Angalia na upakue vifaa vinavyoweza kutumika

Kwa kutumia Dashibodi ya Google Play, unaweza kupakua orodha ya vifaa vilivyozinduliwa kwa umma, vinavyoweza kutumika kwenye Google Play na programu zako ikiwa faili ya thamani zilizotenganishwa kwa koma (CSV). Kwa maelezo zaidi, angalia Vifaa vinavyoweza kutumika kwenye Google Play.

Vifaa vinavyotumika huwa vimetimiza masharti ya Mpango wa Upatanifu wa Android.

Kidokezo: Ukipakua na ufungue faili ya CSV katika programu ya malahajedwali, kama vile Majedwali ya Google na ionekane kuwa na vifaa vichache kuliko unavyotarajia, jaribu kuifungua ukitumia programu tofauti ya malahajedwali au programu ya kufungua faili za CSV.

Kupakua orodha ukitumia Dashibodi ya Google Play

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa.
  4. Chagua kichujio cha Vifaa vyote.
    • Ili upakue orodha ya vifaa mahususi vinavyotumika kwenye programu yako, chagua Vifaa vinavyotumika au Vifaa vilivyotengwa.
  5. Katika upande wa juu kulia wa orodha, chagua Hamisha orodha ya vifaa.

Kwenye faili ya CSV, vifaa hupangwa kialfabeti (A-Z) kulingana na jina la mtengenezaji na kuorodheshwa katika muundo ufuatao:

  • Mtengenezaji, jina la muundo, nambari ya muundo, RAM (jumla ya hifadhi), umbo, mfumo kwenye chipu, GPU, ukubwa wa skrini, uzito wa skrini, ABI, matoleo ya SDK ya Android, Toleo la OpenGL ES

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
849251276746019669
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false