Kudhibiti wakati ambao mabadiliko ya programu yanakaguliwa kuchapishwa

Mnamo Februari 2023, tulifanya mabadiliko kwenye utaratibu wako wa uchapishaji ili kufanya iwe rahisi kuelewa ni mabadiliko gani unayatuma ili yafanyiwe ukaguzi. Pia, unaweza kudhibiti vyema zaidi wakati wa kutuma mabadiliko fulani kwa ajili ukaguzi. Tembelea Blogu ya Wasanidi Programu wa Android ili upate maelezo zaidi.

Unaweza kutumia ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji ili udhibiti wakati ambao mabadiliko ya programu yako yanatumwa ili yakaguliwe na kuchapishwa.

Unaweza kuona mabadiliko yaliyofanywa kwenye programu yako na kutuma mabadiliko mahususi kwenda Google ili yakaguliwe ukiwa tayari. Unaweza pia kuzima na kuwasha mipangilio ya uchapishaji unaodhibitiwa. Mipangilio ya uchapishaji unaodhibitiwa ikiwashwa, unaweza kuona mabadiliko unayotuma ambayo yanakaguliwa na mabadiliko yaliyo tayari kuchapishwa kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji.

Angalia muhtasari wa mabadiliko uliyofanya

Ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji hutoa muhtasari wa mabadiliko yaliyofanywa kwenye programu yako na hukusaidia udhibiti wakati ambao mabadiliko mahususi yanatumwa ili yakaguliwe au kuchapishwa.

Mabadiliko yaliyoorodheshwa yanaweza kujumuisha taarifa kuhusu jinsi programu yako inavyosambazwa kwenye Google Play, kama vile kuongezwa kwa nchi au maeneo mapya kwenye toleo la umma la programu yako. Mabadiliko yanaweza pia kujumuisha maudhui uliyotoa ili kutusaidia kukagua programu yako, kama vile dodoso la ukadiriaji wa maudhui au mabadiliko kwenye hadhira ya programu yako. Kila badiliko linaorodheshwa katika jedwali, pamoja na maelezo ya mabadiliko ya kiwango cha juu na kiungo cha kuelekeza kwenye badiliko lenyewe.

Ukiwasha mipangilio ya uchapishaji unaodhibitiwa, unadhibiti wakati ambao mabadiliko yaliyoidhinishwa yatachapishwa kwenye Google Play.

Kutuma mabadiliko ili yakaguliwe

Sehemu ya "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe" hukupatia urahisi wa kufahamu wakati sahihi wa kutuma mabadiliko ili yakaguliwe. Kila wakati unapofanya mabadiliko kwenye programu yako yanayohitaji kukaguliwa, mabadiliko huwekwa kwenye sehemu hii. Kila badiliko linaorodheshwa katika jedwali, pamoja na maelezo ya mabadiliko ya kiwango cha juu na kiungo cha kuelekeza kwenye badiliko lenyewe. Vipengee havitumwi ili vikaguliwe hadi utakapobofya Tuma ili vikaguliwe. Unaweza kuweka mabadiliko yote katika vifungu na uyatume ili yakaguliwe ukiwa tayari

Mabadiliko yatachapishwa kiotomatiki mara tu baada ya kukaguliwa na kuidhinishwa na Google isipokuwa kama mipangilio ya uchapishaji unaodhibitiwa ikiwa imewashwa. Sehemu ya "Mabadiliko yanayokaguliwa" iliyopo itaendelea kuonyesha mabadiliko uliyofanya ambayo yapo katika mchakato wa kukaguliwa. Iwapo mabadiliko ya programu yako bado hayajachapishwa au yameorodheshwa katika sehemu ya "Yako tayari kuchapishwa", una chaguo la kuyahamisha yarudi kwenye sehemu ya "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe". Hatua hii hukuwezesha urejeshe nakala ya awali ya mabadiliko yoyote usiyoyahitaji yanayokaguliwa au yaliyoidhinishwa na yaliyo tayari kuchapishwa kabla ya wakati unaohitaji yachapishwe.

Kumbuka: Katika baadhi ya hali, ukiondoa mabadiliko ya programu kwenye sehemu ya "Mabadiliko yanayokaguliwa" au "Mabadiliko yaliyo tayari kuchapishwa", bado yanaweza kukaguliwa, hali inayoweza kuathiri mikakati yako ya uchapishaji

Kutumia uchapishaji unaodhibitiwa

Uchapishaji unaodhibitiwa ni muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kufuatilia mabadiliko ya programu na hali zake za kukaguliwa kwa urahisi au kuchapisha sasisho la programu moja kwa moja katika wakati mahususi. Hii inaweza kusaidia wakati wa kuratibu kampeni ya utangazaji, kuzindua tukio au toleo jipya lenye mabadiliko kwenye usambazaji au ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Uchapishaji unaodhibitiwa unaweza kuwa muhimu pia kwa programu ambazo zinategemea muda wa ukaguzi ulioongezwa, kama vile programu zilizotumwa na akaunti mpya za wasanidi programu.

Kabla ya kuanza: Madokezo muhimu kuhusu uchapishaji unaodhibitiwa

Masharti ya msingi

Majaribio

Kupanga kwa ajili ya ukaguzi na kuwasilisha masasisho

  • Mabadiliko yote ya programu yanahitaji kuchakatwa kabla hayajachapishwa. Shughuli ya kuchakata inaweza kuchukua saa chache au hadi siku saba (au zaidi katika hali za kipekee), kwa kuwa inategemea muda wa ukaguzi ambao programu yako imepangiwa.
    • Kidokezo: Tunapendekeza urekebishe ratiba yako ili ujumuishe kipindi cha uakibishaji cha angalau wiki moja kati ya muda wa kutuma programu yako na kuichapisha.
  • Kulingana na hali ya sasisho ya programu yako, huenda lisitumwe kiotomatiki kufanyiwa ukaguzi. Kwa mfano, ikiwa sasisho la programu yako limekataliwa na umefanya mabadiliko ya mara kwa mara ya kujaribu kusuluhisha tatizo hilo, mabadiliko utakayofanya hayatatumwa kiotomatiki kufanyiwa ukaguzi. Ni sharti uende kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji na ubofyeTuma ili yakaguliwe ili uwasilishe mabadiliko uliyofanya. Ili upate maelezo zaidi, angalia Hali za sasisho la programu.

Kuwasha au kuzima uchapishaji unaodhibitiwa

  • Unaweza kuwasha au kuzima uchapishaji unaodhibitiwa wakati wowote, ukiwemo wakati ambao mabadiliko yako yanakaguliwa na kuchakatwa.

Mabadiliko ambayo hayazuiwi na uchapishaji unaodhibitiwa

  • Uchapishaji unaodhibitiwa huzuia mabadiliko mengi unayofanya hadi utakapoamua kuyachapisha. Mifano ni kama ifuatavyo:
    • Usambazaji kamili na kwa hatua wa matoleo yako (isipokuwa hali zilizoorodheshwa hapa chini)
    • Kuzindua na kusasisha usajili wa mapema
    • Mabadiliko ya ukurasa wa programu katika Google Play, ikiwa ni pamoja na mabadiliko yaliyofanyika kwenye kurasa maalum za programu katika Google Play na majaribio yanayoendelea kutumika ya kurasa za programu katika Google Play
    • Mabadiliko kwenye maudhui ya programu
    • Mabadiliko kwenye aina ya programu yako
    • Mipangilio ya Google Play ya kikazi
    • Mabadiliko katika mipangilio ya wachunguzaji wa kikundi (kwa mfano, kuweka orodha mpya ya barua pepe au Kikundi kwenye Google kama orodha ya wachunguzaji)
  • Hata hivyo, kuna hali zisizofuata kanuni, ambazo ni pamoja na, lakini si tu zifuatazo:
    • Kuongeza usambazaji wa sasa kwa hatua hadi asilimia 100
    • Kusasisha sehemu ya "Maelezo kuhusu toleo" katika programu yako
    • Mabadiliko kwenye kanuni za utengaji wa vifaa
    • Mabadiliko katika uanachama wa orodha ya barua pepe au Kikundi kwenye Google kinachotumiwa na kikundi cha jaribio
    • Kubatilisha uchapishaji wa programu yako
    • Mabadiliko kwenye ukurasa wa programu yako wa Bidhaa za ndani ya programu
    • Mabadiliko ya bei
    • Kusimamisha majaribio ya kurasa za programu katika Google Play

Chapisha sasisho la programu ukitumia uchapishaji unaodhibitiwa

Hatua ya 1: Washa uchapishaji unaodhibitiwa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji.
  2. Katika sehemu ya "Hali ya uchapishaji unaodhibitiwa", nenda kwenye Washa uchapishaji unaodhibitiwa.
  3. Chagua Hifadhi.

Baada ya kuwasha kipengele cha uchapishaji unaodhibitiwa, utaona alama ya kuteua ya kijani na ujumbe unaosema “Uchapishaji unaodhibitiwa umewashwa” katika sehemu ya “Hali ya uchapishaji unaodhibitiwa” hadi utakapokizima.

Baada ya kuwasha kipengele cha uchapishaji unaodhibitiwa, fanya na utume mabadiliko ya programu yako kama kawaida. Ili uone maelezo zaidi, angalia Tayarisha na usambaze toleo. Mabadiliko hayatachapishwa hadi yatakapokaguliwa na kuidhinishwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wa “Uchapishaji unaodhibitiwa”.

Hatua ya 2: Kufuatilia na kukagua mabadiliko yako

  1. Baada ya kufanya mabadiliko kwenye programu yako, chagua Muhtasari wa uchapishaji kwenye menyu ya kushoto.
  2. Katika sehemu ya "Mabadiliko yanayokaguliwa", kagua jedwali kulingana na yafuatayo:
    • Safu wima ya "Kipengee kilichobadilishwa" huonyesha jina la kipengee na sehemu ya Dashibodi ya Google Play inayohusiana (kama vile "Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play" au "Maudhui ya programu").
    • Safu wima ya "Maelezo" hutoa maelezo mafupi ya mabadiliko.
    • Katika upande wa kulia wa jedwali, unaweza kuchagua aikoni ya kishale cha kulia ili uende kwenye sehemu husika katika Dashibodi ya Google Play.

Mabadiliko yako yanapokaguliwa na kuidhinishwa, yataanza kujazwa kiotomatiki katika sehemu ya ukurasa wa “Mabadiliko yaliyo tayari kuchapishwa”.

Hatua ya 3: Kuchapisha sasisho la programu yako

Sehemu ya “Mabadiliko yanakaguliwa” inapokosa kitu na mabadiliko yako yote yameorodheshwa chini ya sehemu ya “Mabadiliko yako tayari kuchapishwa,” unaweza kuchapisha sasisho lako kwenye Google Play. Iwapo bado una mabadiliko katika sehemu ya “Mabadiliko yanakaguliwa”, utahitaji kusubiri hadi yatakapoidhinishwa.

  1. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Muhtasari wa uchapishaji.
  2. Hakikisha iwapo mabadiliko yako yote yameidhinishwa na yameorodheshwa chini ya sehemu ya "Mabadiliko yako tayari kuchapishwa."
  3. Chagua Chapisha mabadiliko. Baada ya kuthibitisha kuwa ungependa kuchapisha, sasisho lako litachapishwa kwenye Google Play baada ya dakika chache.

Muhimu: Unapochagua Kagua na uchapishe na kuthibitisha kuwa ungependa kuchapisha, mabadiliko yako yatapatikana na kuonekana kwa watumiaji wa Google Play.

Maswali yanayoulizwa sana

Je, hatua ya kutuma mabadiliko ya ziada kwenye programu yangu itasababisha kuongezeka kwa muda wa ukaguzi?

SLA (mkataba wa huduma) au muda wa ukaguzi huhesabiwa kuanzia wakati mabadiliko ya mwisho ya programu yalipowasilishwa. Hii inamaanisha kuwa iwapo utawasilisha mabadiliko wakati kuna mabadiliko yanayokaguliwa, huenda programu yako ikarudishwa nyuma katika foleni ya ukaguzi wa programu. Iwapo hili litatokea, kipengele cha Kagua na uchapishe kitazimwa hadi ukaguzi wa programu utakapokamilika.

Uchapishaji unaodhibitiwa unafanya kazi vipi katika majaribio ya ndani ya kampuni? Je, sasisho litashughulikiwa na uchapishaji unaodhibitiwa?

Vikundi vya majaribio ya ndani ya kampuni havishughulikiwi na uchapishaji unaodhibitiwa. Katika hali nyingi, iwapo utapakia App Bundle katika kikundi cha majaribio ya ndani ya kampuni, mabadiliko yatatekelezwa mara moja. Masasisho ya programu kwenye kikundi cha majaribio ya ndani ya kampuni hayategemei ukaguzi lakini huenda yakategemea ukaguzi wa nyuma baada ya kuchapishwa kwenye Duka la Google Play.

Kuna ilani mbili za kuzingatia kuhusiana na ukaguzi na vikundi vya majaribio ya ndani ya kampuni, ambazo ni kama ifuatavyo:

  • Iwapo usambazaji wa toleo la kwanza la programu yako unalenga kikundi cha majaribio ya ndani ya kampuni, ni lazima ombi likaguliwe kabla halijachapishwa. Ukaguzi unaweza kuchukua saa chache au hadi siku saba (au zaidi katika hali za kipekee), kwa kuwa unategemea muda wa ukaguzi ambao programu yako imepangiwa.
  • Iwapo ombi lako la kwanza limekataliwa, ni lazima ombi linalofuata likaguliwe kabla halijachapishwa. Katika hali hii, iwapo utapakia App Bundle kwenye toleo la jaribio la ndani, mabadiliko hayatatekelezwa hadi ukaguzi utakapokamilika na kuidhinishwa.
Kuna tofauti gani kati ya kutumia kipengele cha "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe" na uchapishaji unaodhibitiwa? Je, uchapishaji unaodhibitiwa bado utafanya kazi jinsi ulivyokusudiwa?

Sehemu ya "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe" hukuwezesha kuamua wakati wa kutuma mabadiliko yanayohitaji kuidhinishwa ili yakaguliwe. Uchapishaji unaodhibitiwa hukuwezesha uamue wakati wa kuchapisha mabadiliko yaliyoidhinishwa. Na ndiyo, uchapishaji unaodhibitiwa bado utafanya kazi jinsi ulivyokusudiwa.

Je, tunaweza kupata orodha kamili ya mabadiliko yanayojumuishwa na yasiyojumuishwa katika kipengele cha "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe"?

Mabadiliko yanayojumuishwa katika "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili yakaguliwe" ndiyo ambayo hujumuishwa katika uchapishaji unaodhibitiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko yanayojumuishwa na yasiyojumuishwa.

Maudhui yanayohusiana

  • Pata maelezo zaidi kuhusu kuchagua wakati ambapo masasisho ya programu yako yatachapishwa kupitia Uchapishaji unaodhibitiwa kwenye Chuo cha Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1110235728838503747
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false