Upatikanaji wa Huduma na Vipengele

Google Play hujitahidi kuwahudumia wasanidi programu kwa haki na usawa iwe wana programu kubwa au ndogo, programu za wengine au za Google. Kwa mfano, programu zote zinapaswa kufuata sheria na sera sawa na programu zote hutangazwa katika Duka la Google Play kulingana na kanuni sawa.

Google Play ina mamilioni ya wasanidi programu walio na mahitaji na malengo mbalimbali. Ili kutimiza mahitaji hayo, wakati mwingine Google Play itafanya baadhi ya vipengee na utendaji vipatikane kwa wasanidi programu kadhaa, lakini si wote.

Kwa mfano, jinsi Google Play inavyowapa wasanidi programu uwezo wa kufanyia programu zao jaribio la beta kwa kutumia kikundi kidogo cha watumiaji, katika hali fulani, tunaweka vipengele au uwezo mpya kwenye Google Play ambao unapatikana kwa kikundi kidogo cha wasanidi programu, wahudumu wa Google na wengine.  Kwa mfano, tunaweza kutekeleza programu katika toleo la beta ili kujaribu na kupata maoni kuhusu vipengele maalum vya toleo la programu au vipengele maalum vinavyolenga ukurasa wa programu katika Google Play.

Zaidi ya hayo, huenda uwezo wetu wa kushiriki baadhi ya data nje ya Google au kufanya vipengele vipatikane zaidi kwa wasanidi programu wote ukadhibitiwa na masuala ya kisheria, faragha, usalama, ili kulinda siri, taarifa za umiliki au masuala mengine ya biashara ya Google. 

Kwa mfano, katika hali chache, baadhi ya programu za Google zinaweza kufikia taarifa ambazo hazijashirikiwa na wasanidi programu wote. 

  • Baadhi ya programu zinaweza kuwa na uwezo wa moja kwa moja wa kufikia data iliyojumlishwa ya programu zenyewe (kama vile usakinishaji, uondoaji, utembeleaji wa orodha ya duka) ili kufanya uchanganuzi maalum. Tunajitolea kufanya data nyingi ya aina hii iwafikie wasanidi programu kupitia Dashibodi ya Google Play, katika miundo inayoweza kupakuliwa au kupitia API, lakini huenda isiwe katika muundo sawa au uzito sawa.
  • Baadhi ya programu zinaweza kuwa na uwezo wa moja kwa moja wa kufikia data ya programu zenyewe inayoweza kumtambulisha mtumiaji, au kutoka programu nyingine za Google, kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Google. Kwa mfano, data hii inaweza kutumika kutoa huduma za usajili kwenye vifaa vingi kwa mtumiaji mmoja, au kutoa hali mufti ya utumiaji kwenye programu nyingi za Google.  
  • Baadhi ya programu za Google zinaweza pia kuwa na uwezo wa kufikia data iliyojumlishwa kuhusu mfumo wa Google Play ambayo haiwezi kushirikiwa na wasanidi programu wote kwa kuwa data hiyo ni siri, maelezo ya biashara yanayomilikiwa na Google, kwa hivyo ni nyeti kibiashara. Kwa mfano, programu za Google zinaweza kuwa na uwezo wa kufikia jumla ya kiasi kilichotumika katika soko mahususi au jumla ya usakinishaji wa aina fulani ya programu. Tunajitahidi kuongeza idadi ya maarifa ya mfumo yanayopatikana kwa wengine katika Dashibodi ya Google Play na kupitia mipango inayosimamiwa na timu zetu za maendeleo ya biashara.
  • Mwisho, baadhi ya programu za Google zinaweza kufikia vipengele vya Google Play ambavyo ni tofauti na vinavyopatikana kwa wasanidi programu wengine kutokana na sababu kadhaa za kibiashara na masuala ya kiusalama. Kwa mfano, katika hali chache, baadhi ya vipengele vya mfumo wa utozaji wa Google Play vinapatikana tu kwa idadi ndogo ya programu za Google. Maudhui ya Filamu na TV pamoja na vitabu vinavyouzwa kwenye Google Play na katika programu ya Filamu na TV kwenye Google Play, kwa mfano, zinaweza kuagizwa mapema lakini uwezo kama huo haupatikani kwa wasanidi programu wote kutokana na changamoto za unyumbufu. Usajili wa Google Stadia unaweza kulipiwa kupitia njia ya kulipa ya familia katika programu ya Google Stadia. Hata hivyo, kwa kuwa ufafanuzi wa familia au kikundi unaweza kutofautiana kutoka programu moja hadi nyingine, uwezo huu haujawafikia wasanidi programu wengine. Mbali na hayo, Google huratibu usambazaji na masasisho ya Huduma za Google Play za AR na maktaba fulani za malipo wakati watumiaji wanasakinisha programu ambazo huenda vipengele vyake vinategemea programu hii.  Masuala ya uaminifu wa watumiaji hupunguza uwezo wetu wa kufanya utendaji huo upatikane kwa wengi. Mwisho, Google Play huruhusu baadhi ya programu za Google zifikie programu mpya za Google ambazo hazijachapishwa au kujaribu programu zake kwa kutumia wafanyikazi wa Google katika njia ambazo hazipatikani kwenye programu za wengine kwa sababu ya masuala ya kiusalama au masuala nyeti ya kibiashara.  

Katika matukio yote, Google husikiliza na kujitahidi ili kuhakikisha kuwa wasanidi programu wote wana zana na uwezo wanaohitaji kukuza biashara zao kwa ufanisi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12813841377981584286
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false