Kuweka mipangilio ya programu yako kwenye dashibodi ya programu

Baada ya kuunda programu yako, unaweza kuanza kuiwekea mipangilio. Dashibodi ya programu yako itakuongoza kwenye hatua zote muhimu zaidi ili kufanya programu yako ipatikane kwenye Google Play.

Kutumia dashibodi yako

Ili uanze kuweka mipangilio kwenye programu yako, chagua Dashibodi kwenye menyu ya kushoto. Chini ya maelezo ya programu kwenye sehemu ya juu ya ukurasa, utapata aina tofauti na majukumu yanayohusiana na mipangilio ya programu na toleo. Ni lazima ukamilishe majukumu ya lazima kabla ya kuzindua programu yako kwenye Google Play. 

Unapokamilisha jukumu, utaona alama ya tiki ya kijani na maandishi yaliyopigwa mstari katikati. Upau wa shughuli kwenye sehemu ya juu utasasishwa pia. Unapokamilisha majukumu zaidi, dashibodi yako itaweka data ya utendaji na maarifa muhimu yanayolingana na wakati uliowekwa. 

Baada ya kuzindua programu yako, unaweza kutembelea dashibodi yako mara kwa mara ili upate muhtasari wa vipimo muhimu, mitindo na maarifa ya programu yako. Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu vipimo hivi, nenda kwenye Angalia takwimu za programu.

Mipangilio ya awali

Maudhui ya programu

Anza kwa kutoa baadhi ya maelezo kuhusu programu yako na kuweka mipangilio kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Kutoa maelezo haya hutusaidia kuhakikisha kuwa programu yako ni salama kwa watumiaji inayolenga, inatii sera za Google Play na inatimiza mahitaji ya kisheria.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu taarifa unazohitaji kutoa ili utayarishe programu yako, angalia Tayarisha programu yako kukaguliwa.

Uainishaji wa programu na maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play

Chagua aina ya programu, toa maelezo ya mawasiliano na uweke mipangilio kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.

Sambaza programu yako

Jaribu programu yako

Jaribu programu yako kwa kutumia vikundi mahususi vya wachunguzaji, kabla ya kufungua majaribio yako kwa kundi kubwa la watumiaji wa Google Play. Watumiaji wanaweza kutoa maoni muhimu ambayo yanakusaidia kuboresha programu yako bila kuathiri ukadiriaji wa umma wa programu yako.

Muhimu: Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuweza kufikia toleo la umma ili wachapishe programu zao kwenye Google Play, au watumie vipengele vingine kama vile kujisajili mapema au jaribio la watumiaji wengi. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Majukumu ya majaribio yanajumuisha:

  • Kuweka mipangilio ya jaribio la ndani au jaribio la watumiaji mahususi.
  • Kutayarisha na kusambaza toleo kwenye kundi la majaribio.
  • Kuwaalika wanaojaribu kupitia barua pepe au Vikundi vya Google na kukusanya maoni ya faragha.
  • Kuweka mipangilio ya kikundi cha jaribio la watumiaji wengi na kuhamia kwenye jaribio la watumiaji wengi ili mtu yeyote anaweza kujiunga na majaribio yako kwenye Google Play na atoe maoni bila kuathiri ukadiriaji wako wa Google Play.
Kujisajili mapema

Kwa kutumia kipengele cha kujisajili mapema, unaweza kuchapisha ukurasa wa programu yako katika Google Play kabla ya kuizindua ili watumiaji waweze kujisajili mapema. Utakapozindua, watumiaji wowote waliojisajili mapema watapokea arifa ili wapakue programu yako au programu yako itasakinishwa kiotomatiki.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya programu au mchezo wako upatikane, angalia Anzisha uhamasishaji wa programu zako kupitia usajili wa mapema.

Chapisha programu yako (kwa toleo la umma)

Ili uzindue programu yako kwenye Google Play, unahitaji kusambaza toleo kwenye toleo lake la umma.

Baada ya kuzindua

Baada ya kuzindua programu yako, unaweza kutembelea mara kwa mara dashibodi yako ili upate muhtasari wa vipimo muhimu, mitindo na maarifa ya programu yako. Vipimo vilivyoonyeshwa hapa vinaweza kubadilika baada ya muda kadri data zaidi ya matumizi inavyopatikana. Unaweza kuweka mapendeleo kwenye dashibodi yako ili ionyeshe data ambayo ni muhimu zaidi kwako.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6983389431790929991
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false