Arifa

Hivi majuzi tulitangaza mabadiliko kwenye kurasa za uchapishaji. Tafadhali soma hapa ili upate maelezo zaidi.

Kufanya makala yako yaonekane kwenye mifumo mingine ya Google News

Watumiaji wanaweza kupata mada zilizopangwa za habari kuu, makala, video na zaidi kutoka duniani kote kwa kutumia huduma ya Tafuta na Google. Google inatoa njia zifuatazo za kuwasaidia watumiaji wafikie maudhui kutoka kwa wachapishaji wa aina mbalimbali.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google huonyesha habari kwenye mifumo na bidhaa zetu.

Habari kuu

“Habari Kuu” ni sehemu inayoonekana katika huduma ya Tafuta na Google tunapotambua kuwa hoja ya utafutaji inahusiana na habari. Tunalinganisha hoja ya utafutaji na maudhui husika ya habari ambayo ni bora kuonyeshwa. "Habari Kuu" huangazia makala yanayohusiana na hoja ya utafutaji na kiungo cha makala mengine yanayohusiana kwenye kichupo cha Google News. Maudhui huchaguliwa kiotomatiki kwenye kipengele hiki.

Kichupo cha Utafutaji kwenye Google News

Wakati watumiaji wanatafuta habari, kichupo cha Utafutaji kwenye Google News huchuja matokeo ya utafutaji. Watumiaji hupata maudhui yanayohusiana na matukio katika habari. Katika muktadha mpana, kichupo cha Google News huonyesha makala zaidi kuliko hoja ya kawaida ya utafutaji.

Kufanya makala yako yaonekane katika Google News au Habari Kuu

Maudhui ya wachapishaji huzingatiwa kiotomatiki katika sehemu ya "Habari kuu" au kichupo cha Utafutaji kwenye Google News. Unahitaji tu kutunga maudhui ya ubora wa juu na utii sera za maudhui kwenye Google News.

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1443414882249670381
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
100499
false
false