Wamiliki wa shirika wanaweza kuweka, kufuta au kubadilisha majina ya mashirika. Wanaweza pia kuhamisha machapisho kati ya mashirika tofauti wanayoyamiliki. Ili ubadilishe mipangilio mingine yoyote, wasiliana na timu ya usaidizi kwa wateja wa Google kupitia fomu hii.
Kidokezo: Jina la shirika halitaonekana kwa watumiaji wa Google News.
Weka shirika jipya
Ukiwa mmiliki, unaweza kuanzisha shirika jipya na ulipe jina.
- Kwenye kompyuta yako, nenda kwenye Kituo cha Wachapishaji.
- Chini ya “Chaguo zaidi,” bofya Dhibiti chapisho na shirika lako
Dhibiti mashirika unayohusiana nayo.
- Bofya Shirika jipya.
- Weka Jina la shirika.
- Bofya Weka
.
Kufuta shirika lililopo
Ili ufute shirika, unahitaji kufuta kwanza machapisho na akaunti za wachapishaji.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta chapisho na akaunti ya mchapishaji.
Ili uondoe kabisa maudhui na taarifa zako kwenye Kituo cha Wachapishaji cha Google News na programu ya Google News, katika shirika lililopo, bofya Futa.
Kuhamishia chapisho kwenye shirika jingine
Ukiwa mmiliki wa shirika, unaweza kuhamishia chapisho kwenye shirika jingine ambalo unamiliki. Ili uhamishe chapisho kati ya mashirika, ni lazima hali ya chapisho lako la Google News iwe kwenye “Rasimu.”
- Kwenye kompyuta yako, nenda kwenye Kituo cha Wachapishaji.
- Katika sehemu ya juu kulia, ,bofya menyu ya chapisho
mipangilio ya Chapisho
.
- Chini ya “Vitendo,” bofya Hamisha chapisho.
- Kwenye dirisha ibukizi, chagua shirika ambako ungependa kuhamishia chapisho.
- Bofya Hamisha.