Arifa

Hivi majuzi tulitangaza mabadiliko kwenye kurasa za uchapishaji. Tafadhali soma hapa ili upate maelezo zaidi.

Kuhamisha data ya msomaji na maarifa

Unaweza kuhamisha data ya mchangiaji au msomaji aliyejisajili pamoja na maelezo ya kujisajili kwenye jarida au ya usajili wa msomaji moja kwa moja kutoka kwenye Kituo cha Wachapishaji.

Muhimu: Unapochagua folda ya Hifadhi ya Google ya kuhamishia faili, usifungue folda hiyo. Badala yake, ili uchague folda, bofya jina la folda kisha, ubofye Weka.

Kuhamisha maelezo ya mchangiaji au msomaji aliyejisajili

Unaweza kuhamisha faili za CSV na Majedwali ya Google yaliyo na data ya michango ya wanachama, data ya usajili na anwani za barua pepe.

Uhamishaji wako wa data ya wanachama una vichupo hivi:

  • Wanachama
  • Hati za Ununuzi
  • Usajili au Michango

Ili uhamishe maelezo ya mwanachama:

  1. Katika Kituo cha Wachapishaji, nenda kwenye chapisho lako.
  2. Bofya Reader Revenue Manager.
  3. Kwenye "Menyu," bofya Wanachama.
  4. Chagua wanachama ambao ungependa kuhamisha.
  5. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Hamisha wanachama.
  6. Chagua faili ya Hifadhi ya Google ambapo ungependa kuhifadhi faili iliyohamishwa.
    • Huenda ukahitaji kuunda folda mpya ya Hifadhi ya Google ili uhifadhi faili unazohamisha.
  7. Bofya Weka.
  8. Ili upate faili, fungua folda ya Hifadhi ya Google uliyochagua.

Kuhamisha data ya maarifa

Uhamishaji wako wa maarifa una vichupo hivi:

  • Jumla
  • Wanachama wanaosoma kila siku
  • Wanachama wapya kila siku
  • Wanachama wanaotamatisha usajili kila siku

Unaweza kuhamishia data kwenye Jedwali la Google lililo na takwimu za kila siku za mapato, wanachama, kutamatishwa kwa uanachama, wanachama wapya na waliojisajili.

Ili uhamishe data yako ya maarifa:

  1. Katika Kituo cha Wachapishaji, nenda kwenye chapisho lako.
  2. Bofya Reader Revenue Manager.
  3. Kwenye "Menyu," bofya Shughuli.
  4. Chagua muda ambao ungependa kuhamisha data husika.
  5. Katika sehemu ya juu kulia, bofya Hamisha.
  6. Chagua faili ya Hifadhi ya Google ambapo ungependa kuhifadhi faili iliyohamishwa.
    • Huenda ukahitaji kuunda folda mpya ya Hifadhi ya Google ili uhifadhi faili unazohamisha.
  7. Bofya Weka.
  8. Ili upate faili, fungua folda ya Hifadhi ya Google uliyochagua.

Kidokezo: Baada ya kuhamisha faili, huwezi kuifikia moja kwa moja kwenye Kituo cha Wachapishaji. Ili upate faili uliyohamisha, fungua folda kwenye Hifadhi ya Google.

Kuhamisha data ya jarida au usajili

Unaweza kuhamisha faili za CSV na Majedwali ya Google yaliyo na anwani za barua pepe za wasomaji waliojisajili kama wanachama au waliojisajili kwenye jarida lako. Data hii inaweza kupakiwa kwenye zana yako ya kudhibiti wanachama.

Muhimu: Data ya usajili wa wasomaji na ya waliojisajili kwenye jarida itapatikana ili kupakuliwa kwa siku 30 katika kichupo cha Wanachama kwenye Reader Revenue Manager.

Ili uhamishe maelezo ya usajili kwenye jarida au usajili wa wasomaji:

  1. Katika Kituo cha Wachapishaji, nenda kwenye chapisho lako.
  2. Bofya Reader Revenue Manager.
  3. Kwenye "Ufikiaji wa Maudhui," bofya Kujisajili kwenye jarida au Usajili wa msomaji
  4. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Hamisha wanachama.
  5. Chagua faili ya Hifadhi ya Google ambapo ungependa kuhifadhi faili iliyohamishwa.
    • Huenda ukahitaji kuunda folda mpya ya Hifadhi ya Google ili uhifadhi faili unazohamisha.
  6. Bofya Weka.
  7. Ili upate faili, fungua folda ya Hifadhi ya Google uliyochagua.

Kidokezo: Unapochagua folda ya Hifadhi ya Google ya kuhamishia faili, usifungue folda hiyo. Badala yake, ili uchague folda, bofya jina la folda kisha, ubofye Weka.

Kufikia data ya utafiti

Kuna njia 2 za kufikia data ya utafiti:

  • Studio ya Data
  • Google Analytics

Kwenye Studio ya Data

  1. Angalia kiolezo hiki.
  2. Kwenye menyu kunjuzi, chagua akaunti yako ya Takwimu.
  3. Angalia matokeo.
    • Unaweza kuchuja kulingana na aina ya Tukio ili uone data kwa kila swali n.k.

Katika Njia ya Kina ya Google Analytics

  1. Nenda kwenye Google Analytics 4.
  2. Bofya Nenda kwenye Ripoti kisha Ushirikishaji kisha Matukio.
  3. Kwenye Jina la tukio, bofya Utumaji wa utafiti.
    • Kwenye “Swali la Utafiti” na “Jibu la Utafiti,” unaweza kuangalia muhtasari wa idadi ya majibu ya kila swali na majibu.
  4. Bofya Weka ulinganishaji.
    • Chagua “Swali la Utafiti” ili upate maelezo ya ukubwa.
    • Chagua aina ya swali kama vile Nia ya Kununua kama thamani za ukubwa.
  5. Katika sehemu ya “Jibu la Utafiti”, angalia majibu ya kila swali.

Unahitaji usaidizi? Wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9372258380682801597
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
100499
false
false