Kuwasaidia Wasanidi Programu Kufaulu

Duka la Google Play ni duka la kimataifa la maudhui dijitali ya mtandaoni la Google, tunakofanya kazi ili kuwaunganisha watumiaji kwenye hali bora ya utumiaji dijitali kwa kubuni mfumo bora zaidi wa kugundua na usambazaji. Tunatoa sehemu maalum kwa watumiaji kupata, kufurahia na kushiriki programu, michezo, filamu, muziki na vitabu wanavyopenda kwenye vifaa vyao wavipendavyo: Kompyuta kibao na simu za Android, Chromebook, Android TV, Wear OS by Google na zaidi. 

Tunawawezesha wasanidi programu kufanya kazi yao bora zaidi na kuwasaidia kufaulu kwa kuwekeza katika zana na nyenzo ambazo zinasaidia katika ukuaji wa biashara zao. Uwezo wetu wa kusambaza na kufika kila mahali duniani huwasilisha michezo na programu zao kwa zaidi ya watumiaji bilioni moja wa Android—lakini chanzo kikuu cha ufanisi ni jinsi wasanidi programu wanavyotumia fursa ya soko hili kubwa. 

Zana na Huduma

Huduma na zana zetu zimebuniwa ili kuwasaidia kujaribu, kufuatilia na kupata maoni ya watumiaji na kufanya mabadiliko kwa haraka katika michezo na programu zao ili kutimiza mahitaji ya watumiaji. Tunawasaidia wasanidi programu kubuni njia za kudumu na muhimu zaidi za watumiaji kushirikiana na michezo na programu zao kupitia zana zetu za kujaribu na za kushirikisha wateja, ambazo huwawezesha wasanidi programu kufanya majaribio katika njia nyingi ili kuwashirikisha watumiaji kwa njia bora. 

Mfumo wa Google Play huwasaidia wasanidi programu kujibu kwa wepesi na kwa njia nyumbufu wanapoboresha ubora wa michezo na programu zao. Zana za kusambaza kwa hatua, jaribio la beta na arifa za mapema za onyo huwawezesha wasanidi programu kubuni hali bora za utumiaji. 

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Dashibodi ya Google Play inavyoweza kuwasaidia wasanidi programu:

Mfumo wa Biashara

Google Play hutoa miundo msingi ya kimataifa ya malipo dijitali iliyobuniwa ili kuwarahisishia watumiaji miamala kwa kutumia njia za kulipa zinazofaa zaidi kwa maeneo walipo. Google Play hutoa kadi za zawadi kwa watumiaji walio katika zaidi ya maeneo 875,000 zilizo na huduma za rejareja, uwezeshaji wa malipo ya moja kwa moja kupitia watoa huduma 177 wa simu katika masoko 66, uwezeshaji wa kutumia kadi za mikopo katika masoko 150 na huduma za dijitali kama vile PayPal na mikoba saba mipya ya dijitali inayopendelewa katika masoko 15. Tunatoa usaidizi kwa wateja katika zaidi ya masoko 150 duniani kote na usaidizi kwa wauzaji katika zaidi ya masoko 135

Mfumo huu wa kimataifa wa malipo huwanufaisha wasanidi programu kwa kiwango kikubwa kwa sababu unahakikisha malipo ya haraka na rahisi kwa michezo na programu zao bila kujali mahali watumiaji walipo. 

Mfumo wa biashara pia huwawezesha wasanidi programu kuchuma mapato kwa urahisi kutokana na michezo na programu zao kupitia programu inayolipishwa, ununuzi wa ndani ya programu au usajili wa dijitali kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play

Elimu

Pia tunashiriki njia bora zaidi za kujenga biashara fanisi za michezo au programu na kuweka masasisho ya wasanidi programu kuhusu mabadiliko kwenye zana zetu. Mafunzo kwa Wasanidi wa Google Play ni mfumo usiolipishwa wa mafunzo ya mtandaoni kwa wasanidi programu, wafanyabiashara na watangazaji wa michezo na programu za Google Play. Mafunzo hutolewa kwa mtu yeyote aliye na Akaunti ya Google na hayalipishwi. Mafunzo kwenye Chuo cha Google Play ni pamoja na: 

  • Jinsi ya kutumia vipengele vya Dashibodi ya Google Play na kusambaza mchezo au programu yako
  • Njia bora zaidi za kufaulu katika biashara ya michezo na programu
  • Mwongozo kuhusu jinsi ya kuendelea kutii sera za Google Play

Wasanidi programu wanaweza pia kutufuatilia kupitia blogu ya wasanidi programu wa Android, akaunti ya Google Play kwenye tovuti ya Medium, YouTube ya Wasanidi Programu wa Android na Twitter ili kupata habari na masasisho.  

Tunajengea siku zijazo 

Katika Google Play, tumejitolea kutoa hali salama na shirikishi ya utumiaji kwa wasanidi programu na watumiaji duniani kote ambao hupakia, kupakua na kutiririsha filamu, vitabu, programu na michezo ya kupendeza kila siku. Kubuni mfumo wa kimataifa ambao unaweza kufikiwa na kila mtu na kutoa zana muhimu kwa ajili ya wasanidi programu kumekuwa lengo letu tangu tulipozindua kifaa cha kwanza kabisa cha Android.

Kadri maudhui na vifaa vyetu vinavyozidi kubadilika, ndivyo Duka la Google Play litakavyozidi kubadilika pia na tunalenga kuwaletea wasanidi programu na watumiaji huduma bora zaidi ya djitali ya kugundua na utumiaji wa duka. Ili upate mifano ya wasanidi programu wanaopata mafanikio kwenye Google Play, tafadhali tembelea https://developer.android.com/stories/.

Ili upate maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu ya ripoti ya Jinsi Google Play Inavyofanya Kazi katika: android.com/play/how-google-play-works.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4098616340426398932
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false