Haturuhusu programu au akaunti za wasanidi programu zinazokiuka haki za uvumbuzi za watu wengine (ikiwa ni pamoja na chapa za biashara, hakimiliki, hataza, siri za biashara na haki zingine za umiliki) Pia haturuhusu programu zinazohimiza au kushawishi ukiukaji wa haki za uvumbuzi.
Tutajibu taarifa dhahiri za madai ya ukiukaji wa hakimiliki. Kwa maelezo zaidi au kuwasilisha ombi la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali), tafadhali tembelea taratibu zetu za hakimilki.
Ili uwasilishe malalamiko kuhusu uuzaji au matangazo ya uuzaji wa bidhaa ghushi ndani ya programu, tafadhali wasilisha onyo la bidhaa ghushi.
Kama wewe ni mmiliki wa Chapa ya Biashara na unaamini kuna programu kwenye Google Play inayokiuka haki zako za chapa ya biashara, tunakuhimiza uwasiliane na msanidi programu moja kwa moja ili utatue tatizo lako. Ikiwa huwezi kutatua tatizo na msanidi programu, tafadhali tuma malalamiko kuhusu chapa ya biashara kupitia fomu hii.
Ikiwa una hati iliyoandikwa inayothibitisha kuwa una ruhusa ya kutumia mali ya uvumbuzi wa wengine katika programu au orodha yako ya duka (kama vile Majina ya chapa na nembo na vipengee vya picha), wasiliana na timu ya Google Play kabla ya kuchapisha programu yako ili kuhakikisha kuwa programu hiyo haikataliwi kwa misingi ya ukiukaji wa haki za uvumbuzi.
KUNJA ZOTE PANUA ZOTE
Matumizi Yasiyoidhinishwa ya Maudhui yenye HakimilikiHaturuhusu programu zinazokiuka hakimiliki. Kubadilisha maudhui yenye hakimiliki bado kunaweza kusababisha ukiukaji. Huenda wasanidi programu wakahitajika kutoa ushahidi wa haki zao za kutumia maudhui yaliyo na hakimiliki. Tafadhali kuwa makini unapotumia maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki ili kuonyesha utendaji wa programu yako. Kwa jumla, njia ya uhakika ni kutengeneza programu ambayo ni halisi.
|
Zinazoshawishi Ukiukaji wa HakimilikiHaturuhusu programu zinazohimiza au kushawishi ukiukaji wa hakimiliki. Kabla ya kuchapisha programu yako, tafuta njia ambazo programu yako inaweza kuwa inahimiza ukiukaji wa hakimiliki na upate ushauri wa kisheria ikibidi.
Mifano ya kawaida ya ukiukaji
|