Maktaba ya Vidokezo vya Gemini kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Kutumia vidokezo kutoka kwenye maktaba ya vidokezo

Kidokezo ni swali unalouliza au maagizo unayoipatia Gemini, kiratibu chako kinachotumia AI kutoka Google, ili kutayarisha matokeo unayohitaji. Maktaba hii ya vidokezo ni mkusanyiko wa mifano ya vidokezo vinavyohusiana na taratibu za kawaida za kazi katika mashirika yasiyolenga faida. Kumbuka kuzingatia mbinu za kutumia AI kwa kuwajibika unapotumia zana za AI.

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu bora za msingi unapoandika vidokezo ili kupata usaidizi kutoka Gemini

Kutumia lugha ya kawaida

Piga gumzo na Gemini kama unavyofanya na rafiki au mwenzako. 

  • Badala ya kuandika..."Mapendekezo ya data ya ubora kwa mashirika yasiyolenga faida" 
  • Jaribu kuandika hivi...“Pendekeza njia za kukusanya data ya ubora kama vile ushahidi wa waajiri ili kuonyesha matokeo yetu. Shirika letu lisilolenga faida hutoa huduma za kuwatafutia watu kazi na mafunzo ya ufundi kwa wakazi wa eneo husika wanaokumbana na changamoto za kupata ajira.”

Kutumia maelezo mafupi na yanayoeleweka

Tumia maagizo mafupi na uepuke kutumia lugha inayokanganya.

  • Badala ya kuandika ..."Mchakato wa kuwasiliana na wafadhili kupitia barua pepe." 
  • Jaribu kuandika hivi...“Andika kiolezo cha barua pepe fupi salama ya kuwashirikisha upya wafadhili ambao hawajatoa michango kwa shirika lisilolenga faida katika mwaka uliopita“

Kubainisha muktadha

Weka muktadha ili ombi lako lieleweke vyema na utayarishe jibu linalofaa zaidi.  Ipatie Gemini historia kuhusu malengo, hadhira na vikwazo vyovyote husika vinavyolikabili shirika lako.

  • Badala ya kuandika..."Andika chapisho kwenye blogu" 
  • Jaribu kuandika hivi..."Nisaidie kuunda chapisho kwenye blogu. Hadhira ni vijana na lengo kuu ni kuhimiza michango kwa kutangaza warsha mpya ya mazoezi ya usimbaji ili kuwapa ujuzi zaidi wanaoanza. Tumia toni ya upole na ya dharura na ujumuishe mwito wa kuchukua hatua."

Kutumia maneno muhimu mahususi na yanayofaa

Gemini inaweza kuelewa maana ya neno moja na sentensi. Kutumia maneno muhimu mahususi na yanayohusiana katika kidokezo chako kutasaidia AI itayarishe jibu sahihi na lenye maelezo zaidi.

  • Badala ya kuandika..."Tayarisha maswali ya usaili kwa wanaojitolea katika shirika lisilo la faida."
  • Jaribu kuandika hivi..."Tayarisha maswali matano ya usaili yanayoshirikisha ya kutumia katika sehemu ya kuwatambulisha wanaojitolea kwenye tovuti yetu ya shirika lisilo la faida linaloshughulikia haki za kijamii."

Kuainisha majukumu changamano katika vidokezo tofauti

Iwapo ungependa Gemini itekeleze majukumu kadhaa yanayohusiana, yaainishe katika vidokezo tofauti. Kuainisha kutasaidia Gemini ielewe jukumu na itoe majibu yanayofaa.

  • Badala ya kuandika...“Tayarisha hoja kuhusu tukio la kuchangisha pesa za kusaidia shirika lisilolenga faida na jinsi ya kulitangaza.“
  • Jaribu kuandika hivi...“Ninapanga kuhusu tukio la kuchangisha pesa litakalojumuisha watu 200 ili kusaidia shirika langu lisilolenga faida linaloshughulikia kuwezesha na kudumisha upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa. Pendekeza hoja za tukio hilo.”
    • "Andika kiolezo cha barua pepe inayohusiana na hoja ya kwanza ya kutuma kwa watakaohudhuria mkutano ili kuhimiza michango."
    • "Sasa tayarisha ratiba ya wiki 4 ya kutangaza hoja hii kwa kuhusisha mseto wa mbinu za kufanya mawasiliano za mtandaoni na za nje ya mtandao.”

Kufanya mazungumzo

Usitegemee kidokezo kimoja pekee. Iwapo jibu la Gemini linafaa, endelea kuongeza vidokezo zaidi ili ulichuje lilingane na malengo na madhumuni ya shirika lako lisilo la faida. Boresha na ujaribu ukitumia maneno tofauti ili upate matokeo bora zaidi

  • "Jibu hili linaonekana kuwa na hisia sana, unaweza kulirekebisha ili lifae chapisho kwenye blogu?"

Kujumuisha data kwenye mazungumzo

Iwapo una data mahususi iliyopo, ijumuishe kwenye vidokezo vyako 

  • "Rekebisha machapisho ya mitandao ya kijamii yanayotangaza mpango wetu wa ushauri ili ubainishe kuwa asilimia 90 ya washiriki wamehitimu shule ya upili"
Hakikisha ukweli: Kila wakati thibitisha taarifa – hasa takwimu au lugha ya kisheria inayopendekezwa – kabla ya kutumia matokeo ya Gemini kwa kufanya utafiti wako nje ya Gemini.

 


Mifano ya vidokezo

Mifano ifuatayo ya vidokezo imepangwa katika aina zinazohusiana na shughuli pamoja na majukumu ya kawaida ya mashirika yasiyolenga faida. Unaweza kutumia mifano hii ya vidokezo ili ikuongoze unapoandika vidokezo kwenye Gemini

Katika mifano mingi, unaweza kurekebisha vidokezo kwa kuweka maelezo yanayohusiana na shirika lako lisilolenga faida ili kuipatia Gemini muktadha. Kwa mfano, katika kidokezo cha kwanza cha kuandika pendekezo la ruzuku, unaweza kubadilisha malengo ya shirika lisilo la faida kwa kuweka malengo ya shirika lako lisilo la faida. Unaweza pia kuandika vidokezo vya nyongeza kwenye Gemini unapotaka kurekebisha au kuchuja matokeo. Utapata baadhi ya mifano ya vidokezo vya nyongeza kwenye maktaba ya vidokezo.

Kuchangisha

Kuandika Pendekezo la Kuomba Ruzuku
  • “Unganisha hoja muhimu katika maelezo haya ya ruzuku ili kulenga makusudio na vipaumbele mahususi vya mfadhili.” Sasa nakili na ubandike lugha iliyo kwenye maelezo ya ombi la ruzuku katika gumzo, jumuisha kiungo cha tovuti au pakia faili husika.
  • “Shirika letu lisilolenga faida linaomba ruzuku kutoka kwa [mfadhili]. Dondoa sehemu 3 kuu zenye umuhimu kwa mfadhili huyu kwa kutumia tu maelezo kutoka kwenye tovuti yake: [jumuisha URL]”
Kumshirikisha Mfadhili
  • “Orodhesha njia tofauti za kuwashukuru wafadhili wa mashirika yasiyolenga faida, ikiwa ni pamoja na barua zilizowekewa mapendeleo na ujumbe wa kipekee wa kuwapongeza kwenye mitandao ya kijamii”.
  • “Ainisha mikakati ya kuongeza viwango vya wafadhili kuendelea kulichangia shirika lisilolenga faida“. 
  • “Andika mada tatu zinazovutia za barua pepe ya kuomba michango ya kusaidia shirika letu lisilolenga faida lilinde viumbe wa majini.” -- “Shukrani, inafaa zaidi. Sasa andika barua pepe ya kuomba mchango kutoka kwa mtu ambaye aliwahi kuchangia shughuli hii hapo awali.”
  • “Bainisha sehemu muhimu za kampeni ya uchangishaji ya shirika lisilolenga faida linaloshughulikia kuboresha maisha ya watu walioathiriwa na ugonjwa wa akili wa watoto. Hakikisha kuwa sehemu hizi muhimu zinaongeza uhitaji na kuhamasisha uchangiaji."
  • “Tayarisha dhana za kampeni ya kila mwezi ya kuchangia ili kuongeza idadi ya michango ya mara kwa mara ya kuwasaidia watu na wasaidizi wao kukabiliana na athari za ugonjwa wa Alzeima.”
  • “Fanya kazi kama Mkurugenzi wa Uchangaji wa Pesa mwenye uzoefu. Andaa kiolezo cha barua pepe fupi ya kuwashirikisha tena wafadhili katika robo ya 4 ambao hawajatoa michango katika mwaka uliopita. Lengo ni kuangazia ukuzaji wa ujuzi wa wafanyakazi bila kuingilia kupita kiasi..”
  • “Andaa muhtasari wa kampeni ya mtandao wa kijamii ili kutangaza ruzuku ya shindano la zawadi inayolingana kwa shirika lisilolenga faida la uongozi kwa vijana. Sisitiza jinsi michango itakavyoongezeka mara mbili."

Hoja na Matukio ya Uchangishaji

  • “Eleza hoja bunifu zitakazotumia gharama kidogo za kuchangisha kwa shirika dogo lisilolenga faida linalosaidia wazee katika jamii yetu.”
  • “Shirika letu lisilolenga faida linaandaa tukio la kukimbia umbali wa kilomita 5 ili kusaidia utafiti kuhusu lymphoma. Tayarisha hoja za tangazo la mtandao wa kijamii linalolenga wakereketwa wa siha jijini Louisville, KY.”
  • “Fanya kazi kama Msimamizi wa Mradi. Pendekeza mada tatu tofauti za maonyesho ya kazi ya eneo husika yanayolenga waajiri 50 wa mahali husika."
    1. “Ninapenda mada ya 'Uchangiaji kwa Jamii'. Sasa, andika barua pepe ya mwaliko kwa viongozi wa biashara ndogo za eneo husika zinazoweza kutumia tena nishati ili wahudhurie kama waonyeshaji.”
    2.  “Sasa, tayarisha ratiba ya wiki 4 ya kutangaza ili kuajiri wanaotafuta kazi kwenye maonyesho haya mahususi, ikijumuisha mbinu za mitandao ya kijamii na barua pepe."

Kudhibiti Mpango

Kudhibiti Mpango
  • “Bainisha vipimo 3 hadi 4 vya kufuatilia mafanikio ya mpango wa shirika lisilolenga faida wa elimu kwa vijana. Kwa kila kipimo, pendekeza zana bora zaidi ya ukusanyaji data (k.m., utafiti wa kabla na baada ya tukio, kumbukumbu ya mahudhurio, kiolezo cha mahojiano) na ueleze umuhimu wa kila zana.”
  • “Fanya kazi kama Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimkakati. Orodhesha vigezo ambavyo shirika letu lisilolenga faida linaloshughulikia kutoa misaada dhidi ya majanga linapaswa kuzingatia linapotathmini uwezekano wa kushirikiana na shirika lingine au biashara. Weka matokeo katika muundo wa orodha hakikishi iliyoainishwa kulingana na hatari na manufaa. Tunahitaji kuhakikisha kuwa kuna mpangilio wa haraka wa majibu na maadili ya pamoja wakati wa hali za dharura.”
  • “Pendekeza njia zinazoonyesha utambulisho na zinazoficha utambulisho za kukusanya maoni kutoka kwa watu wanaohudumiwa na shirika letu lisilolenga faida la kuokoa wanyama.”
  • “Bainisha vidokezo vya kudhibiti muda kwa ufanisi vitakavyotumiwa na timu ya shirika letu lisilolenga faida ukijumuisha vipaumbele vingi bora.”
Kuripoti kuhusu Mpango na Matokeo
  • "Orodhesha sehemu muhimu za ripoti ya mwaka ya shirika lisilolenga faida linaloshughulikia kulinda wanyamapori katika eneo letu la [jiji/jimbo/nchi]. Weka matokeo katika muundo wa jedwali lenye safu wima za Majina ya Sehemu, Kipimo Muhimu cha Kujumuisha na Hadhira."
  • "Fanya kazi kama Mkurugenzi wa Mpango. Andaa rasimu ya muhtasari na aya mbili kuu za 'ripoti ya taarifa za kila wiki kuhusu mitindo ya kuajiri na kuweka watu katika kazi katika eneo husika. Tumia toni ya kitaalamu na ya uchanganuzi na ujumuishe pointi tatu zifuatazo za data [Bandika pointi za data]."
Kusimamia Wanaojitolea
  • “Fanya kazi kama Mratibu wa Wanaojitolea. Pendekeza baadhi ya maeneo ambapo shirika letu lisilolenga faida linaweza kutangaza kwa ufanisi nafasi za kujitolea. Onyesha mawazo kama orodha iliyoainishwa (k.m., mifumo ya mtandaoni, vituo vya jamii, vyuo vikuu). Tunatoa mipango na huduma za sanaa katika [jimbo] na tunahitaji mapendekezo yaliyojanibishwa na yenye matokeo ya hali ya juu."
  • “Fafanua kinachopaswa kujumuishwa katika mchakato wa kina wa kuajiri wanaojitolea kwenye shirika lisilolenga faida linalofanya kazi na vijana.”
  • “Orodhesha mawazo ya bei nafuu ili kuwashukuru wanaojitolea kuwahifadhi wanyama pamoja na kuwapa motisha.”
  • “Pendekeza baadhi ya mikakati ya shirika lisilolenga faida ili kupata na kunufaika kutokana na wanaojitolea walio na ujuzi maalum (usanifu wa picha na michoro, sheria, n.k.).”
  • “Fanya kazi kama Mratibu wa Wanaojitolea. Buni utafiti wa kusaidia kulinganisha ujuzi na mapendeleo ya wanaojitolea na mahitaji ya mpango wetu. Toa matokeo kama orodha ya maswali 10 ya kujieleza na ya kuchagua jibu moja. Shirika letu lisilolenga faida linaendeleza mbinu zinazofaa za kazi na maisha, kwa hivyo maswali yanapaswa kupima historia zao za kitaaluma, ujuzi wa vitendo na upatikanaji."

Utangazaji

Utangazaji
  • "Fanya kazi kama Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika Lisilolenga Faida. Tayarisha vivutio 5 vinavyopendeza. Tunaendesha kampeni ya mitandao ya kijamii inayohamasisha elimu kwa umma na tunahitaji iwe ya dharura lakini yenye kuhamasisha."
  • “Fanya kazi kama Mpiga Picha Mtaalamu wa Kibiashara. Tayarisha mchoro wa vekta wa kishale kilichoelekezwa upande wa juu. Mtindo unapaswa kuwa wa picha halisi wenye mwangaza laini na uwiano wa 16:9. Mchoro huu ni mahususi kwa jarida linalohamasisha kuhusu ufadhili wa warsha za mazoezi za kuongeza ujuzi ili kuongeza nafasi za kazi za kiwango cha chini, kwa hivyo hali inapaswa kuwa ya matumaini." —“Badilisha urekebishaji wa rangi ili ujumuishe toni zaidi za buluu kwenye picha.:
  • “Pendekeza usawa unaofaa kwenye aina za maudhui (taarifa, masimulizi ya michango, miito ya kuchukua hatua, n.k.) kwenye jarida la kila mwezi la shirika letu lisilolenga faida kwa wafadhili wanaochangia wanamuziki.”
  • “Pendekeza njia zinazovutia ukitumia picha ili kuwakilisha shirika letu lisilolenga faida linaloshughulikia mafunzo ya kusoma kwa watoto wadogo kwenye machapisho ya mitandao ya kijamii au video za kampeni.”
  • "Fanya kazi kama Mtaalamu wa Uhamasishaji Anayejitolea. Tayarisha maswali 5 ya usaili yanayoshirikisha. Maswali haya yatatumiwa katika sehemu ya kuwatambulisha wanaojitolea kwenye tovuti yetu ya shirika lisilolenga faida, kwa hivyo maswali yanapaswa kuhimiza simulizi kuhusu biashara na kutafakari."
    • AU: Ukitumia Gem, unaweza kutayarisha maagizo mahususi na yanayojirudia ili Gemini iyafuate. Unaweza kugeuza kidokezo hiki kuwa "Gem" maalum iliyopakiwa mapema na maagizo: "Lengo lako ni kutayarisha maswali ya usaili wa wanaojitolea yanayolingana na fursa ya kujitolea iliyotolewa." Angalia maagizo ya jinsi ya kubuni Gem hapa.

Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vinavyopatikana kwa mashirika yasiyolenga faida kupitia Google Workspace kwa Mashirika Yasiyolenga Faida na mapunguzo mahususi kwa mashirika yasiyolenga faida kwa matoleo ya Google Workspace Business na Enterprise. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
13857557579877916114
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
false
false
false
false