Kuorodheshwa na Kutambulika kwa Programu

Lengo letu ni kuwasaidia watumiaji watambue michezo na programu kwa urahisi, ambazo watafurahia kutoka kwenye orodha iliyo na mamilioni ya michezo na programu katika Google Play. 

Watumiaji wanaweza kupata maelezo na kusakinisha programu kwa njia nyingi tofauti kwenye Google Play, katika aina nyingi tofauti za vifaa, zikiwemo simu, kompyuta kibao na TV. Kwa mfano, watumiaji wanaweza kuvinjari ukurasa wa kwanza au kurasa za chini, kutafuta programu, kupata maelezo kwenye ukurasa wa maelezo ya programu au kusoma chaguo za wahariri. 

Tungependa watumiaji waone maudhui ambayo yanawafaa na wafurahie programu wanazopakua. Kwa kawaida tunapendelea programu zenye ubora wa juu na zinazofaa hadhira pana. Kitu bora ambacho msanidi programu anaweza kufanya ili kuongeza uwezo wa kutambulika ni kubuni programu ambazo watu watafurahia na kuwapendekezea wengine.

Tunajaribu na kuboresha mara kwa mara hali ya kutambulika kwenye Google Play, kuanzia kuweka kurasa mpya za kutambulika hadi kufanya majaribio kwa kutumia miundo mbalimbali ya kuonekana na kuboresha algoriti zetu za uorodheshaji.

Kufahamu programu

Google Play inapaswa kuelewa maudhui na utendaji wa programu ili kuwasaidia watumiaji kutambua programu inayofaa kwa wakati unaofaa. 

Wakati msanidi programu anatuma programu kwenye Google Play, msanidi programu huyo hutoa maelezo kuhusu programu na sifa zake (kwa mfano mada, aina, vipengee vya picha na ufafanuzi wa programu) na maelezo kuhusu maudhui na utendaji wa programu.  Mbali na hayo, Google hutambua sifa za ziada kutoka kwa programu (kwa mfano, kuwa programu ni mchezo “wa wachezaji wengi") na huchanganua maoni ya watumiaji (kwa mfano, kupitia ukadiriaji, maoni na kushirikishwa). Maelezo haya hutumiwa kwenye mbinu ya Google ya kuorodhesha na husaidia Google kupanga programu na kuzionyesha kwa watumiaji iwe wanatafuta kitu kipya au mada mahususi.

Kupanga na kuorodhesha programu

Watumiaji wana chaguo nyingi kuhusu jinsi ya kutambua programu kwenye Google Play. Lengo letu la kupanga programu katika Google Play ni kubaini programu ambazo zinapaswa kuonyeshwa, idadi ya programu zinazopaswa kuonyeshwa na jinsi ya kuonyesha programu hizo kwa njia rahisi ya kutumia.  Vigezo vingi huzingatiwa wakati wa kupanga programu, ikiwa ni pamoja na:

  • Ufaafu kwa watumiaji: Programu zinazomfaa zaidi mtumiaji hulingana na mahali anakovinjari au hoja anayotafuta. 
  • Ubora wa hali ya programu: Programu zilizo na utendaji thabiti wa kiufundi na hali bora ya utumiaji hupendelewa sana ikilinganishwa na programu zilizo na ubora wa chini.
  • Thamani ya uhariri: Google Play hutoa mapendekezo yaliyoratibiwa ili kusaidia watumiaji wapate maudhui yanayowafaa na kufurahisha.  
  • Matangazo: Baadhi ya wasanidi programu huchagua kutangaza kwenye Google Play kwa njia sawa na huduma nyingine za Google. Matangazo haya hubainishwa vizuri na kuonyeshwa pamoja na maudhui mengine. 
  • Hali ya utumiaji: Google Play hujitahidi kuhakikisha kuwa watumiaji wanafurahia wanapopitia aina mbalimbali za programu zinazopatikana.

Vigezo hivi vikuu vinavyoathiri uorodheshaji huchukuliwa kwa njia tofauti kulingana na mahali ambapo mtazamaji anatafuta kwenye Google Play, kifaa anachotumia na mapendeleo yake binafsi. Kwa mfano, programu zinazoonyeshwa kwenye Chati Maarufu hutegemea zaidi umaarufu, ilhali programu zinazoonyeshwa kwenye matokeo ya utafutaji hutegemea zaidi ufaafu wa hoja ya mtumiaji. Mbali na hayo, baadhi ya programu hubuniwa kwa ajili ya vifaa tofauti na zinaweza kupewa nafasi ya juu zinapotafutwa kwenye TV ikilinganishwa na kifaa cha mkononi kwa mfano, au zinaweza tu kupatikana katika vifaa fulani (kwa mfano, kwenye gari). 

Maelezo zaidi kuhusu vigezo vikuu vinavyoathiri uorodheshaji:

A. Ufaafu kwa watumiaji

Tungependa kuonyesha watu maudhui yanayowafaa.  Jambo la kwanza ni kubainisha mfumo wa Google Play ambao mtumiaji anatumia na kuhakikisha kuwa programu zinapatikana na zinafaa.  Kwa mfano, baadhi ya programu zinapatikana tu katika nchi fulani au zinatumika tu kwenye vifaa fulani (ikiwa ni pamoja na maumbo mahususi), kama vile Android TV.

Ili kuwapa watumiaji maudhui yanawayofaa, tunahitaji pia kufahamu wanachotafuta.  Tunaweza kubainisha nia ya mtumiaji kwa kutumia ishara dhahiri au zisizo dhahiri.  Kwa mfano, iwapo mtumiaji anatembelea eneo mahususi kama vile kichupo cha “Watoto” (pata maelezo zaidi kuhusu Mpango wetu wa Programu Zilizoidhinishwa na Walimu), wana nia ya kuona programu za watoto pekee, na kwa kutembelea kichupo cha “Chaguo la Mhariri’, wana nia ya kuona programu zinazopendekezwa na wahariri wa Google Play pekee.  

Wakati mtumiaji anatumia kipengele cha kutafuta, tunahitaji kufahamu nia ya hoja yake. Tunafanya hivyo kwa kufasili maneno ambayo mtumiaji anaandika na kujaribu kubainisha iwapo anatafuta programu mahususi (kwa kuandika tunachotambua kuwa jina la programu) au aina ya programu (kwa mfano, michezo ya mbio za magari). Hii inaweza kujumuisha kubaini maneno mengine, kama vile visawe, ili kuleta kundi la matokeo yanayofaa.  Pindi tu tunapotambua nia, metadata (kwa mfano mada, maelezo, aina) na ishara nyingine hutumiwa kubainisha programu zinazolingana zaidi na hoja ya mtumiaji. Wakati nia ni mahususi zaidi, (kama vile utafutaji wa mada halisi), tunajaribu kuonyesha matokeo ya mada hiyo. Hata hivyo, nia inapokuwa pana (kwa mfano, utafutaji wa “kuhariri picha”), programu nyingi zinaweza kuifaa. Google Play inaweza kuzingatia ishara nyingine ambazo tunaamini zitawasaidia watumiaji kupata programu ambazo zitawapa hali bora ya utumiaji, kama vile vigezo vingine vinavyofafanuliwa hapa chini (kwa mfano, ubora wa programu) au jinsi watumiaji hushughulikia matokeo ya hoja fulani.  Tunaweza pia kujumuisha maudhui ya Vitabu na Filamu za Google Play iwapo tunaamini kuwa watumiaji wanatafuta maudhui kama hayo kupitia kipengele cha kutafuta.

Tunahitaji kushughulikia mabilioni ya watumiaji, kutoka zaidi ya nchi 190 na rika mbalimbali. Kwa sababu hiyo, kwenye Google Play, tunazingatia pia iwapo programu inaweza kufaa hadhira pana. Iwapo ufaafu au hadhira inayolengwa na programu ni mahususi zaidi, tunaweza tu kupendelea programu hiyo iwapo tunaweza kubainisha kwa uhakika zaidi (k.m kupitia  hoja ya utafutaji au hali ya kuvinjari) kuwa mtumiaji anatafuta aina hizi za programu ambazo zinalenga au kufaa hadhira mahususi.  Tunaweza pia kuonyesha mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo kwa watumiaji. Kwa mfano, tunaweza kutumia maelezo ambayo tumekusanya (kama vile programu ambazo mtumiaji alisakinisha awali) ili kubuni mapendekezo ya programu kwenye sehemu ya “Kwa Ajili Yako”. Sera ya Faragha ya Google hutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi Google huwekea mapendeleo huduma zake na vidhibiti vya faragha ya watumiaji.

Dhibiti mipangilio yako ya kuweka mapendeleo

Ili uzime mipangilio ya kuweka mapendeleo ukitumia historia ya oda na shughuli kwenye Google:

  1. Ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Nenda kwenye Vidhibiti vya shughuli.
  3. Zima mipangilio ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu.

Ili utafute na kufuta shughuli za zamani na uondoe kwenye mapendeleo:

  1. Ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Nenda kwenye Vidhibiti vya shughuli.
  3. Nenda kwenye Dhibiti shughuli.

Kwa maelezo ya kina, soma Futa shughuli yako.

Kidokezo: Ukifuta shughuli ya zamani, inaweza kuathiri hali yako ya utumiaji katika huduma nyingine za Google kama vile huduma ya Tafuta na Google na programu ya Mratibu wa Google. Unaweza kuwasha tena wakati wowote mipangilio yako ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, kuifuta au kubadilisha mipangilio yako katika account.google.com.

Pata maelezo zaidi kuhusu Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu.

 

B. Ubora wa hali ya programu

Watumiaji wa Android hutarajia programu zenye ubora wa juu, k.m programu zinazotoa hali bora ya utumiaji kwa jumla na zinazowapa watumiaji thamani ya juu mbali na uwezo wa kawaida wa vifaa.  Tunathamini pia programu zenye ubora wa juu kwa vile tunaamini kuwa watumiaji wanapofurahia programu wanazosakinisha, kuna uwezekano mkubwa kuwa wataamini ubora wa programu kwenye Google Play, hali ambayo hunufaisha mfumo wote.

Tanatumia ishara zinazowekwa na mbinu za kialgoriti kuhakikisha kuwa programu tunazopendekezea watumiaji zina ubora wa juu.  “Ubora wa programu” si tu kigezo cha hali ya ndani ya programu yenyewe, lakini pia ni cha vipengele muhimu vya hali ya kabla ya usakinishaji, kama vile aikoni, mada, picha za skrini, video, maelezo na viungo vya programu. Ishara hizi zinapaswa kusaidia hali ya kufanya uamuzi na kutoa uwakilishi bora wa programu na sifa zake. Hali ya usaidizi kwa wateja ambayo msanidi programu hutoa pia inaweza kufaa.  Vigezo vingine vinavyoweza kusaidia kuonyesha kuwa programu ni ya ubora wa juu ni pamoja na iwapo programu: 

  • inatoa kiwango cha kawaida cha muundo wa kuonekana na mitindo ya shughuli za mtumiaji ili kupata hali ya utumiaji inayotabirika na isiyobadilika; 
  • Iwapo inaonyesha matangazo, ina hali nzuri ya matangazo ndani ya programu;
  • ina vipengele, maudhui na hali ya utendaji unaotarajiwa; na
  • inatoa utendaji, uoanifu, uthabiti na hatua zinazotarajiwa na watumiaji. 

Kubaini iwapo programu ni ya ubora wa juu- au ubora wa chini ni muhimu kwa kusaidia kuhakikisha kuwa programu zinazotoa thamani ya chini kwa watumiaji au ambazo hazitendi jinsi watumiaji wanavyotarajia hazionyeshwi kwenye mifumo ambako watumiaji wanatumia kutambua mapendekezo mapya ya programu au kuonekana juu kwenye matokeo ya utafutaji. Kwa kuwa ubora wa programu utasaidia kubaini jinsi programu hupangwa kwenye Google Play, tunajitahidi kuwapa wasanidi programu mwongozo na zana za kuwasaidia kuimarisha ubora wa programu zao. Tunawapa wasanidi programu mwongozo wa majaribio ili kuwasaidia kufikia vipengele muhimu vya ubora katika programu zao; mwongozo wa ziada ili kuhakikisha wasanidi programu wanatoa hali bora zaidi ya utumiaji na kufahamu zaidi programu za Wear OS, TV na Auto; na orodha hakikishi kwa wasanidi programu wanaotumia Huduma za Michezo ya Google Play.  Tunawawezesha wasanidi programu kutumia ushauri ili kuimarisha ubora wa programu zao kabla ya kuzindua kwa kukusanya maoni kutoka kwa wanaojaribu kupitia majaribio ya ndani, ya watu wachache na ya watu wengi. Pia, tunawapa wasanidi programu nyenzo na vidokezo vya kuimarisha ubora wa programu kupitia Mafunzo kwa Wasanidi wa Google Play. Katika Dashibodi ya Google Play, wasanidi programu wanaweza kutumia zana kama vile takwimu za programu, Android vitals kwa uchanganuzi wa utendaji wa kiufundi, ukadiriaji na uchanganuzi wa maoni. Dashibodi ya Google Play huwaruhusu wasanidi programu kulinganisha utendaji wa programu yao na vikundi vya programu nyingine ili kusaidia kuelewa vyema maeneo wanakoweza kuboresha utendaji wa programu zao. Wasanidi programu pia wana uwezo wa kufikia maoni ya watumiaji kupitia njia ya ukadiriaji na maoni ya umma, ambayo ni muhimu katika kutambua masuala ya utumiaji au ubora kutoka kwa watumiaji.

C. Thamani ya uhariri

Watumiaji pia hutegemea mtazamo wa Google Play kuhusu maudhui yanayowafaa na yanayovutia, na tunatoa mapendekezo yaliyoratibiwa kutoka kwa timu ya Google Play ili kuwasaidia kuyapata.  

Hii inajumuisha uteuzi wa maudhui ya kuangazia na kutangaza na kubuni uwekaji maalum. Jukumu hili linafanywa na timu ya wahariri na wauzaji bidhaa kwenye Google Play. Uwekaji huu unaweza kuwa endelevu (kwa mfano, makala, lebo au ufafanuzi) au wa muda mfupi (kwa mfano matukio ya msimu), na unaweza kuonyeshwa kwa kutumia miundo mbalimbali ya maonyesho.

Unapochagua maudhui, timu za wauzaji bidhaa na wahariri hulenga ubora wa hali ya programu (angalia hapo juu), pamoja na vigezo kama vile upya, muundo, umuhimu wa maudhui na uwezo wa kushawishi.  Tunatumia lebo ya “Chaguo la Wahariri’ kuangazia programu tunazochukulia kuwa bora zaidi katika mada mahususi. Tunaweza pia kutoa ufafanuzi wa ziada ulioandikwa kuhusu mambo tunayofikiri kuwa hufanya maudhui yavutie (k.m vidokezo vya “kwa nini tunapenda haya”).

Tunaweza pia kufanya kampeni za bidhaa.  Timu inaweza kuzingatia muda na ufaafu inapoanzisha kampeni na kampeni kama hizo zinaweza kujumuisha matangazo (k.m ofa za Black Friday), matukio ya mahali uliko (k.m. Halloween), au matukio ya maudhui (k.m chapisho jipya au sasisho kuu).  Kwa baadhi ya kampeni, timu inaweza pia kuzingatia uwezo wa kuchuma mapato inapochagua maudhui.

D. Matangazo

Wasanidi programu wanaweza kulipa ili programu zao zionyeshwe katika sehemu zilizobainishwa za Google Play kupitia utangazaji. Matangazo hubainishwa kupitia lebo kama vile 'matangazo' au 'yamefadhiliwa'. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanzisha kampeni ya Google Ads ya programu yako.

E. Hali ya utumiaji kwenye Google Play

Tungependa kuhakikisha kuwa watumiaji wanafurahia wanapovinjari kwenye Google Play na wanaweza kutambua programu ambazo wanapenda na zile hawajazitambua. Pia tunapenda kuwe na maelezo muhimu kuhusu programu hizo.  Kwa hivyo tunazingatia hali ya utumiaji katika harakati zote kwenye Google Play, kwa mfano, jinsi tunavyopanga programu, mahali na idadi ya matangazo ya kuonyeshwa katika matokeo na miundo tunayotumia kuonyesha programu kwa watumiaji. Kadri hali ya utumiaji inavyowafaa na kuwashirikisha watumiaji kwenye Google Play, ndivyo watumiaji watakavyorudi mara nyingi kugundua na kusakinisha programu mpya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11440842029279315312
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false