Anza kubuni kwenye Wingu la Google ukitumia salio zisizolipishwa kisha uchague huduma zisizolipishwa (hadi vikomo mahususi vya kila mwezi) ili uboreshe dhamira ya shirika lako lisilolenga faida kwa kutumia mbinu za kisasa.
Kiwango Kisicholipishwa cha Wingu la Google hukupa idhini chache za kufikia bidhaa na huduma nyingi za kawaida za Wingu la Google bila kulipia.
Watumiaji wote wa Wingu la Google wanaweza kutumia bidhaa mahususi za Wingu la Google—kama vile Compute Engine, Hifadhi ya Wingu na BigQuery—bila kulipia, kwa vikomo mahususi vya matumizi ya kila mwezi. Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya ziada ya kiwango kisicholipishwa.
Mfano wa Manufaa ya Wingu kwa Mashirika Yasiyolenga Faida
- Kunukuu matamshi: Kunukuu Matamshi hurahisisha ujumuishaji wa teknolojia za Google za utambuzi wa matamshi kwenye programu za wasanidi.
- Hifadhi ya wingu: Hifadhi ya Wingu huruhusu nafasi kubwa ya hifadhi na urejeshaji wa kiasi chochote cha data wakati wowote.
- Big Query: BigQuery ni mfumo wa data ya takwimu unaodhibitiwa kikamilifu na Wingu la Google wenye ukubwa wa petabaiti na wa gharama nafuu unaokuruhusu uchakate takwimu za viwango vikubwa vya data kwa ukadiriaji wa muda halisi.
Baada ya Jaribio Lisilolipishwa
Jaribio Lisilolipishwa likiisha, nyenzo zote ulizobuni wakati wa jaribio husimamishwa kiotomatiki, akaunti yako ya bili ya Jaribio Lisilolipishwa itasimamishwa na hutatozwa.
- Ukiamua kufungua akaunti kamili inayolipishwa ya Bili ya Wingu ndani ya siku 30 baada ya jaribio kuisha: Nyenzo zako hutiwa alama ili zifutwe, lakini unaweza kuzirejesha. Pata maelezo zaidi kuhusu ufutaji wa data kwenye Wingu la Google.
- Ukifungua akaunti kamili inayolipishwa zaidi ya siku 30 baada ya jaribio kuisha: Nyenzo zako za Jaribio Lisilolipishwa zitapotea.
Kuzidisha vikomo vya Kiwango Kisicholipishwa
- Matumizi yoyote yanayozidi vikomo vya matumizi vya Kiwango Kisicholipishwa yatatozwa kiotomatiki kwa viwango vya kawaida.
- Unaweza kusaidia kufuatilia na kudhibiti gharama kwa kuweka mipangilio ya bajeti na arifa kupitia dashibodi ya Wingu la Google.
Soma mwongozo usiolipishwa wa mpango wa Wingu ukihitaji usaidizi wa moja kwa moja, usaidizi wa jumuiya pamoja, hati pamoja na ukiwa na maswali.