Fahamisha watu kuhusu programu zako kwa kutumia usajili wa mapema

Kwa kutumia usajili wa mapema, unaweza kuleta msisimko na hamasa kwa programu na michezo yako katika nchi unazochagua kabla ya kuchapisha programu na michezo yako kwenye Google Play.

Baada ya kufanya programu au mchezo upatikane kwa ajili ya usajili wa mapema, watumiaji wanaweza kutembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play ili kupata maelezo zaidi na kujisajili mapema kwa programu au mchezo wako. Kisha, ukichapisha programu au mchezo wako baadaye, watumiaji wote waliosajiliwa mapema watapokea arifa za programu kutoka Google Play ili wasakinishe mchezo au programu hiyo. Pia, programu au mchezo utakapozinduliwa, utasakinishwa kiotomatiki kwenye vifaa vinavyostahiki.

Kumbuka: Watumiaji ambao tayari wamesakinisha toleo la jaribio la programu hawatapokea arifa za programu.

Hatua ya 1: Kujiandaa kwa usajili wa mapema

Kabla ya kuweka mipangilio ya kampeni ya kujisajili mapema kwenye Dashibodi ya Google Play, soma mwongozo na masharti yetu ya kujisajili mapema na mapendekezo yetu ya shughuli za maandalizi ya kujisajili wa mapema.

Masharti na mwongozo

Yafuatayo ni mambo unayopaswa kuzingatia kabla ya kuanzisha usajili wa mapema:

  • Tunapendekeza usambaze toleo kwenye kikundi cha majaribio na ujaribu programu yako kabla ya kuanzisha usajili wa mapema. Kampeni za kujisajili mapema zinaweza tu kuchukua siku 90, ambapo baada yake unahitaji kuizindua programu yako katika toleo la umma.
  • Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play na, pia, kabla ya kuweza kutumia kipengele cha kujisajili mapema. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.
  • Hutaweza kutumia kipengele cha kujisajili mapema hadi utoe maelezo fulani kuhusu maudhui ya programu yako, ambayo hutusaidia kuhakikisha kuwa programu yako ni salama kwa watumiaji lengwa, inatii sera za Google Play na inatimiza mahitaji ya kisheria. Fahamu maelezo unayohitaji kutoa ili utayarishe programu yako kukaguliwa.
  • Baada ya kuchapisha programu au mchezo kwa ajili ya usajili wa mapema katika nchi, unapaswa kuzindua katika toleo la umma kwenye nchi hiyo ndani ya siku 90.
  • Unaweza kuwasilisha hadi programu mbili au michezo miwili kwa ajili ya usajili wa mapema kwa wakati mmoja.
  • Tunapendekeza uweke mipangilio ya kampeni yako ya kujisajili mapema wakati taarifa na mipangilio ya programu yako imekaribia zaidi toleo unalonuia kuchapisha kwa umma kadri iwezekanavyo. Hii huwezesha programu yako kusakinishwa kiotomatiki na pia huhakikisha kuwa watumiaji wanaojisajili mapema wanapokea arifa ya kuzinduliwa kwa programu.
Hatua za kina za kujiandaa kwa usajili wa mapema

Unda ukurasa kamili wa programu yako katika Google Play

Kabla ya kuanzisha kampeni yako ya kujisajili mapema, hakikisha kuwa umeunda ukurasa wa kina wa programu katika Google Play ambao una vipengee vya picha na umetafsiriwa katika lugha zingine. Hatua hii inaweza kuongeza uwezekano wa watumiaji wanaojisajili mapema kusakinisha programu au mchezo wako.

Kufanya programu yako itimize masharti ya kusakinishwa kiotomatiki

Ukichagua kufanya programu yako itimize masharti ya kusakinishwa kiotomatiki, Google Play inaweza kutuma programu yako kwa vifaa vya watumiaji kiotomatiki siku ya uzinduzi (wakijijumuisha).

Ili kufanya programu yako iweze kusakinishwa kiotomatiki, fuata hatua zifuatazo:

  • Bainisha iwapo programu yako ina matangazo au haina.
  • Iwapo programu au mchezo wako una bidhaa za ndani ya programu, hakikisha toleo la sasa la Android App Bundle kwenye kikundi cha kujisajili mapema linajumuisha <uses-permission android:name="com.android.vending.BILLING" /> katika faili ya maelezo ya programu.
    • Uwezo wa mtumiaji kutumia kipengele cha kusakinisha kiotomatiki unategemea masharti fulani.

Muhimu: Utendaji na upatikanaji wa kipengele cha kusakinisha kiotomatiki unategemea masharti yafuatayo:

  • Mtumiaji anaweza tu kutumia kipengele cha kusakinisha kiotomatiki akitimiza masharti yafuatayo:
    • Awe na kifaa cha Android M au toleo jipya zaidi.
    • Awe anatumia toleo la 19.2 au toleo jipya zaidi la Duka la Google Play.
  • Akaunti za Google za watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 na akaunti za kazini zinazosimamiwa hazijatimiza masharti ya kusakinisha programu kiotomatiki.
  • Programu zinazozidi MB 200 zitapakuliwa na kusakinishwa kupitia Wi-Fi pekee, bila kujali mipangilio ya kusakinisha ya mtumiaji.
  • Vifaa vitaendelea tu kusakinisha programu kiotomatiki iwapo vina chaji ya betri ya kutosha.
  • Vifaa ambavyo havijatimiza masharti vitapokea arifa ya kawaida ya kuzindua kipengele cha kujisajili mapema na Google Play itajaribu tena kusakinisha programu kiotomatiki kifaa kitakapotimiza masharti yanayohitajika.

Kujiandaa kuelekeza watumiaji kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play

Tunapendekeza ujiandae kuelekeza watumiaji wajisajili mapema kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play kupitia huduma unazotumia za matangazo ukitumia viungo mahususi kwenye tovuti za wengine, mitandao ya kijamii, makala kwenye vyombo vya habari, majarida ya barua pepe n.k.

  • Kidokezo: Baada ya kuwasha kipengele cha kujisajili mapema, URL ya kujisajili mapema kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play itakuwa: https://play.google.com/store/apps/details?id=jina la kifurushi cha programu au mchezo wako.
  • Kwa mfano: Ikiwa jina la kifurushi cha programu yako ni your.new.app, URL ya kujisajili mapema kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play itakuwa: https://play.google.com/store/apps/details?id=your.new.app

Tumia beji rasmi ya kujisajili mapema kutoka Google Play

Tumia beji rasmi ya kujisajili mapema kutoka Google Play kutangaza kampeni yako kwenye tovuti za wengine. Hatua hii inaweza kusaidia kuendesha hatua ya kujisajili mapema kabla ya kuzindua programu.

Hatua ya 2: Kubainisha vifaa vitakavyotumika katika usajili wa mapema

Unaweza kupakia App Bundle ili ubainishe vifaa ambavyo watumiaji wanaweza kutumia kujisajili mapema ili kupata programu yako. Dashibodi ya Google Play hutumia faili ya maelezo ya programu ili kubaini vifaa vinavyotumika kwenye usajili wa mapema.

Kumbuka:

  • App Bundle zozote unazopakia kwenye kikundi chako cha usajili wa mapema zinatumika tu kubainisha vifaa vinavyotumika na hazitolewi kwa watumiaji.
  • Ikiwa programu yako ina bidhaa za ndani ya programu, hakikisha kuwa angalau mojawapo ya App Bundle unayopakia inajumuisha Maktaba ya Malipo kupitia Google Play.
Kubainisha vifaa ambavyo watumiaji wanaweza kutumia kujisajili mapema ili kupata programu yako

Ili upakie App Bundle inayobainisha vifaa vinavyostahiki kwa usajili wa mapema, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu au mchezo.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Chagua kichupo cha Vifaa vinavyotumika.
  5. Buruta na udondoshe Android App Bundle zako (.aab) kwenye kisanduku ili upakie au chagua Pakia.
  6. Chagua Hifadhi.

Hatua ya 3: Kuweka nchi ambako watumiaji wanaweza kujisajili mapema

Unaweza kuchagua nchi na maeneo ambako ungependa watumiaji wajisajili mapema ili kupata programu yako.

Kumbuka: Hizi ni nchi au maeneo ambako mtumiaji amesajiliwa kwenye Google Play, si eneo lake halisi.

Kuweka nchi au maeneo ambako watumiaji wanaweza kujisajili mapema

Ili kuhakikisha programu au mchezo wako unapatikana kwa usajili wa mapema, ni sharti uchague nchi ambako ungependa watumiaji waweze kujisajili mapema kisha ufuate hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu au mchezo.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Chagua kichupo cha Nchi au maeneo.
  5. Chagua Weka nchi au maeneo.
  6. Chagua nchi au maeneo ambako ungependa kufanya programu yako ipatikane kwa usajili wa mapema.
  7. Chagua Hifadhi.

Kumbuka: Unaweza pia kuweka nchi baada ya kuanzisha kampeni yako ya kujisajili mapema. Kipindi cha siku 90 cha nchi huanza unapofanya usajili wa mapema upatikane katika nchi hiyo kwa mara ya kwanza.

Hatua ya nne: Wape watumiaji zawadi ya kujisajili mapema (si lazima)

Kupitia zawadi za kujisajili mapema, unaweza kuwapa watumiaji bidhaa ya ndani ya programu bila malipo baada ya kujisajili mapema ili kupata mchezo au programu yako. Zawadi za kujisajili mapema ni sawa na ofa. Hata hivyo, badala ya kuandika kuponi ya ofa ili kupokea kipengee kisicholipishwa, watumiaji hupokea kipengee baada ya kuchagua kitufe cha Kujisajili mapema kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.

Mambo muhimu unayohitaji kujua kuhusu zawadi za kujisajili mapema

Yafuatayo ni mambo muhimu unayopaswa kujua kabla ya kuweka zawadi za kujisajili mapema:

  • Unaweza kujumuisha zawadi moja ya kujisajili mapema itakayopatikana siku zote za kampeni ya kujisajili mapema kwa mchezo au programu yako.
  • Baada ya kujumuisha zawadi ya kujisajili mapema, unaweza kuibadilisha au kuifuta.
  • Unaweza kuwasha au kuzima chaguo la zawadi, lakini si wakati kampeni yako ya kujisajili mapema inaendelea.
  • Unaweza tu kutoa bidhaa zinazotumika za ndani ya programu, wala si usajili au bidhaa zisizotumika za ndani ya programu, kuwa zawadi za kujisajili mapema.
  • Unatakiwa kuweka zawadi ya usajili wa mapema kabla ya kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema katika programu yako.
  • Programu yako inahitaji kuwa na bidhaa za ndani ya programu na iweze kutekeleza utaratibu wa kutumia zawadi, jinsi ilivyo katika ofa zinazotumika (angalia masharti ya kiufundi ili upate maelezo zaidi).
  • Badala ya kutumia upya bidhaa iliyopo ya ndani ya programu, ni lazima uweke bidhaa ya ndani ya programu ambayo utaitumia tu kwa ajili ya zawadi za kujisajili mapema.

Ukiamua kutumia zawadi za kujisajili mapema na ushindwe kuwasilisha zawadi kwa watumiaji, tunaweza kusimamisha programu yako kwenye Duka la Google Play.

Masharti ya utekelezaji wa kiufundi
  • Unatakiwa kuanzisha SKU ya bidhaa ya ndani ya programu inayodhibitiwa (kwa mfano, kipengee kilicho ndani ya programu, herufi maalum, kifurushi cha sarafu) ambayo Google Play itawapa watumiaji wanaojisajili mapema.
  • Kabla ya kuanzisha kampeni yako ya kujisajili mapema, bidhaa ya ndani ya programu ambayo unatumia katika zawadi za kujisajili mapema sharti iwe inatumika.
  • Kama ilivyo katika utumiaji wa ofa, ni lazima programu yako iweze kutumika kwa njia ya kiufundi wakati developerPayload na orderId hazipatikani.
  • Watumiaji wanapopokea zawadi, unapaswa kuwaarifu ndani ya muda unaofaa kupitia ujumbe wa ndani ya mchezo.
    • Kumbuka: Unaweza kukamilisha kazi ya kiufundi inayohitajika ili utume ujumbe kwa watumiaji katika kipindi kilicho kati ya wakati wa kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema na wakati wa kuzindua programu yako kikamilifu.
Kujumuisha zawadi ya kujisajili mapema na kuweka mipangilio yake

Kabla ya kuanzisha ujisajili wa mapema katika nchi yoyote ambako ungependa kutumia zawadi za kujisajili mapema, hakikisha umeweka mipangilio ya zawadi ya kujisajili mapema ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanaojisajili mapema wanapokea zawadi zao. Ili kufungua na kuweka mipangilio ya zawadi ya kujisajili mapema, chukua hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Chagua kichupo cha Zawadi.
  5. Chagua iwapo ungependa kuwapa watumiaji zawadi ya kujisajili mapema:
    • Usiwape watumiaji zawadi ya kujisajili mapema: Ukiteua chaguo hili, unahitaji kuhifadhi mabadiliko uliyofanya kabla ya kwenda kwenye Hatua ya 5: Kuanzisha usajili wa mapema.
    • Wape watumiaji zawadi ya kujisajili mapema: Ukiteua chaguo hili, endelea na hatua zifuatazo.
  6. Kagua na ukubali Sheria na Masharti ya zawadi ya Kujisajili mapema.
  7. Katika hatua hii, ikiwa hujaweka bidhaa ya ndani ya programu, utaona ujumbe ukikudokezea uiweke. Badala ya kutumia bidhaa iliyopo ya ndani ya programu, ni sharti uweke bidhaa ya ndani ya programu ambayo utaitumia tu kwa ajili ya zawadi za kujisajili mapema. Jaza maelezo yafuatayo kwenye sehemu ya “Weka zawadi ya kujisajili mapema”:
    • Bidhaa: Chagua bidhaa yako kwenye menyu kunjuzi.
    • Beji ya zawadi (si lazima): Beji hii itaonyeshwa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play karibu na zawadi ya kujisajili mapema.
    • URL za Sheria na Masharti: Weka kiungo cha kufikia Sheria na Masharti yako ambayo ni sharti watumiaji wayakubali kabla ya kupokea zawadi. Unaweza kuweka viungo vya ziada kwa nchi au maeneo tofauti.
  8. Chagua Hifadhi kisha Anzisha ili uthibitishe kuwa ungependa kujumuisha zawadi ya kujisajili mapema.
    • Kumbuka: Watumiaji wataona zawadi hiyo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Huwezi kubadilisha au kuondoa zawadi wakati kampeni yako ya kujisajili mapema inaendelea.
Kuondoa zawadi ya kujisajili mapema

Huwezi kubadilisha zawadi ya kusajili mapema wakati una kampeni ya kujisajili mapema inayoendelea, lakini unaweza kufanya hivyo iwapo kampeni yako bado haijaanza au hakuna nchi au maeneo ambako kampeni za kujisajili mapema zinaendelea. Ili kuondoa zawadi ya kujisajili mapema, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua mchezo au programu ambako ungependa kuondoa zawadi ya kujisajili mapema.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Chagua kichupo cha Zawadi.
  5. Chagua Usiwape watumiaji zawadi ya kujisajili mapema.
  6. Chagua Hifadhi kisha Ondoa ili uthibitishe kuwa ungependa kuondoa zawadi ya kujisajili mapema.
    • Kumbuka: Watumiaji hawataiona zawadi hii kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Huwezi kuweka zawadi mpya wakati kampeni yako ya kujisajili mapema inaendelea.
Kujaribu utoaji wa zawadi ya kujisajili mapema kabla ya kuzindua programu yako

Kwa kuwa zawadi za kujisajili mapema ni sawa na ofa, unaweza kutumia njia sawa kuzijaribu. Ili ujaribu utoaji wa zawadi ya kujisajili mapema, tengeneza na utumie kuponi ya ofakwenye Dashibodi ya Google Play kwa bidhaa ya ndani ya programu unayotumia kama zawadi.

Hatua ya 5: Kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema

Baada ya kubainisha vifaa vinavyotumika, kuchagua nchi ambako ungependa kampeni yako iendeshwe na kuamua iwapo ungependa au hungependa kutoa zawadi ya kujisajili mapema, utakuwa tayari kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema.

Baada ya kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema, hakikisha umetangaza kampeni yako ukitumia URL ya mchezo au programu yako kwenye ukurasa wa kujisajili mapema katika Google Play kwenye vituo vyako vyote vya utangazaji. Vituo maarufu unavyoweza kutumia ni pamoja na viungo mahususi kwenye tovuti za wengine, mitandao jamii, makala kwenye vyombo vya habari na majarida ya barua pepe.

Kuanzisha kampeni yako ya kujisajili mapema

Ili kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu au mchezo ambako ungependa kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Chagua Anzisha kampeni ya kujisajili mapema.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kuanzisha kampeni ya kujisajili mapema, sehemu ya “Muhtasari wa kikundi” kwenye ukurasa wa Kujisajili mapema ambayo kufikia sasa haikuwa na kitu chochote, itawekwa maelezo ya kujisajili mapema ya toleo lako.

Kudhibiti kampeni ya kujisajili mapema

Kampeni yako ya kujisajili mapema inapoendelea, kuna shughuli mbalimbali za usimamizi ambazo zinaweza kukusaidia, kama vile kuangalia takwimu, kuangalia muda uliosalia katika nchi au maeneo tofauti na kufanya majaribio. Huenda shughuli hizi zikakufaa unapotayarisha uzinduzi wa mchezo au programu yako.

Kuangalia vipimo muhimu vya utendaji wa kampeni ya kujisajili mapema

Ili kuangalia vipimo muhimu vya utendaji wakati na baada ya kampeni yako ya kujisajili mapema, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua mchezo au programu uliyojumuisha kwenye kampeni ya kujisajili mapema.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  4. Weka mipangilio ya ripoti ukitumia vipimo viwili kati ya vinavyopatikana kwa usajili wa mapema:
    • Watumiaji waliojisajili mapema: Idadi ya watumiaji waliojisajili mapema kupata programu yako.
    • Kushawishika: Idadi ya watumiaji waliojisajili mapema ambao wamesakinisha programu ndani ya siku 14 baada ya programu kupatikana. Idadi hii inajumuisha watumiaji waliojisajili mapema ambao wamesakinisha programu kupitia toleo la Beta na njia nyingine za jaribio la kabla ya uzinduzi.
  5. Baada ya kuchagua vipimo ambavyo ungependa kuangalia, hifadhi ripoti yako.

Unaweza pia kuangalia muhtasari wa takwimu za kujisajili mapema kwa kuchagua programu kisha kuangalia maelezo ya toleo kwenye ukurasa wa Muhtasari wa matoleo au kwenye sehemu ya “Muhtasari wa kikundi” katika ukurasa wa Kujisajili mapema.

Kuangalia muhtasari wa takwimu za kujisajili mapema

Baada ya kuanza kutumia kipengele cha kujisajili mapema, ni sharti ufuatilie muda uliosalia kwa kampeni yako katika kila nchi au eneo ambako umefanya kipengele cha kujisajili mapema kipatikane. Usipozindua kampeni ya kujisajili mapema ndani ya siku 90 katika mojawapo ya nchi hizi, tutaisitisha katika nchi zote na hutaweza kuanzisha kampeni mpya ya kujisajili mapema.

Ili uangalie takwimu za muhtasari wa kujisajili mapema, ufuatilie muda uliosalia kwa kampeni yako katika kila nchi na uone hali ya kampeni yako katika kila nchi, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua mchezo au programu uliyojumuisha kwenye kampeni ya kujisajili mapema.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Majaribio > Kujisajili mapema.
  4. Tafuta toleo lako la usajili wa mapema katika sehemu ya "Muhtasari wa kikundi" kisha ukague maelezo, ambayo yatajumuisha yafuatayo:
    • Hali ya kujisajili mapema
      • Rasimu au Inakaguliwa: Kampeni imeidhinishwa katika nchi au eneo husika na inakaguliwa.
      • Imeanzishwa: Kampeni ya kujisajili mapema inaendelea na sharti uzindue programu yako kwa umma kabla ya tarehe iliyobainishwa (hadi siku 90).
      • Muda wake umekwisha: Kampeni ya kujisajili mapema imepitisha siku 90 zinazoruhusiwa na sharti uzindue programu yako haraka iwezekanavyo.
      • Katika toleo la umma: Kampeni ya kujisajili mapema inapatikana kwa watu wote au programu imezinduliwa kwa umma katika nchi hii bila kampeni ya kujisajili mapema kuendeshwa kwanza katika nchi husika.
      • Haiendelei: Kampeni ya kujisajili mapema imesitishwa (kikomo cha siku 90 bado kinatumika).
      • Haijaanzishwa: Kampeni ya kujisajili mapema bado haijaanzishwa.
    • Idadi ya waliojisajili
    • Idadi ya vifaa vinavyoweza kutumika
    • Idadi ya nchi au maeneo uliyoweka
Kuzindua programu au mchezo wako baada ya kampeni ya kujisajili mapema

Ukiwa tayari kuzindua programu au mchezo wako na kutamatisha kampeni yako ya kujisajili mapema, fuata hatua zifuatazo ili kuchagua nchi ambako ungependa mchezo au programu yako ipatikane. Baada ya kuchapisha mchezo au programu yako kwa umma, watumiaji waliojisajili mapema watapokea arifa kutoka Duka la Google Play kuwajulisha kuwa programu au mchezo unapatikana na unaweza kupakuliwa; na programu au mchezo utasakinishwa kiotomatiki kwenye vifaa vinavyostahiki.

Ili kuzindua programu au mchezo wako baada ya kampeni ya kujisajili mapema, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua mchezo au programu unayotaka kuzindua.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Jaribu > Toleo la umma.
  4. Chagua kichupo cha Nchi au maeneo.
  5. Chagua Weka nchi au maeneo.
  6. Chagua nchi au maeneo ambako ungependa programu yako ipatikane.
  7. Chagua Hifadhi.

Muhimu: Ili programu yako ipatikane kwenye Google Play katika nchi unazochagua, hakikisha umechapisha mchezo au programu yako kwa umma.

Kufanya majaribio wakati wa kujisajili mapema

Unaweza kutumia kipengele cha kujisajili mapema pamoja na vipengele vingine vya uzinduzi wa mapema kwenye Dashibodi ya Google Play, ikijumuisha majaribio ya kabla ya uzinduzi. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kutumia usajili wa mapema na kufanya majaribio kwa wakati mmoja:

  • Unaweza kuendesha kampeni ya kujisajili mapema katika nchi unazochagua na ufanye majaribio ya kabla ya uzinduzi kwa wakati mmoja katika nchi zingine.
  • Ikiwa unafanya jaribio la watumiaji wengi au watumiaji wachache katika nchi ambako sasa ungependa mchezo au programu yako ipatikane kwa usajili wa mapema, bado unaweza kwenda kwenye usajili wa mapema. Baada ya kwenda kwenye usajili wa mapema katika nchi hiyo, zingatia yafuatayo:
    • Watumiaji ambao tayari wamejiunga kwenye jaribio lako wataendelea kupokea masasisho unayotoa kwenye toleo lao husika. Watumiaji wengine wataona kitufe cha Jisajili mapema badala ya kitufe cha Sakinisha kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.
    • Kumbuka: Ukianzisha kampeni ya kujisajili mapema katika nchi ambako tayari unafanya jaribio la watumiaji wengi, watumiaji katika nchi hiyo hawataweza tena kujijumuisha kwenye jaribio lako kupitia ukurasa wa programu yako katika Google Play, lakini bado wanaweza kujiunga kupitia URL ya kujijumuisha inayopatikana. kwenye Dashibodi ya Google Play.
      • Ili upate URL ya kujijumuisha kwenye jaribio lako, ingia kwenye Dashibodi ya Google Play, kisha nenda kwenye Toleo > Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi au Jaribio la watumiaji wengi halafu uchague kichupo cha Wanaojaribu.
      • URL ya kujijumuisha katika jaribio lako itakuwa: https://play.google.com/apps/testing/jina la kifurushi cha programu au mchezo wako
      • Kwa mfano: Ikiwa jina la kifurushi cha programu yako ni your.new.app, URL ya kujijumuisha kwenye jaribio lako itakuwa: https://play.google.com/store/apps/testing/your.new.app
    • Watumiaji ambao tayari wamejiunga kwenye jaribio lako hawataweza kujisajili mapema hadi watakapoondoa programu au kujiondoa katika mpango wa kujaribu programu yako.
    • Ikiwa tayari umeanzisha kampeni ya kujisajili mapema katika nchi ambako baadaye ungependa kufanya jaribio la watumiaji wengi au la watumiaji mahususi, ni muhimu kujua kwamba unapochapisha toleo la jaribio kwa nchi hiyo, watumiaji wanaostahiki na waliojijumuisha kushiriki majaribio watapokea arifa ya kujisajili mapema inayowaomba kusakinisha programu. Hawatapokea arifa inayofuata baada ya kuzindua programu au mchezo wako katika kundi la umma. Kwa majaribio ya watumiaji mahususi, watumiaji uliowaalika na wamejijumuisha kwenye mpango wa kujaribu watapokea arifa.

Maudhui yanayohusiana

  • Pata maelezo zaidi kuhusu Kuimarisha kasi ya matukio ya kabla ya uzinduzi wa kujisajili mapema katika Chuo cha Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9025735633628306551
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false