Muhtasari wa Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ni mpango ambao husaidia mashirika yasiyo ya faida kuwasiliana na wahisani, wafadhili na wanaojitolea.

Katika hali nyingi, video ni muundo mpya na muhimu wa kutoa simulizi kuhusu biashara. Kwa kuwa YouTube hupata watazamaji bilioni moja kila mwezi, mashirika yote yasiyo ya faida yanaweza kutumia video kwenye YouTube kushiriki hadithi zao na hadhira ya kimataifa. Unaweza kupata nyenzo zote kwenye tovuti ya YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Masharti ya mpango

Ili kuhakikisha kama shirika lako lisilo la faida linatimiza mahitaji ya kushiriki katika mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, soma mwongozo wa masharti ya kujiunga kwenye mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Vipengele vya mpango

Ukiwa mshirika kwenye mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, unaweza kutumia vipengele hivi vilivyoundwa kwa ajili ya washirika:

Kuunganisha moja kwa moja kwenye tovuti yako kutoka kwenye video zako

Kadi za Kuunganisha Popote

Unaweza kuwaelekeza watazamaji wako kwenye kurasa za kutua za nje za kampeni yako ukitumia kadi za Kuunganisha Popote, aina maalum ya kadi ambazo zinakuwezesha kuunganisha kwenye URL ya nje. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka kadi za Kuunganisha Popote kwenye video zako.

Kuboresha maudhui yako 

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia YouTube ili kufahamu hadhira yako na kukuza ushawishi wako.

Usaidizi maalum wa kiufundi

Tuko tayari kuwasaidia washirika wa mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuhusu matatizo yoyote ya kufungua chaneli ya shirika lako lisilo la faida kwenye YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasiliana nasi

 
Hakikisha unakagua aina mbalimbali za vipengele vya chaneli ya watayarishi wa YouTube vinavyopatikana kwa ajili ya watayarishi wote wa mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
14053881458233184056
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
false
false
false
false