Sasisha au ubatilishe uchapishaji wa programu yako

In February 2023, we made changes to your publishing workflow to make it easier to understand which changes you're sending for review. You can also better control when you send certain changes for review.

Visit the Android Developers Blog to learn more.
Ukiwa tayari kufanya mabadiliko kwenye programu yako, makala haya yanafafanua unachohitaji ili kuhakikisha kuwa watumiaji waliopo wanapokea sasisho lako.

Tayarisha masasisho yako

  • Lazima jina la kifurushi cha Android App Bundle iliyosasishwa liwe sawa na toleo la sasa.
  • Ni lazima msimbo wa toleo uwe mpya zaidi kuliko wa toleo la sasa. Nenda kwenye tovuti ya Wasanidi programu ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka matoleo ya programu yako.
  • Lazima App Bundle iliyosasishwa iambatishwe cheti kwa kutumia cheti sawa na kile cha toleo la sasa.
Thibitisha cheti cha App Bundle
Ili uhakikishe kwamba app bundle yako inatumia cheti sawa na toleo la awali, unaweza kutekeleza amri ifuatayo kwenye matoleo yote mawili na ulinganishe matokeo:

$ jarsigner -verify -verbose -certs my_application.aab

Kama matokeo yanafanana, unatumia ufunguo ule ule wa kupakia na unaweza kuendelea. Kama matokeo ni tofauti, itabidi uipe App Bundle cheti upya kwa kutumia ufunguo sahihi wa kupakia.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuambatisha cheti kwenye programu yako.

Kidokezo: Tumia Kichunguzi cha App Bundle ili udhibiti kwa urahisi App Bundle zako katika eneo moja.

Pakia App Bundle yako 

Baada vizalia vya programu ulivyosasisha kuwa tayari, unaweza kuunda toleo jipya.

Kutuma masasisho

Baada ya kutuma sasisho kwenye programu, utaona "Inakaguliwa" chini ya "Hali ya sasisho" katika Dashibodi ya programu yako. Baada ya kuchapisha sasisho, sasisho lako litaanza kusambazwa kwa watumiaji waliopo.

Sasisho lako litakapopatikana, watumiaji wataweza kulipakua kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play au kutoka kwenye ukurasa wa Programu zangu kwenye programu ya Duka la Google Play. Iwapo mtumiaji amewasha masasisho ya kiotomatiki ya programu yako, sasisho litapakuliwa na kusakinishwa kiotomatiki.

Kumbuka kuwa masasisho yanaweza kuchukua muda ili yatumwe kwa watumiaji waliopo.

Batilisha uchapishaji wa programu

Unapobatilisha programu, watumiaji waliopo bado wanaweza kutumia programu yako na kupokea masasisho ya programu, lakini watumiaji wapya hawataweza kuipata na kuipakua kwenye Google Play.

Kabla ya kubatilisha uchapishaji wa programu, ni lazima uhakikishe kuwa:

Kubatilisha uchapishaji wa programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Nenda kwenye Toleo> Mipangilio> Mipangilio ya kina.
  4. Kwenye kichupo cha Upatikanaji wa Programu, chagua Batilisha uchapishaji.

Kusasisha programu za mfumo

Watumiaji wataona programu za mfumo (zikiwemo programu zozote zilizopakiwa mapema) katika sehemu ya Programu Zangu kwenye Duka la Google Play pindi programu yenye jina sawa la kifurushi itakapopakiwa kwenye Dashibodi ya Google Play (hata kama programu hiyo haijachapishwa).

Google Play inaweza kudhibiti masasisho ya programu zilizopakiwa mapema, ilimradi masharti yafuatayo yametimizwa:

  • Programu zilizopakiwa mapema inabidi ziwe katika nafasi ya mfumo.
  • Programu zilizopakiwa mapema inabidi zisiwe za kulipia.
  • Programu zilizopakiwa mapema zinapaswa kuambatishwa cheti kwa kutumia cheti sawa na programu iliyochapishwa kwenye Google Play.
  • Jina la kifurushi cha programu iliyopakiwa mapema na la programu iliyosasishwa, yanapaswa kufanana.
  • Msimbo wa toleo la programu iliyosasishwa unapaswa kuwa mpya zaidi ya ule wa programu iliyopakiwa mapema.

Kidokezo: Tumia API ya Msanidi Programu wa Google Play kupakua APK za mfumo zinazotengenezwa kutoka kwenye App Bundle unayopakia kwenye Google Play.

Kama unataka kupakia programu ya mfumo na ukapokea ujumbe wa hitilafu wakati ukifanya hivyo, tafadhali wasiliana nasi.

Maudhui yanayohusiana

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2260297147794164976
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false