Unda na uweke mipangilio kwenye programu yako

Baada ya kufungua akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play, unaweza kuunda programu na kuziwekea mipangilio ukitumia Dashibodi ya Google Play.

Kuunda programu yako

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua Programu zote > Unda programu.
  3. Chagua lugha chaguomsingi na uweke jina la programu yako jinsi unavyotaka lionekane kwenye Google Play. Unaweza kubadilisha mipangilio haya baadaye.
  4. Bainisha iwapo programu yako ni mchezo au programu. Unaweza kubadilisha mipangilio haya baadaye.
  5. Bainisha iwapo programu yako inalipishwa au hailipishwi.
  6. Weka anwani ya barua pepe ambayo watumiaji wa Duka la Google Play wanaweza kutumia kuwasiliana nawe kuhusu programu hii.
  7. Katika sehemu ya "Taarifa":
  8. Chagua Unda programu.

Weka mipangilio ya programu yako

Baada ya kuunda programu yako, unaweza kuanza kuiwekea mipangilio. Dashibodi ya programu yako itakuongoza kwenye hatua zote muhimu zaidi ili kufanya programu yako ipatikane kwenye Google Play.

Utaanza kwa kutoa maelezo kuhusu maudhui ya programu yako na kuweka maelezo ya ukurasa wako wa programu katika Google Play. Baada ya hapo, unaweza kwenda kwenye sehemu ya toleo la programu. Hii inatoa mwongozo kuhusu udhibiti wa toleo la mapema, majaribio na matangazo ya kusisimua na kuhamasisha watumiaji kuhusu toleo la mapema. Hatua ya mwisho ni kuzindua programu yako kwenye Google Play na kuifanya ipatikane kwa mabilioni ya watumiaji.

Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Ili uanze kuweka mipangilio kwenye programu yako, chagua Dashibodi kwenye menyu ya kushoto. Kwa hatua zinazofuata, nenda kwenye Weka mipangilio ya programu yako kwenye dashibodi ya programu.

Dhibiti programu na App Bundle zako

Google Play hutumia Android App Bundle ili kubuni na kusambaza APK ambazo zimeboreshwa katika kila usanidi wa kifaa, hali inayotoa programu bora kwa watumiaji. Hii inamaanisha kuwa unahitaji tu kuunda, kuambatisha cheti na kupakia App Bundle moja ili utumie APK zilizoboreshwa katika aina mbalimbali za usanidi wa vifaa. Kisha Google Play itadhibiti na kuwasilisha APK za usambazaji wa programu kwa niaba yako.

Majina ya vifurushi vya faili za programu ni ya kipekee na hayawezi kubadilishwa, kwa hivyo tafadhali vipe vifurushi majina kwa umakini. Majina ya vifurushi hayawezi kufutwa au kutumika tena baadaye.

Toleo lako linaweza kuwa na mojawapo ya hali tatu:

  • Rasimu: APK ambazo bado hazijatumwa kwa watumiaji
  • Zinazotumika: APK ambazo zinatumwa kwa watumiaji
  • Zilizohifadhiwa kwenye kumbukumbu: APK ambazo zilitumika wakati fulani lakini kwa sasa hazitumiki
Kutafuta faili zako za APK

Ili uone APK na App Bundle zako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo> Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Ukurasa wa kichunguzi cha App Bundle una kichujio cha toleo la programu kwenye sehemu ya juu kulia katika ukurasa, ambacho unaweza kutumia pamoja na vichupo vitatu (Maelezo, Vipakuliwa na Uwasilishaji) ili ugundue matoleo na mipangilio tofauti ya APK za programu yako kwenye vifaa tofauti.
  • Kumbuka: Kichujio hiki cha toleo la programu kinafanya kazi sawa na “Maktaba ya vizalia vya programu” kwenye toleo la zamani la Dashibodi ya Google Play.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu kudhibiti vizalia vyako vya programu, nenda kwenye Kagua matoleo ya programu ukitumia kichunguzi cha App Bundle.

Kima cha ukubwa wa juu zaidi

Programu katika Google Play zina kima cha ukubwa ambacho kinawekwa kulingana na ukubwa wa juu zaidi uliobanwa wa APK zako wakati wa kuzipakua katika vifaa vyote vinavyoweza kutumika.

Baada ya kupakia App Bundle, Dashibodi ya Google Play hutumia gzip kukadiria ukubwa wa programu inayopakuliwa. Google Play hutumia zana za kina zaidi za ubanaji kumaanisha kuwa ukubwa halisi wa programu ya kupakuliwa wa mtumiaji hautazidi ukubwa uliokadiriwa unaoonekana kwenye Dashibodi ya Google Play.

Ukubwa wa juu zaidi ni:

  • MB 200: Ukubwa wa juu zaidi uliobanwa wa APK unazopakua wa kifaa kimoja uliozalishwa kwenye App Bundle. App Bundle yenyewe inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko ukubwa huu.
  • MB 100: Ukubwa wa juu zaidi uliobanwa wa APK unayopakua wa programu zilizochapishwa kwa kutumia APK (inatumika kwa programu zilizoundwa kabla ya Agosti 2021 pekee).
Kuweka mipangilio ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu ya Google Play

Android inahitaji programu zote ziwe na cheti dijitali kabla ya kusakinishwa. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android. Unapounda toleo lako la kwanza unaweza kuweka mipangilio ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu ya Google Play ili kuamua iwapo programu yako inapaswa kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu uliozalishwa kwenye Google au ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu unaochagua.

Masharti ya toleo la programu katika Dashibodi ya Google Play

Kila APK na App Bundle ina Msimbo wa toleo katika faili ya maelezo unaoongezwa, kila unaposasisha programu yako.

Ili upakie programu yako kwenye Dashibodi ya Google Play, thamani ya juu zaidi inayowezekana ya Msimbo wa toleo ni 2100000000. Kama Msimbo wa toleo wa programu yako unazidi thamani hii, Dashibodi ya Google Play itakuzuia kuwasilisha App Bundle mpya.

Unapochagua Msimbo wa toleo kwa ajili ya App Bundle yako, kumbuka kuwa utahitaji kuongeza thamani ya Msimbo wa toleo kwa kila sasisho na usizidi thamani ya juu inayoruhusiwa.

Kumbuka: Kwa maelezo zaidi kuhusu kupanga matoleo ya programu yako, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android. Kumbuka kuwa masharti ya kupakia Android MAXINT ni tofauti na ya Dashibodi ya Google Play.

Timiza masharti ya kiwango lengwa cha API

Unapopakia app bundle, inahitaji kutimiza masharti ya kiwango lengwa cha API ya Google Play. Hivi ni viwango ambavyo programu zinatakiwa kulenga kwa sasa na baadaye.

Rejelea Masharti ya kiwango lengwa cha API ya programu za Google Play ili uelewe kiwango lengwa cha API kinachohitajika ili kuwapa watumiaji wa Android na Google Play ulinzi na hali salama ya utumiaji.

Unda ukurasa wako wa programu katika Google Play na uweke mipangilio

Ukurasa wa programu katika Google Play huonyeshwa kwenye Google Play na unajumuisha maelezo ambayo yanawasaidia watumiaji kupata maelezo zaidi kuhusu programu yako. Ukurasa wa programu yako katika Google Play unashirikiwa kwenye vikundi vyote, ikiwa ni pamoja na kikundi cha kujaribu.

Maelezo ya bidhaa
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play .
  2. Jaza sehemu zilizo chini ya "Maelezo ya Programu."
Sehemu Maelezo Idadi ya juu ya herufi* Madokezo
Jina la programu Jina la programu yako kwenye Google Play. Herufi zisizozidi 30

Unaweza kuongeza jina moja liliyojanibishwa kwa kila lugha.

Maelezo mafupi Maandishi ya kwanza wanayoona watumiaji wanapoangalia ukurasa wa maelezo ya programu yako kwenye Duka la Google Play. Herufi zisizozidi 80 Watumiaji wanaweza kupanua maandishi haya ili waone maelezo kamili ya programu yako.
Maelezo kamili Maelezo ya programu yako kwenye Google Play. Herufi zisizozidi 4000  

*Masharti ya idadi ya juu ya herufi yanatumika kwa herufi za upana kamili na herufi za upana nusu — nambari zilizoorodheshwa hapo juu ni idadi za juu  zaidi bila kujali aina ya herufi unazotumia.

Kumbuka: Matumizi ya maneno muhimu yanayorudiwarudiwa au yasiyohusiana katika jina la programu, maelezo au maelezo ya matangazo yanaweza kusababisha hali isiyo nzuri ya utumiaji kwa mteja na kupelekea programu isimamishwe kwenye Google Play. Tafadhali rejelea mwongozo kamili katika Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play.

Vipengee vya kukagua

Pata maelezo zaidi kuhusu kuongeza vipengee vya kukagua(pamoja na maelezo mafupi, picha za skrini na video) vya kuonyesha programu yako.

Lugha na tafsiri

Ongeza na udhibiti tafsiri

Unapopakia programu, lugha chaguomsingi ni Kiingereza cha Marekani (en-US). Unaweza kuongeza tafsiri za maelezo ya programu yako, pamoja na picha za skrini katika lugha lengwa na vipengee vingine vya picha. Nenda kwenye Tafsiri na ujanibishe programu yako ili upate maelezo.

Picha na video zilizojanibishwa

Ili utangaze programu yako katika lugha mbalimbali kwa ufanisi zaidi, unaweza kuweka vipengee vya picha vilivyojanibishwa kwenye Ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play.

Watumiaji wataona vipengee vya picha vilivyojanibishwa kwenye Google Play ikiwa lugha walizopendelea zinalingana na lugha ulizoongeza.

Tafsiri za kiotomatiki

Usipoongeza tafsiri zako mwenyewe, watumiaji wanaweza kuona tafsiri za kiotomatiki za ukurasa wa programu yako kwenye Google Play wakitumia huduma ya Google Tafsiri au lugha chaguomsingi ya programu yako.

Kwa tafsiri za kiotomatiki, kutakuwa na dokezo linaloelezea kuwa tafsiri imefanywa kiotomatiki na pia chaguo la kuangalia lugha chaguomsingi ya programu. Kumbuka tafsiri za kiotomatiki hazitumiki katika lugha za Kiarmenia, Kiroma cha Raeto, Kitagalogi na Kizulu.

Uainishaji na lebo

Unaweza kuchagua aina na uweke lebo kwenye programu au mchezo wako katika Dashibodi ya Google Play. Lebo na aina huwasaidia watumiaji kutafuta na kugundua programu zinazowafaa zaidi katika Duka la Google Play.

Pata maelezo zaidi kuhusu kuchagua na kuongeza aina na lebo ya mchezo au programu yako.

Maelezo ya mawasiliano

Unapotoa anwani ya barua pepe, tovuti au nambari ya simu ya programu yako, anwani yako ya mawasiliano itapatikana kwa watumiaji kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Ni sharti uweke anwani ya barua pepe ya mawasiliano. Hata hivyo, ili uwape watumiaji wako hali bora ya utumiaji wa huduma za usaidizi, tunapendekeza zaidi ujumuishe tovuti ambapo watumiaji wanaweza kuwasiliana nawe.

Ili uweke maelezo yako ya usaidizi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mipangilio ya Duka la Google Play (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Mipangilio ya Duka la Google Play)
  2. Nenda chini kwenye "Maelezo ya Mawasiliano."
  3. Weka anwani yako ya barua pepe ya usaidizi (inahitajika), nambari ya simu na URL ya tovuti.

Kidokezo: Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwapa usaidizi watumiaji wa programu yako.

Hatua zinazofuata

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7893835628107401472
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false