Kuboresha ukubwa wa programu yako na kuzingatia vikomo vya ukubwa vilivyowekwa na Google Play

Ukubwa wa programu ni kigezo muhimu cha ubora wa kiufundi kinachoweza kuathiri vipimo vya matukio ya kuweka au kuondoa programu yako kwenye vifaa. Google Play pia ina vikomo vya ukubwa wa programu na maudhui yanayobadilika kiotomatiki, kama vile sehemu za vipengele na vifurushi vya vipengee. Makala haya yanaeleza kwa kina vikomo vya ukubwa vya Google Play na kueleza jinsi unavyoweza kutumia Dashibodi ya Google Play kuelewa ukubwa unaohusiana na programu yako, ili udumishe ukubwa wa programu ulioboreshwa iwezekanavyo.

Kuelewa ukubwa wa programu

Ni muhimu ufuatilie mara kwa mara na uelewe jinsi unavyoweza kupunguza ukubwa wa programu yako inayopakuliwa na kuwekwa kwenye vifaa kwa sababu vigezo hivi vinaweza kuathiri ufanisi wa matukio ya kuweka na kuondoa programu kwenye vifaa mtawalia. Hivi ndivyo namna vipimo hivi viwili vya ukubwa hutofautiana:

  • Ukubwa wa programu ya kupakuliwa: Ukubwa wa programu yako ambayo watumiaji hupakua kutoka kwenye Google Play. Wakati programu ni kubwa zaidi, itachukua muda mrefu kupakuliwa.
  • Ukubwa wa programu kwenye kifaa: Nafasi inayohitajika ili kuweka programu yako kwenye kifaa. Kwa kuwa programu huwa zinabanwa zinapopakuliwa, hali hii inaweza kufanya programu ya kuwekwa kwenye kifaa iwe kubwa kuliko programu ya kupakuliwa. Wakati programu ya kusakinishwa ni kubwa zaidi, nafasi zaidi inahitajika kwenye kifaa cha mtumiaji ili kukamilisha usakinishaji. Baada ya programu kufunguliwa, ukubwa wake kwenye diski hutegemea matumizi ya programu.

Vikomo vya juu zaidi vya ukubwa wa programu kwenye Google Play

App Bundle, sehemu za vipengele, vifurushi vya vipengee na vifurushi vya ML vinategemea vikomo vya ukubwa vilivyowekwa hapa chini. Vikomo vyote vya ukubwa vilivyowekwa na Google Play vinalingana na ukubwa uliobanwa wa programu inayopakuliwa, kama inavyokokotolewa na Dashibodi ya Google Play baada ya kupakia App Bundle yako. Unaweza kukadiria kwa karibu ukubwa kabla ya kupakia kwenye Google Play ukitumia zana ya mkondo wa amri ya bundletool, ambayo hutumia mbinu inayofanana (lakini si ile ile) ya kukokotoa.

Muhimu: Google Play inapendekeza kuwa utumie ukubwa wa programu ambao ni mdogo na ulioboreshwa iwezekanavyo ili kusaidia vipimo vyako vya programu zinazowekwa kwenye vifaa. Wasanidi programu wengi wanapaswa kutumia vikomo vya ukubwa vilivyo chini ya hivi.

Kipengee cha programu

Kikomo cha ukubwa wa programu inayopakuliwa

Sehemu ya msingi

MB 200

Sehemu mahususi za kipengele

MB 200

Vifurushi mahususi vya kipengee

GB 1.5

Jumla ya ukubwa wa sehemu zote na vifurushi vya kipengee vya muda vya uwekaji wa programu kwenye kifaa

GB 4

Jumla ya ukubwa wa vifurushi vya vipengee vinavyowasilishwa mtumiaji anapohitaji au vya ufuatiliaji haraka

GB 4*

Wasanidi programu walio katika Mpango wa Washirika wa Google Play kwa ajili ya Michezo wanaruhusiwa kuwasilisha virufushi vya ziada vya vipengee vya hadi GB 6. Hii inamaanisha kuwa jumla ya ukubwa wa vifurushi vya vipengele vilivyowasilishwa mtumiaji anapohitaji na vya ufuatiliaji wa haraka ni GB 10 badala ya GB 4.

Pamoja na vikomo vya ukubwa vilivyoorodheshwa hapo juu, kumbuka yafuatayo:

  • Programu zenye ukubwa wa zaidi ya GB 1 lazima zilenge toleo la chini zaidi la SDK la Android Lollipop (kiwango cha API cha 21) au matoleo mapya zaidi.
  • Kiasi cha juu zaidi kinachopendekezwa cha idadi ya sehemu za vipengele ni 100 kwa programu zinazolenga toleo la chini zaidi la SDK la Android Oreo (kiwango cha API cha 26) au matoleo mapya zaidi. Idadi ya juu zaidi ya sehemu za vipengele ni 50 unapolenga toleo la chini zaidi la SDK.
  • Idadi ya juu zaidi inayoruhusiwa ya vifurushi vya vipengee kwenye App Bundle mahususi ni 100.
  • Ikiwa ukubwa wa programu yako ni zaidi ya MB 200, watumiaji wanaotumia muunganisho wa data kwa simu za mkononi wataona kidirisha kisicho na kizuizi wanapopakua programu kutoka kwenye Google Play kinachowafahamisha kuhusu hali ya ukubwa wa programu zao kwenye vifaa vyao vya Android.
  • Programu ambazo bado zinachapishwa kwa kutumia APK badala ya App Bundle zinasimamiwa na vikomo vya ukubwa wa APK vilivyopitwa na wakati (yaani, ukubwa wa juu zaidi wa APK wa MB 100) bali si vikomo vya ukubwa vilivyobainishwa hapo juu.

Kuangalia ukubwa wa programu yako ya kupakuliwa na kuwekwa kwenye vifaa

Baada ya kuchapisha programu yako katika kikundi cha toleo la umma, hapa ndipo unakoweza kuona ukubwa wa programu yako inayopakuliwa na kuwekwa kwenye vifaa:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Ukubwa wa programu (UboraAndroid vitals > Ukubwa wa programu).
  2. Katika sehemu ya juu kulia kwenye skrini, unaweza kuchuja data ya ukurasa kulingana na Ukubwa wa programu ya kupakuliwa au Ukubwa wa programu kwenye kifaa.

Unaweza kupata data ifuatayo kwenye ukurasa wa Ukubwa wa programu:

  • Ukubwa wa programu ya kupakuliwa au wa programu kwenye kifaa: Ukubwa wa programu yako kwenye kifaa kinachorejelewa na viwango vya ukubwa katika mipangilio yote ya vifaa.
  • Ukubwa wa programu ya kupakuliwa au wa programu kwenye kifaa ikilinganishwa na programu zingine: Jinsi ukubwa wa programu yako unavyolinganishwa na programu zingine.
    • Ili uanzishe kikundi cha programu zilizochaguliwa na mtumiaji cha kati ya programu 8-12, bofya Badilisha kikundi cha programu zingine.
  • Ukubwa wa programu ya kupakuliwa au wa programu kwenye kifaa baada ya muda fulani: Jinsi ukubwa wa programu yako unavyobadilika na unavyolinganishwa na programu zingine baada ya muda fulani.
    • Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye chati, unaweza kuchagua kipindi unachotaka kuangalia na uchague kisanduku cha kuteua ili kuonyesha ukubwa wa programu yako katika mipangilio ya vifaa vyote.
  • Vifaa vinavyotumika vilivyo na nafasi ya hifadhi ya chini ya GB 2 ambayo haijatumika: Asilimia ya watumiaji wanaotumia programu yako waliosalia na nafasi ya hifadhi ya kifaa ya chini ya GB 2.
  • Mara ambazo programu iliondolewa kwenye vifaa vilivyo na nafasi ya hifadhi ya chini ya GB 2 ambayo haikutumika: Uwiano wa mara ambazo programu iliondolewa kwenye vifaa vinavyotumika vilivyosalia na nafasi ya hifadhi ya chini ya GB 2 ukilinganisha na mara ambazo programu iliondolewa kwenye vifaa vyote vinavyotumika.

Vidokezo:

  • Kumbuka: Vipimo vyote vya ukubwa vinakadiriwa kulingana na toleo lako jipya kabisa la umma na mipangilio ya kifaa cha XXXHDPI ARMv8 au mipangilio ya kifaa inayotumika, ambayo inakaribia zaidi mipangilio ya programu yako.
  • Vipimo vya Vifaa vinavyotumika vilivyo na nafasi ya hifadhi ya chini ya GB 2 ambayo haijatumika na Mara ambazo programu imeondolewa kwenye vifaa vilivyo na nafasi ya hifadhi ya chini ya GB 2 ambayo haijatumika hukokotolewa kulingana na wastani wa ununuzi wa programu kwa siku 30 na huonyeshwa tu vinapobainishwa kuwa vinaweza kutumika kwenye programu yako.

Angalia uchanganuzi wa ukubwa

Ikiwa utachapisha programu ukitumia Android App Bundle, unaweza kuona chati ambayo imepangwa kulingana na msimbo wa toleo la kifurushi. Pia, ina maelezo kuhusu ukubwa wa nafasi ambayo vipengele mbalimbali vya programu yako huchukua ikilinganishwa na jumla ya ukubwa wa programu yako ya kupakuliwa au kusakinishwa kwa matoleo yako matano ya awali.

Unaweza kutumia maelezo haya kugundua vipengele vya programu yako vinavyochukua nafasi nyingi na kutambua yale unayoweza kuboresha zaidi kwa ajili ya kuokoa nafasi. Maelezo kulingana na APK zilizoundwa kutokana na kifurushi cha programu yako kwa ajili ya mipangilio ya kifaa kinachorejelewa.

Uchanganuzi unaonyesha data ifuatayo:

  • Uchanganuzi wa ukubwa wa programu inayopakuliwa:
    • Msimbo/DEX: Misimbo yote ya Java au Kotlin katika programu yako iliyojumuishwa kwa ajili ya utekelezaji kwenye Android katika muundo wa DEX.
    • Nyenzo: Nyenzo zinajumuisha jedwali la nyenzo na vipengele visivyo na misimbo vya programu yako katika saraka ya res/, kama vile picha au mifuatano.
    • Vipengee: Vipengee ni faili nyingine ambazo programu yako hutumia katika saraka ya assets/, kama vile faili za sauti au video.
    • Maktaba asili: Msimbo wa asili kwenye saraka ya libs/ ya programu yako. Kwa kawaida huu ni msimbo wowote ambao si wa Java wala Kotlin.
    • Nyingine: Faili nyingine kwenye programu yako.
  • Uchanganuzi wa ukubwa wa programu kwenye kifaa pia huonyesha: 
    • Maktaba za mfumo zilizochopolewa: Maktaba za mfumo zinapobanwa katika APK, ni lazima zichopolewe katika hifadhi ya kifaa ili kutekeleza programu yako.
    • DEX iliyoboresha: Msimbo wa DEX uliobadilishwa kuwa msimbo wa mfumo na programu ya muda wa Android wa kutekeleza ya utendaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15420507052051849292
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false