Weka jaribio la watumiaji wengi, watumiaji mahususi au la ndani

Muhimu: Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Ukitumia Dashibodi ya Google Play, unaweza kujaribu programu yako ukitumia makundi mahususi ya watumiaji au kwa kuweka wazi jaribio lako kwa watumiaji wa Google Play.

Kitendo cha kujaribu programu yako kinakuruhusu kurekebisha matatizo yoyote ya kiufundi au ya hali ya utumiaji yenye athari chache zaidi kwa watumiaji, ili uweze kuchapisha toleo bora la programu yako kwenye Google Play.

Kabla ya kuanza

  • Masharti ya barua pepe: Watumiaji wanahitaji Akaunti ya Google (@gmail.com) au akaunti ya Google Workspace ili waweze kufanya jaribio.
  • Mabadiliko kwenye uchumaji wa mapato:: Ikiwa utafanya mabadiliko kwenye bei ya programu yako, hatua hii huathiri matoleo ya sasa na ya baadaye ya programu yako kwenye vikundi vyote.
  • Mabadiliko kwenye upatikanaji katika nchi: Iwapo utafanya mabadiliko yoyote katika nchi na maeneo ambako programu yako husambazwa, hatua hii huathiri matoleo ya sasa na ya baadaye ya programu yako kwenye vikundi vyote.
  • Toleo:
    • Ni lazima ujaribu programu yako kabla ya kuichapisha kwenye toleo la umma.
    • Baada ya kuchapisha jaribio la watumiaji wengi, watumiaji mahususi au la ndani kwa mara ya kwanza, inaweza kuchukua saa kadhaa kabla ya kiungo chako cha jaribio kupatikana kwa wachunguzaji. Iwapo utachapisha mabadiliko ya ziada, huenda yatachukua saa kadhaa kabla ya kupatikana kwa wachunguzaji.
  • Weka mashirika kwenye jaribio:
    • Ili uweke wachunguzaji wanaohusiana na shirika linalotumia Google Play ya kikazi, nenda kwenye kichupo cha Google Play ya Kikazi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina ya programu yako (Weka > Mipangilio ya kina) kisha uchague kisanduku kilicho karibu na "Washa."
    • Iwapo programu yako ni ya matumizi ya faragha, unahitaji pia kuweka shirika linalohusishwa na jaribio lako kwenye orodha ya wanaolengwa.
  • Maoni: Maoni kutoka kwa watumiaji wako wanaojaribu hayataathiri ukadiriaji wa umma wa programu yako.
  • Programu zinazolipishwa: Iwapo unafanya jaribio la programu inayolipishwa ukitumia jaribio la watumiaji wengi au mahususi, bado wachunguzaji wanahitaji kuinunua. Iwapo unafanya jaribio la programu inayolipishwa ukitumia jaribio la ndani, wanaojaribu wanaweza kuisakinisha programu yako bila malipo.

Tofauti kati ya jaribio la ndani, la watumiaji mahususi na la watumiaji wengi

Unaweza kuweka matoleo kwenye vikundi vitatu vya kujaribu kabla ya kuchapisha programu yako kwenye toleo la umma. Kila awamu ya kujaribu hukusaidia ukusanye maoni unayohitaji ili kuboresha programu yako wakati inasanidiwa.

Jaribio la ndani: Unda toleo la jaribio la ndani ili usambaze kwa haraka programu yako kwa hadi wachunguzaji 100 kwa ajili ya kuhakikisha ubora wa programu mapema. Tunapendekeza ufanye jaribio la ndani kabla ya kuchapisha programu yako kwa vikundi vya watumiaji mahususi au wengi. Panapohitajika, unaweza kufanya jaribio la ndani sambamba na jaribio la watumiaji wengi na wachache kwa matoleo tofauti ya programu yako. Unaweza kuanzisha jaribio la ndani kabla hujamaliza kusanidi programu yako.

Jaribio la watumiaji mahususi: Unda toleo la jaribio la watumiaji mahususi ili ujaribu matoleo ya mapema ya programu yako kwa kutumia idadi pana ya wachunguzaji ili ukusanye maoni zaidi yanayolengwa. Baada ya kujaribu toleo kwa kutumia kikundi kidogo cha waajiriwa au watumiaji unaowaamini, unaweza kupanua jaribio lako kwa watumiaji wengi. Kwenye ukurasa wako wa Jaribio la watumiaji mahususi, toleo la jaribio la watumiaji mahususi litapatikana kama jaribio lako la kwanza la watumiaji mahususi. Panapohitajika, unaweza pia kuunda na kuvipa majina vikundi vya ziada vya watumiaji mahususi.

Kama unajaribu programu iliyopo na ambayo umechapisha hapo awali, watumiaji walio kwenye kundi lako la jaribio ndio pekee watakaopokea sasisho la toleo lako la jaribio la watumiaji mahususi.

Jaribio la watumiaji wengi: Unda toleo la jaribio la watumiaji wengi ili ufanye jaribio ukitumia kikundi kikubwa na uweke toleo la jaribio la programu yako kwenye Google Play. Ukifanya jaribio la watumiaji wengi, mtu yeyote anaweza kujiunga na mradi wako wa kufanya jaribio na akupe maoni kwa faragha. Kabla ya kuteua chaguo hili, hakikisha kuwa programu na ukurasa wa programu yako katika Google Play viko tayari kuonekana kwenye Google Play.

Kunja Zote Panua Zote

Vidokezo

Nitaanzaje?

Tunapendekeza uanze na jaribio la ndani, kisha ulipanue kwa kikundi kidogo cha jaribio la wachunguzaji wachache. Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play na, pia, kabla ya kuweza kutumia kipengele cha kujisajili mapema. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Kwa nini ninahitaji kufanya jaribio la ndani?

Unapounda toleo la jaribio la ndani, unaweza kuchapisha programu yako papo hapo kwa watumiaji wa jaribio la ndani. Kufanya hivyo kunaweza kukusaidia kutambua matatizo na kupokea maoni mapema unaposanidi programu. Jaribio la ndani lina sifa zifuatazo:

  • Haraka: Unaweza kusambaza programu kupitia toleo la jaribio la ndani kwa haraka zaidi kuliko matoleo ya majaribio ya watumiaji wengi au ya watumiji mahususi. Unapochapisha Android App Bundle mpya kwenye toleo la jaribio la ndani, itapatikana kwa wanaojaribu baada ya dakika chache.
    • Kumbuka: Iwapo unachapisha programu kwa mara ya kwanza, itapatikana tu mara moja kwa wanaofanya jaribio la ndani, lakini itakuwa na jina la muda na maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play kwa hadi saa 48.
  • Kubadilishwa kwa urahisi: Unaweza kubadilisha majaribio ya ndani ili yatumike katika hatua tofauti za kujaribu, kama vile kuhakikisha ubora na kutatua hitilafu zinazoweza kutokea baada ya kuzindua programu.
  • Salama: Ukitumia kikundi cha jaribio la ndani, programu unayojaribu husambazwa kwa njia salama kwa watumiaji kupitia Duka la Google Play.
Ninaweza kufanya majaribio kadhaa kwa kila programu kwa wakati mmoja?

Kama unataka kufanya majaribio kadhaa kwenye programu moja, zingatia mambo yafuatayo:

  • Unaweza kufanya majaribio mengi ya watumiaji mahususi na jaribio moja la watumiaji wengi wakati wowote.
  • Mtumiaji anayejijumuisha katika jaribio la ndani la programu yako hatastahiki tena kupokea jaribio la watumiaji wengi au watumiaji mahususi. Ili uweze kufikia jaribio la watumiaji wengi au mahususi, ni lazima mtumiaji aondoke kwenye jaribio la ndani na arudi kwenye jaribio la watumiaji wengi au la watumiaji mahususi.

Hatua ya 1: Kuweka maelezo ya jaribio

Chagua njia ya kufanya majaribio

Jaribio la ndani: dhibiti hadi watumiaji 100 wanaojaribu

Unaweza kuunda orodha ya wanaojaribu programu kupitia anwani ya barua pepe. Jaribio la ndani linaweza kuwa na hadi watumiaji 100 wanaojaribu kila programu.

Unapoanzisha jaribio la ndani, kumbuka yafuatayo:

  • Usambazaji katika nchi: Unaweza kuweka watumiaji kutoka eneo lolote kwenye jaribio lako la ndani. Ikiwa mtumiaji anayefanya jaribio la ndani anapatikana katika nchi ambako toleo la umma la watumiaji wengi au mahususi la programu yako halipatikani, bado mtumiaji atapokea uwezo wa kufikia jaribio la ndani.
  • Malipo: Kwa programu zinazolipishwa, wachunguzaji wanaweza kusakinisha toleo lako la jaribio la ndani bila malipo. Wachunguzaji wanahitaji kulipia ununuzi wa ndani ya programu isipokuwa wawe pia wameongezwa kwenye orodha ya wachunguzaji wenye leseni.
  • Masharti ya kutojumuisha kifaa: Masharti ya kutojumuisha kifaa hayatumiki kwa wanaofanya jaribio la ndani.
  • Ukaguzi wa sera na usalama: Majaribio ya ndani huenda yasitegemee sera ya kawaida ya Google Play au ukaguzi wa usalama. Programu zinazotumika kwenye matoleo ya majaribio ya ndani hazijumuishwi katika Sehemu ya usalama wa data ya Google Play.

Anzisha jaribio la ndani

Tunga orodha ya anwani za barua pepe za wachunguzaji wa programu yako:

Iwapo tayari umetunga orodha ya barua pepe, nenda kwenye sehemu ya maagizo ya "Weka wachunguzaji".

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la ndani (Jaribio > Jaribio la ndani).
  2. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  3. Chini ya "Wachunguzaji," chagua Tunga orodha ya barua pepe.
  4. Weka jina la orodha. Unaweza kutumia orodha hiyo kufanya majaribio ya baadaye kwenye programu zako zozote.
  5. Weka anwani za barua pepe zilizotengwa kwa koma au ubofye Pakia faili ya CSV. Ikiwa unatumia faili ya .CSV, weka kila anwani ya barua pepe kwenye mstari wake bila koma zozote.
    • Kumbuka: Ukipakia faili ya .CSV, itabatilisha anwani zozote za barua pepe ulizoweka.
  6. Chagua Hifadhi mabadiliko, kisha Tunga.

Weka wanaojaribu

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la ndani (Jaribio > Jaribio la ndani).
  2. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  3. Kwenye jedwali la "Wachunguzaji", chagua orodha za watumiaji ambazo ungependa kutumia kujaribu toleo lako.
  4. Weka URL ya maoni au anwani ya barua pepe ili ukusanye maoni kutoka kwa wachunguzaji. Njia ya kutoa maoni kuhusu programu yako itaonyeshwa kwa watumiaji kwenye ukurasa wa kujijumuisha wa wanaojaribu.
  5. Nakili kiungo kinachoweza kushirikiwa ili ushiriki toleo na wanaojaribu.
  6. Chagua Hifadhi mabadiliko.

Jaribu programu ambazo hazijawekewa mipangilio kikamilifu

Unaweza pia kubuni toleo la jaribio la ndani iwapo programu yako haijawekewa mipangilio kikamilifu. Pindi unapopata App Bundle sahihi, unaweza kuisambaza haraka kwa idadi ndogo ya wanaojaribu. Iwapo ungependa kujaribu programu ambayo haijawekewa mipangilio kikamilifu, unapaswa kukumbuka yafuatayo:

  • Kabla programu ikaguliwe kwa mara ya kwanza, watumiaji wataona jina linalotumika kwa muda mfupi la programu hiyo kwenye Google Play. Unaweza kupata jina la programu yako linalotumika kwa muda mfupi kwenye muhtasari wa programu katika Dashibodi ya programu yako.
  • Pindi unapopakia vizalia vya programu, jina la kifurushi cha programu hilo haliwezi kubadilishwa.
Jaribio la watumiaji mahususi: dhibiti wachunguzaji kulingana na anwani ya barua pepe au Vikundi kwenye Google

Ukitumia jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kutunga orodha ya wachunguzaji kwa kutumia anwani ya barua pepe. Unaweza kuunda jumla ya orodha 200 na kila orodha inaweza kuwa na hadi watumiaji 2,000. Unaweza kuweka hadi orodha 50 kwa kila kundi.

Weka maelezo yanayohitajika ili kuandaa toleo la jaribio lako la ndani, hifadhi mabadiliko uliyofanya na uchague Kagua toleo.

Anza jaribio la watumiaji mahususi

Tunga orodha ya anwani za barua pepe za wachunguzaji wa programu yako

Iwapo tayari umetunga orodha ya wanaojaribu, nenda kwenye sehemu ya maagizo ya "Weka wanaojaribu".

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la watumiaji mahususi (Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi).
  2. Chagua Dhibiti kikundi.
  3. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  4. Chini ya "Wachunguzaji," chagua Tunga orodha ya barua pepe.
  5. Weka jina la orodha. Unaweza kutumia orodha hiyo kufanya majaribio ya baadaye kwenye programu zako zozote.
  6. Weka anwani za barua pepe zilizotengwa kwa koma au ubofye Pakia faili ya CSV. Ikiwa unatumia faili ya .CSV, weka kila anwani ya barua pepe kwenye mstari wake bila koma zozote.
    • Kumbuka: Ukipakia faili ya .CSV, itabatilisha anwani zozote za barua pepe ulizoweka.
  7. Chagua Hifadhi mabadiliko, kisha Tunga.

Weka wanaojaribu

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la watumiaji mahususi (Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi).
  2. Chagua Dhibiti kikundi.
  3. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  4. Kwenye sehemu ya "Wachunguzaji", unaweza kuongeza wachunguzaji kupitia barua pepe au Vikundi kwenye Google:
    • Barua pepe: Barua pepe huchaguliwa kiotomatiki. Iwapo ungependa kutumia barua pepe, chagua tu orodha za watumiaji ambazo ungependa kutumia kujaribu toleo lako.
    • Vikundi kwenye Google: Chagua Vikundi kwenye Google na uweke anwani za barua pepe za Vikundi kwenye Google, ambazo zinatumia muundo: yourgroupname@googlegroups.com. Watumiaji ambao ni wanachama wa Vikundi kwenye Google utakaowaweka ndio tu wataweza kujiunga kwenye jaribio lako.
  5. Weka URL ya maoni au anwani ya barua pepe ili ukusanye maoni kutoka kwa wachunguzaji. Njia ya kutoa maoni kuhusu programu yako itaonyeshwa kwa watumiaji kwenye ukurasa wa kujijumuisha wa wanaojaribu.

  6. Nakili kiungo kinachoweza kushirikiwa ili ushiriki toleo na wanaojaribu.

  7. Chagua Hifadhi mabadiliko.
Jaribio la watumiaji mahususi: simamia wachunguzaji wa programu kupitia shirika

Kupitia jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kuchagua shirika linaloweza kufikia kikundi chako. Wasimamizi wa mashirika haya wanaweza kuwaruhusu watumiaji kujaribu toleo lako.

Tunapendekeza uweke tu wachunguzaji kupitia Dashibodi ya Google Play au kutoka kwenye ukurasa wa mipangilio ya Programu ya Android katika dashibodi ya Msimamizi wa Google. Iwapo mtumiaji amechaguliwa kujaribu programu kwenye Dashibodi ya Google Play na dashibodi ya Msimamizi, atapata toleo la juu zaidi kati ya matoleo yote ya programu yanayopatikana.

Ili uweke wanaojaribu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la watumiaji mahususi (Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi).
  2. Chagua Dhibiti kikundi.
  3. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  4. Katika sehemu ya "Simamia mashirika", chagua Weka shirika.
  5. Weka Kitambulisho na jina la shirika ambalo linaweza kufikia kikundi chako.
  6. Chagua Ongeza.
  7. Chagua Hifadhi mabadiliko.
Jaribio la watumiaji wengi: weka programu yako ya jaribio kwenye Google Play

Iwapo utaweka jaribio la watumiaji wengi, watumiaji wataweza kupata programu yako ya jaribio kwenye Google Play. Hakikisha kuwa programu yako iko tayari kuonekana kwenye Google Play kabla ya kuteua chaguo hili.

  • Kwa programu za matoleo ya Beta (programu mpya ambazo hazijachapishwa katika toleo la umma): Watumiaji wanaweza kupata jaribio la watumiaji wengi kupitia utafutaji kwenye Google Play. Baada ya watumiaji kupata ukurasa wa programu yako katika Google Play, wanaweza kusakinisha na kutumia programu yako.
  • Kwa programu zilizo na toleo lililochapishwa kwa umma: Watumiaji wanaweza kujijumuisha kwenye jaribio lako la watumiaji wengi kupitia ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Unaweza pia kushiriki kiungo cha URL kwenye tovuti au barua pepe. Kila mtumiaji aliye na kiungo anaweza kufikia jaribio la watumiaji wengi.

Kuanza jaribio la watumiaji wengi

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la watumiaji wengi (Jaribio > Jaribio la watumiaji wengi).
  2. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  3. Panua sehemu ya "Simamia wachunguzaji". Iwapo sehemu ya "Dhibiti wanaojaribu" haina kitu, hakikisha umepakia App Bundle.
  4. Chagua idadi ya watumiaji wanaoweza kujaribu programu yako:
    • Bila kikomo: Chaguo hili huteuliwa kwa chaguomsingi.
    • Idadi ndogo: Unaweza kubainisha kikomo (sharti kiwe angalau 1,000).
  5. Weka URL ya maoni au anwani ya barua pepe ili ukusanye maoni kutoka kwa wachunguzaji. Njia ya kutoa maoni kuhusu programu yako itaonyeshwa kwa watumiaji kwenye ukurasa wa kujijumuisha wa wanaojaribu.
  6. Nakili kiungo kinachoweza kushirikiwa ili ushiriki toleo na wanaojaribu.
  7. Chagua Hifadhi mabadiliko.
Unda makundi zaidi ya jaribio la watumiaji mahususi kwa ajili ya timu zako za usanidi

Katika hali zingine, unaweza kuhitaji makundi zaidi ya jaribio la watumiaji mahususi. Kwa mfano, unaweza kuwa na timu tofauti za usanidi ambazo zinahitaji kushughulikia hitilafu katika vipengele tofauti. Iwapo kila timu itabuni kikundi chake cha jaribio, timu zitaweza kushughulikia vipengele tofauti kwa wakati mmoja.

Kwa kutumia vikundi vya ziada vya majaribio, unaweza kutunga orodha ya wanaojaribu kwa kutumia anwani za barua pepe au kudhibiti wanaojaribu kwa kutumia Google Groups. Hakuna vikwazo vya idadi ya watu walio katika vikundi hivi.

Anzisha kundi la ziada la jaribio

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Jaribio la watumiaji mahususi (Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi).
  2. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, chagua Anzisha.
  3. Weka jina la kikundi. Jina la kundi hili linatumika kwenye Dashibodi ya Google Play na API ya Wasanidi Programu wa Google Play kama jina la lakabu la kundi.
  4. Chagua Unda kundi.
  5. Chagua kichupo cha Wachunguzaji.
  6. Kwenye sehemu ya "Wachunguzaji", unaweza kuongeza wachunguzaji kupitia barua pepe au Vikundi kwenye Google:
    • Barua pepe: Barua pepe huchaguliwa kiotomatiki. Iwapo ungependa kutumia barua pepe, chagua tu orodha za watumiaji ambazo ungependa kutumia kujaribu toleo lako.
    • Vikundi kwenye Google: Chagua Vikundi kwenye Google na uweke anwani za barua pepe za Vikundi kwenye Google, ambazo zinatumia muundo: yourgroupname@googlegroups.com. Watumiaji ambao ni wanachama wa Vikundi kwenye Google utakaowaongeza ndio tu wataweza kujiunga kwenye jaribio lako.
  7. Weka URL ya maoni au anwani ya barua pepe ili ukusanye maoni kutoka kwa wanaojaribu. Njia ya kutoa maoni kuhusu programu yako itaonyeshwa kwa watumiaji kwenye ukurasa wa kujijumuisha wa wanaojaribu.
  8. Nakili kiungo kinachoweza kushirikiwa ili ushiriki toleo na wanaojaribu.
  9. Chagua Hifadhi.

Usaidizi na vidokezo vya majaribio

Unapounda makundi zaidi ya jaribio la watumiaji mahususi, vipengele vifuatavyo havitumiki:

Simamia watakaojaribu Huduma za Michezo ya Google Play

Iwapo unatumia Huduma za michezo ya Google Play, vikundi vya wanaojaribu hushirikiwa kiotomatiki kati ya programu yako na Huduma za Michezo ya Google Play.

Wachunguzaji wanaweza kujaribu mabadiliko uliyohifadhi kwenye miradi ya michezo yako, kama vile mafanikio na mbao za wanaoongoza, kabla hayajachapishwa kwa watumiaji halisi. Unaweza kuwasimamia wachunguzi mahususi ukitumia anwani zao za barua pepe au utumie tena wachunguzaji sawa katika vikundi lengwa.

Kwenye ukurasa wako wa Huduma za Michezo ya Google Play > Kudhibiti na kuweka mipangilio > ukurasa wa Wachunguzaji, unaweza kutumia swichi ya wanaojaribu ili kujumuisha kiotomatiki watumiaji wowote ambao wamejijumuisha kwenye jaribio la programu yako.

Ili uweke mwenyewe watumiaji mahususi wa majaribio ya Huduma za Michezo ya Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa wachunguzaji wa Huduma za Michezo ya Google Play (Huduma za Michezo ya Google Play > Kudhibiti na kuweka mipangilio > Wachunguzaji).
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Huduma za Michezo ya Google Play > Kudhibiti na kuweka mipangilio > Wachunguzaji.
  3. Andika anwani za barua pepe ambazo ungependa kuongeza. Anwani za barua pepe sharti ziwe akaunti sahihi za Google unazoingia kwa kutumia anwani ya Michezo ya Google Play.
  4. Chagua Ongeza.

Pindi wachunguzaji wanapochagua kuingia kwenye kundi lako la jaribio, wanaweza kuingia kwa kutumia Huduma za Michezo ya Google Play, kupata mafanikio yaliyo katika hali ya rasimu au yaliyochapishwa na kuchapisha kwenye mbao za wanaoongoza zilizochapishwa au zilizo katika hali ya rasimu.

Hatua ya 2: Unda toleo

Baada ya kuweka mipangilio ya maelezo ya jaribio la programu yako, unaweza kutayarisha na kusambaza toleo.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti upatikanaji wa programu katika matoleo ya majaribio ya watumiaji mahususi na matoleo ya majaribio ya watumiaji wengi, nenda kwenye sambaza matoleo ya programu katika nchi mahususi.

Hatua ya 3: Shiriki programu yako na wachunguzaji

Iwapo unafanya jaribio la watumiaji mahususi au wengi, wachunguzi wanaweza kupata programu yako ya jaribio kwenye Google Play wakitumia kifaa chao. Iwapo ni jaribio la watumiaji mahususi, bado programu yako ya jaribio itapatikana tu kwa wachunguzaji walio kwenye orodha au kikundi chako.

Iwapo unafanya jaribio la ndani au la watumiaji mahususi kabla ya kufanya programu yako ipatikane kupitia jaribio la wengi au kuisambaza kwenye toleo la umma, wachunguzaji hawataweza kuipata kwa kuitafuta kwenye Google Play. Unahitaji kushiriki URL ya programu yako ya Duka la Google Play na wachunguzaji ili waweze kuipakua.

Iwapo kwa sababu yoyote, wanaojaribu programu yako hawawezi kuipata kwenye Google Play, una pia chaguo la kushiriki kiungo cha kujijumuisha nao. Vifuatavyo ni vidokezo vya kutumia kiungo cha kujijumuisha:

  • Kiungo cha kujijumuisha huonekana wakati programu "Imechapishwa." Programu zilizo katika hali ya "Rasimu" au "Inasubiri kuchapishwa" hazitaonyesha kiungo cha kujijumuisha.
  • Baada ya kubofya kiungo cha kujijumuisha, wachunguzaji wa programu yako watapata maelezo kuhusu maana ya kuwa mchunguzaji na kiungo cha kujijumuisha. Kila mchunguzaji anahitaji kujijumuisha akitumia kiungo.
  • Iwapo unafanya jaribio la watumiaji mahususi ukitumia Kikundi kwenye Google, watumiaji wanahitaji kujiunga kwenye kikundi kabla ya kujijumuisha kwenye jaribio lako.

Hatua ya 4: Kupata maoni

Pindi wachunguzaji wa programu yako wanapoisakinisha, wataarifiwa kiotomatiki kutumia toleo la majaribio baada ya dakika chache.

Wachunguzaji hawawezi kutoa maoni hadharani kwenye Google Play kuhusu toleo la programu yako ya jaribio. Kwa hivyo, ni vyema kujumuisha njia ya kutoa maoni au uwafahamishe watumiaji wako jinsi wanavyoweza kutoa maoni (kupitia barua pepe, tovuti, au mijadala ya ujumbe).

Iwapo unafanya jaribio la wengi au wachache, watu wanaojaribu wanaweza pia kutoa maoni ya faragha kupitia Google Play.

Hatua ya 5: Kukamilisha jaribio

Ili uondoe watumiaji kwenye jaribio la programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa majaribio ili upate jaribo ambalo ungependa kukamilisha:
  2. Pata jaribio ambalo ungependa kukamilisha na uchague Dhibiti kikundi.
    • Kumbuka: Kulingana na aina ya jaribio unalokamilisha na idadi ya majaribio unayofanya, huenda hutahitaji kutekeleza hatua hii.
  3. Karibu na sehemu ya juu kulia ya ukurasa, chagua Simamisha kikundi.
  4. Baada ya kukamilisha jaribio, wachunguzaji hawatapokea masasisho lakini programu haitaondolewa kwenye vifaa vyao.

Hali za misimbo ya matoleo na vikundi vya kujaribu

Masharti ya msimbo wa toleo

Watumiaji hupokea toleo la programu ambalo:

  • lina msimbo wa toleo jipya zaidi ambalo linaoana na kifaa chao na
  • limechapishwa kwenye kikundi wanachostahiki kupokea.

Watumiaji wote wanastahiki kila wakati kupokea kikundi cha Toleo la umma . Ikiwa App Bundle yenye msimbo wa toleo jipya imechapishwa katika kikundi cha Toleo la umma badala ya kwenye kikundi cha jaribio ambacho mtumiaji amejijumuisha, mtumiaji atapokea toleo la umma.

Ili mtumiaji atimize masharti ya kupokea kikundi cha jaribio, ni sharti:

  • ajumuishwe kwenye mipangilio ya kikundi kinachosimamiwa na
  • achague kujijumuisha katika mpango wa jaribio husika

Watumiaji wanaostahiki kupokea vikundi vingi watapokea msimbo wa toleo jipya zaidi lililochapishwa kwenye vikundi hivyo. Kwa mfano, watumiaji walio katika jaribio la watumiaji wengi wanastahiki majaribio yote mawili ya kikundi cha Toleo la umma na kikundi cha Jaribio la watumiaji wengi . Watumiaji walio katika jaribio la watumiaji mahususi wanastahiki majaribio yote mawili ya kikundi chaToleo la umma na la kikundi chaWatumiaji mahususi . Watumiaji katika majaribio ya watumiaji wengi na majaribio ya watumiaji mahususi wanastahiki kujijumuisha katika vikundi vya Toleo la umma, Jaribio la watumiaji wengi na Jaribio la watumiaji mahususi.

Watumiaji waliojijumuisha katika jaribio la ndani hawastahiki kwenye jaribio la watumiaji wengi na jaribio la watumiaji mahususi, hata kama wamejumuishwa kama wachunguzaji. Watumiaji hawa hawatapokea msimbo wa toleo jipya zaidi uliochapishwa kwenye vikundi hivyo na watapokea tu msimbo wa toleo uliochapishwa kwenye kikundi cha Jaribio la ndani.

Kwa maelezo zaidi, angalia Toleo la programu yako.

Hali za vikundi vya majaribio

Wakati unasambaza toleo lako, unaweza kuona ujumbe wa uthibitishaji unaoonyesha wakati watumiaji wa kikundi fulani wanapokea masasisho ya programu kutoka kwenye kikundi kingine–kinachojulikana kama hali mbadala ya kikundi.

Hali na masharti ya kibadala

  • Iliyodhibitiwa: App Bundle moja hudhibiti App Bundle nyingine inapotumika kama sehemu au usanidi wote wa kifaa na ina msimbo wa toleo jipya zaidi.
  • Iliyokuzwa: App Bundle zote za kikundi zinazotumika zinapatikana katika App Bundle mbadala za kikundi zinazotumika (kwa mfano, matoleo yote ya jaribio la watumiaji wengi yanayotumika ya App Bundles pia yanatumika katika toleo la umma). Huenda ukaona hii ikiwa utachapisha toleo la kwanza kwenye kikundi cha jaribio na kisha uchapishe App Bundle zilizofanyiwa jaribio kwenye toleo thabiti zaidi.
  • Za zamani: App Bundle zinazotumika katika kikundi ni za zamani na nafasi yake zimechukuliwa na App Bundle zinazotumika zenye msimbo wa toleo jipya zaidi katika kikundi mbadala. Hakuna App Bundle zozote katika kikundi zinazotumiwa na watumiaji kwa kuwa watapata App Bundle kutoka kwenye kikundi mbadala. Hii inamaanisha kwamba mpango wa kufanya majaribio unaowakilishwa na kikundi cha zamani ulikomeshwa.
  • Iliyodhibitiwa kiasi: Angalau mojawapo ya App Bundle zinazotumika katika kikundi inadhibitiwa na App Bundle yenye msimbo wa toleo jipya zaidi katika kikundi mbadala. Hii inamaanisha kwamba baadhi ya watumiaji wa matoleo ya majaribio ya watumiaji wengi watasambaziwa App Bundle kutoka kwenye toleo la jaribio la watumiaji wengi, huku wengine huenda wakatumia App Bundle kutoka toleo la umma. Hii mara nyingi huwa ni hitilafu katika kukabidhi misimbo ya toleo.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3704506133586663417
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false