Kuchapisha programu yako

Iwe unachapisha programu yako kwa mara ya kwanza au unasasisha, hali ya uchapishaji wa programu hukusaidia uelewe upatikanaji wake kwenye Google Play.

Unaweza kuona hali ya sasa ya uchapishaji wa programu yako chini ya jina la programu na jina la kifurushi unapochagua programu kwenye Dashibodi ya Google Play.

Kumbuka: Katika akaunti fulani za wasanidi programu, tutatumia muda zaidi kukagua programu yako kwa kina ili kutusaidia kulinda watumiaji kwa njia bora. Hali hii huenda ikasababisha kuongezeka kwa muda wa ukaguzi kwa hadi siku saba au zaidi katika hali za kipekee.

Hali ya uchapishaji

Kuna aina tatu za hali za uchapishaji:

  • Hali ya programu: Hukusaidia kuelewa upatikanaji wa programu yako kwenye Google Play na anayeweza kuipata (kama vile wachunguzaji, watumiaji wote wa Google Play na zaidi).
  • Hali ya sasisho: Hukusaidia kuelewa upatikanaji wa sasisho jipya la programu yako. Sasisho ni seti ya mabadiliko ambayo umefanya kwenye programu yako.
  • Hali ya kipengee: Hukusaidia ufahamu upatikanaji wa sehemu mahususi ya sasisho, kama vile toleo, daraja la maudhui au majaribio ya kurasa za programu katika Google Play.

Uwezekano wote wa hali za programu, masasisho na vipengee umeelezewa hapa chini.

Hali ya programu
Hali Maelezo
Rasimu Programu yako haipatikani kwenye Google Play kwa sababu bado hujaichapisha au ilikataliwa wakati wa mchakato wa ukaguzi.

Jaribio la ndani

Programu yako inapatikana kwa wachunguzaji wa jaribio la ndani kupitia URL pekee–haiwezi kutambuliwa kwenye Google Play.
Jaribio la watumiaji mahususi Programu yako inaweza kutambuliwa kwenye Google Play lakini wachunguzaji waliochaguliwa ndio tu wanaweza kuisakinisha na kuitumia.
Jaribio la watumiaji wengi

Programu yako inaweza kutambulika kwenye Google Play na mtumiaji yeyote anaweza kuwa mchunguzaji. Unaweza kuweka kikomo cha idadi ya wachunguzaji.

Kujisajili mapema Programu yako inapatikana kwa watumiaji ili wajisajili mapema kwenye Google Play. Utakapoizindua, wateja ambao wamejisajili mapema watapokea arifa ya kupakua programu.
Toleo la umma Programu yako inaweza kupakuliwa na watumiaji wa Google Play katika nchi au eneo ulilochagua.
Hakuna matoleo yanayotumika Hii inamaanisha kuwa hukusambaza masasisho kwenye vikundi vyovyote au masasisho yalikataliwa. 
Yaliyobatilishwa uchapishaji Umechagua kuacha kuchapisha programu yako kwenye Google Play. Inaweza kutambuliwa kwenye Google Play kwa watumiaji waliopo pekee. Masasisho yanapatikana kwa watumiaji waliopo pekee.
Imeondolewa na Google Google imeondoa programu yako kwa muda usiojulikana–haiwezi kutambuliwa kwenye Google Play na unahitaji kutuma sasisho linalotii sera ili irejeshwe.
Imesimamishwa na Google Google imeondoa programu yako kwa muda usiojulikana–haiwezi kutambuliwa kwenye Google Play na unahitaji kukata rufaa ili irejeshwe.
Hali ya sasisho
Aina Maelezo
Hakuna mabadiliko yanayosubiri kufanywa Programu yako haina mabadiliko yanayopaswa kutumwa.
Inakaguliwa Tunakagua sasisho lako.
Sasisho limekataliwa Mabadiliko kwenye sasisho lako hayatii Sera ya Google Play au Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Unaweza kurekebisha tatizo kisha utume tena au unaweza kukata rufaa.
Programu imekataliwa

Mabadiliko kwenye sasisho lako hayatii Sera ya Google Play au Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Unaweza kurekebisha tatizo kisha utume tena au unaweza kukata rufaa.

Kumbuka: Tofauti kati ya hali hii na ya 'Sasisho limekataliwa' ni kuwa hali ya 'Programu imekataliwa' inatumika tu kwa programu zilizo katika hali ya Rasimu ambazo unajaribu kuchapisha kwa mara ya kwanza.

Mabadiliko bado hayajatumwa ili yakaguliwe

Umefanya mabadiliko kwenye programu yako ambayo bado hayajakaguliwa.

Kumbuka: Kila wakati unapofanya mabadiliko kwenye programu yako yanayohitaji kukaguliwa, mabadiliko hayo huwekwa kwenye sehemu hii ya "Mabadiliko bado hayajatumwa ili yakaguliwe" kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji. Mabadiliko yako hayatumwi kiotomatiki ili yakaguliwe. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti mabadiliko yanapochapishwa.

Yaliyotangulia Hili ni sasisho sahihi ulilofanya awali. Hali hii hukusaidia ufahamu na kuweka rekodi ya mawasilisho uliyotuma awali, ambayo yanaweza kukusaidia iwapo unatumia uchapishaji unaodhibitiwa.
Hali ya kipengee
Hali Maelezo
Rasimu Kipengee hiki hakijawahi kutumwa ili kikaguliwe.
Inakaguliwa Kipengee hiki ni sehemu ya sasisho tunalokagua.

Sasisho limekataliwa

Programu imekataliwa (ikiwa inatoka hali ya 'Rasimu' kuwa 'Imechapishwa')

Kipengee hiki ni sehemu ya sasisho ambalo halitii sera ya Google Play au Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Unaweza kurekebisha tatizo kisha utume tena au unaweza kukata rufaa.

Kumbuka: Tofauti kati ya 'Sasisho limekataliwa' na hali hii ni kuwa 'Programu imekataliwa' hutumika tu kwa programu ambazo ziko katika hali ya Rasimu, ambazo unajaribu kuchapisha.
Programu imekataliwa

Kipengee hiki ni sehemu ya sasisho ambalo halitii sera ya Google Play au Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Unaweza kurekebisha tatizo kisha utume tena au unaweza kukata rufaa.

Kumbuka: Tofauti kati ya hali hii na hali ya 'Sasisho limekataliwa' ni kuwa hali ya 'Programu imekataliwa' inatumika tu kwa programu zilizo katika hali ya Rasimu, ambazo unajaribu kuchapisha.

Linapatikana Toleo jipya kabisa la kipengee hiki linapatikana katika programu yako na kwenye Google Play.
Yaliyotangulia Hiki ni kipengee sahihi ulichowasilisha awali lakini nafasi yake ikachukuliwa na toleo jipya zaidi au kilipitwa na wakati kutokana na wasilisho lililofuata.

Chapisha rasimu ya programu

Wakati uko tayari kuchapisha rasimu ya programu, utahitaji kusambaza toleo. Mwishoni mwa mchakato huu wa kuchapisha toleo, hatua ya kubofya Toleo itachapisha pia programu yako.

Una matatizo ya kuchapisha rasimu ya programu?

Ukiona mada "Muhtasari wa hitilafu" kwenye sehemu ya juu ya ukurasa wa muhtasari wa ukaguzi wa toleo la programu yako, bofya Onyesha zaidi ili uone maelezo. Unaweza pia kuangalia ubora unaopendekezwa au unaohitajika, ikiwa upo. Huwezi kuchapisha programu yako hadi usuluhishe hitilafu. Iwapo una maonyo, matatizo madogo au yote mawili, basi unaweza kuchapisha programu yako, lakini tunapendekeza uyashughulikie kabla ya kuchapisha.

Chapisha sasisho la programu

Unaweza kutumia uchapishaji wa kawaida au unaodhibitiwa ili kuchapisha sasisho la programu iliyopo.

  • Uchapishaji wa kawaida: Masasisho ya programu zilizopo huchakatwa na kuchapishwa haraka iwezekanavyo. Kwa chaguo msingi, programu yako itatumia uchapishaji wa kawaida. Huenda programu fulani zikakaguliwa kwa muda mrefu, hatua ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa muda wa ukaguzi kwa hadi siku saba au zaidi katika hali za kipekee. Nenda kwenye sehemu ya Sasisha au batilisha uchapishaji wa programu yako ili upate maelezo zaidi kuhusu uchapishaji wa Kawaida.
  • Uchapishaji unaodhibitiwa: Masasisho ya programu zilizopo huchakatwa kwa njia ya kawaida. Baada ya kuidhinishwa, unadhibiti wakati mabadiliko yatakapochapishwa. Nenda kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu uchapishaji uliodhibitiwa na kudhibiti mabadiliko yanapokaguliwa na kuchapishwa.

Muhimu: Ili uchapishe masasisho, shirikiana na mmiliki wa akaunti yako ili kuamua ruhusa unazohitaji kati ya zifuatazo:

Maudhui yanayohusiana

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9743597829620363247
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false