Ili ujisajili kupokea jarida, fuata hatua hizi:
- Nenda kwenye www.google.com/nonprofits/account/settings/edit
- Teua kisanduku kilicho karibu na Majarida kisha ubofye Hifadhi.
- Utapokea barua pepe kutoka Google yenye mada: "Thibitisha kuwa ungependa kupokea Majarida kutoka Google kwa Mashirika Yasiyolenga Faida." Katika barua pepe hii, bofya Ndiyo, ningependa kupokea Majarida.
Sasa umejisajili upokee jarida la Google kwa shirika lisilolenga faida.