Shiriki APK na vifurushi vya programu ndani ya kampuni

Kuanzia Agosti 2021, programu mpya zitatakiwa kuchapishwa kwa kutumia Android App Bundle kwenye Google Play. Programu mpya zenye ukubwa wa zaidi ya MB 200 zinaweza kutumia Play Asset Delivery au Utumaji wa Vipengele vya Google Play.

Kuanzia tarehe 30 Juni 2023, Google Play haitaruhusu tena masasisho ya programu ya televisheni kwa kutumia APK. Masasisho yote ya programu ya televisheni lazima yachapishwe kwa kutumia Android App Bundle (AAB).

Ili upate maelezo zaidi, soma makala ya Mustakabali wa Android App Bundles umewadia, kwenye Blogu ya Wasanidi Programu wa Android.

Kwa kushiriki programu ndani ya kampuni, unaweza kushiriki kwa haraka Android App Bundle na timu yako na wanaojaribu programu ndani ya kampuni kwa kupakia APK au App Bundle kwenye ukurasa wa kupakia programu ya kushiriki ndani ya kampuni na kutengeneza kiungo. Unaposhiriki programu yako kwa njia hii, unaweza kuruhusu ufikiaji kupitia orodha za barua pepe pekee au kumruhusu mtu yeyote unayeshiriki kiungo naye apakue programu.

Kabla ya kuanza

Kabla ya kupakia faili kwa ajili ya kushiriki programu ndani ya kampuni, yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu unayohitaji kufahamu:

  • Ikiwa una ruhusa ya Kusambaza programu kwenye vikundi vya majaribio, una idhini ya kupakia APK na App Bundle za kushiriki programu ndani ya kampuni kwa chaguomsingi.
  • Si lazima misimbo ya toleo iwe mipya au ya kipekee na unaweza kutumia tena misimbo ya toleo kwa ajili ya App Bundle au APK ambazo unashiriki.
  • Unaweza kupakia na kushiriki APK au App Bundle zinazoweza kutatuliwa.
  • Vizalia vya programu vilivyopakiwa kwa ajili ya kushiriki programu ndani ya kampuni havionyeshwi kwenye kichunguzi cha App Bundle yako wala haviwezi kujumuishwa kwenye matoleo ya vikundi vya majaribio au toleo la umma.
  • Vizalia vya programu vilivyopakiwa kwa ajili ya programu ya kushiriki ndani ya kampuni vinaweza kuambatishwa cheti kwa kutumia ufunguo wowote na havihitaji kuambatishwa cheti kwa kutumia ufunguo wa kupakia au wa toleo la umma. Zinatiwa sahihi kiotomatiki na ufunguo wa Kushiriki Programu Ndani ya Kampuni, ambao unatengenezwa kiotomatiki na Google kwa ajili ya programu yako.
  • Unaweza kushiriki kiungo cha kushiriki programu ndani ya kampuni na watumiaji wengi utakavyo, lakini idadi ya juu ya watumiaji watakaoweza kupakua programu yako kwa kutumia kiungo ni 100.
  • Muda wa kutumia viungo vya kupakua huisha siku 60 baada ya tarehe ya kupakiwa.

Pakia na ushiriki programu

Pakia na ushiriki programu kwa ajili ya majaribio
  1. Baada ya kuingia kwenye Akaunti ya Google ambayo imeongezwa kama mpakiaji aliyeidhinishwa, tembelea ukurasa wa kupakia programu ya kushiriki ndani ya kampuni.
  2. Chagua Pakia.
  3. Andika jina la toleo ili likusaidie wewe na wanaojaribu programu yako kutambua programu yako au tumia jina la toleo lililotengwa kwenye APK au App Bundle yako.
  4. Chagua Thibitisha upakiaji.
  5. Karibu na APK au App Bundle uliyopakia, bofya aikoni ya kunakili ili unakili URL ya programu kwenye ubao wako wa kunakili.
  6. Shiriki kiungo cha kupakua na watumiaji wako wanaojaribu.

Ongeza wanaopakia na wanaojaribu walioidhinishwa

Ongeza wanaopakia walioidhinishwa

Chaguo la 1: Unda orodha mpya ya wanaopakia walioidhinishwa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo Mipangilio Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Kwenye kichupo cha Wanaopakia na wanaojaribu, nenda kwenye sehemu ya "Dhibiti wanaopakia" kisha uchague Tunga orodha ya barua pepe.
  5. Andika jina ili utambulishe orodha yako ya wanaopakia.
    • Unaweza kutumia orodha hiyo kufanya majaribio ya baadaye kwenye programu zako zozote.
  6. Weka anwani za barua pepe zilizotenganishwa kwa koma au uchague Pakia faili ya CSV. Ikiwa unatumia faili ya CSV, weka kila anwani ya barua pepe kwenye mstari wake bila koma zozote.
    • Ukipakia faili ya CSV baada ya kuandika anwani za barua pepe, itabadilisha anwani zozote za barua pepe ulizoongeza.
    • Si lazima wanaopakia walioidhinishwa wawe watumiaji wa akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play.
  7. Chagua Hifadhi mabadiliko.
  8. Chagua kisanduku cha kuteua kilicho karibu na jina la orodha unayotaka kutumia.

Kumbuka: Ukitunga orodha ya anwani za barua pepe, unaweza kuitumia tena unapoongeza wanaopakia, wanaopakua na wanaojaribu walioidhinishwa kwa ajili ya vikundi vya majaribio kwenye akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play.

Chaguo 2: Tumia orodha iliyopo ya wanaopakia walioidhinishwa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Majaribio ya ndani ya kampuni > Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Kwenye kichupo cha Wanaopakia na wanaojaribu, nenda kwenye sehemu ya “Dhibiti wanaopakia” na uchague kisanduku cha kuteua kilicho karibu na jina la orodha unazotaka kutumia.
Ongeza wanaojaribu walioidhinishwa

Muhimu: Baada ya kuongeza wanaojaribu walioidhinishwa, wape maagizo kuhusu jinsi ya kuwasha hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni.

Chaguo 1: Ifanye programu yako ipatikane kwa yeyote aliye na kiungo

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Majaribio ya ndani ya kampuni > Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Kwenye kichupo cha Wanaopakia na wanaojaribu, nenda kwenye sehemu ya “Dhibiti wanaopakia” na uhakikishe kwamba chaguo la "Yeyote uliyeshiriki naye kiungo anaweza kupakua" limechaguliwa (linapaswa kuchaguliwa kwa chaguomsingi).

Chaguo la 2: Unda orodha mpya ya wanaojaribu walioidhinishwa

  1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo > Mipangilio > Kushiriki programu ndani ya kampuni > Orodha ya barua pepe.
  4. Chagua kichupo cha "Wanaojaribu walioidhinishwa".
  5. Chini ya "Upatikanaji wa kiungo," chagua Orodha za barua pepe.
  6. Bofya Unda orodha.
  7. Andika jina ili utambulishe orodha yako ya wanaojaribu. Unaweza kutumia orodha hiyo kufanya majaribio ya baadaye kwenye programu zako zozote.
  8. Ongeza anwani za barua pepe zilizotengwa kwa koma au ubofye Pakia faili mpya ya CSV. Ikiwa unatumia faili ya CSV, weka kila anwani ya barua pepe kwenye mstari wake bila koma zozote.
    • Kumbuka: Ukipakia faili ya CSV baada ya kuandika anwani za barua pepe, itabadilisha anwani zozote za barua pepe ulizoongeza
  9. Bofya Hifadhi.
  10. Chagua kisanduku cha kuteua kilicho karibu na jina la orodha unayotaka kutumia.

Kumbuka: Ukitunga orodha ya anwani za barua pepe, unaweza kuitumia tena unapoongeza wanaopakia, wanaopakua na wanaojaribu walioidhinishwa kwa ajili ya vikundi vya majaribio kwenye akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Majaribio ya ndani ya kampuni > Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Chagua kichupo cha Orodha za barua pepe.
  5. Karibu na “Wanaopakua,” chagua Tunga orodha ya barua pepe.
  6. Andika jina ili utambulishe orodha ya wanaopakua programu yako.
    • Unaweza kutumia orodha hiyo kufanya majaribio ya baadaye kwenye programu zako zozote.
  7. Weka anwani za barua pepe zilizotenganishwa kwa koma au uchague Pakia faili ya CSV. Ikiwa unatumia faili ya CSV, weka kila anwani ya barua pepe kwenye mstari wake bila koma zozote.
    • Ukipakia faili ya CSV baada ya kuandika anwani za barua pepe, itabadilisha anwani zozote za barua pepe ulizoongeza.
    • Si lazima wanaopakia walioidhinishwa wawe watumiaji wa akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play.
  8. Chagua Hifadhi mabadiliko.
  9. Chagua kisanduku cha kuteua kilicho karibu na jina la orodha unayotaka kutumia.

Kumbuka: Ukitunga orodha ya anwani za barua pepe, unaweza kuitumia tena unapoongeza wanaopakia, wanaopakua na wanaojaribu walioidhinishwa kwa ajili ya vikundi vya majaribio kwenye akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play.

Chaguo la 3: Tumia orodha iliyopo ya wanaojaribu walioidhinishwa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Majaribio ya ndani ya kampuni > Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Chagua kichupo cha Orodha za barua pepe.
  5. Karibu na “Wanaopakua,” chagua kisanduku cha kuteua kilicho karibu na jina la orodha unazotaka kutumia.

Jinsi wanaojaribu walioidhinishwa wanavyoweza kuwasha hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni

Kabla ya wanaojaribu walioidhinishwa kupakua programu kwa kutumia hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni, wanahitajika kuwasha hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni kwenye programu yao ya Duka la Google Play.

  1. Fungua programu ya Duka la Google Play Google Play.
  2. Gusa Menyu Menyu > Mipangilio.
  3. Kwenye sehemu ya "Kuhusu", gusa toleo la Duka la Google Play mara 7.
  4. Baada ya mipangilio ya Kushiriki programu ndani ya kampuni kutokea, gusa swichi ili uwashe hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni.
  5. Gusa Washa.

Pakua vyeti

Ili kutumia huduma zao, baadhi ya watoa huduma za API huomba cheti ili kukioanisha na jina la kifurushi cha programu. Baada ya kupakia APK au App Bundle kwenye ukurasa wa kupakia programu ya kushiriki ndani ya kampunikwa mara ya kwanza, Dashibodi ya Google Play hutengeneza cheti kinachotumika kila mara programu yako inapopakiwa. Kila APK huambatishwa upya cheti hiki cha majaribio, bila kujali cheti ulichotumia kuambatisha cheti kwenye programu yako.

Ili kupakua cheti chako cha jaribio:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Toleo> Majaribio ya ndani ya kampuni > Kushiriki programu ndani ya kampuni.
  4. Kwenye kichupo cha Wanaopakia na wanaojaribu, nenda kwenye sehemu ya "Cheti cha kujaribu programu ndani ya kampuni".
  5. Chagua Cheti cha kupakua.
    • Ikiwa unahitaji alama bainifu za cheti maalum, bofya aikoni ya kunakili karibu na aina ya cheti ili kukinakili kwenye ubao wako wa kunakili.

Kutatua matatizo

Ukipata matatizo unapotumia hali ya kushiriki programu ndani ya kampuni, zifuatazo ni mbinu chache za kuyatatua:

Mtumiaji hafanyii majaribio kipengele cha kushiriki programu ndani ya kampuni
Ikiwa watumiaji wako wanaojaribu wanapata matatizo kupakua programu yako ya ndani, hakikisha kuwa umewaongeza kuwa wanaojaribu walioidhinishwa au umeifanya programu yako ipatikane kwa kila mtu aliye na kiungo.
Programu haipatikani kwa wanaojaribu

Ikiwa programu haipatikani kwa mtumiaji kwenye Google Play, basi hawataweza kuipakua kwa kutumia jaribio la ndani la programu. Ili wanaojaribu waweze kupakua programu yako ya ndani, wanahitaji kuwa na uwezo wa kufikia ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Ifuatayo ni baadhi ya mifano inayoonyesha kwa nini programu ya ndani haitapatikana kwa mtumiaji kuipakua:

Idadi ya juu ya wanaojaribu wamepakua programu yako

Ukishiriki kiungo cha kushiriki programu ndani ya kampuni na watumiaji wengi, unaweza kufikia idadi ya juu ya watumiaji (100) wanaoweza kupakua programu yako kwa kutumia kiungo kimoja.

Ili ushiriki programu yako na watumiaji wengi kwa kutumia kiungo, pakia APK au App Bundle sawa na utapokea kiungo kipya cha kupakua. Watumiaji wasiozidi 100 wanaweza kupakua programu yako kupitia kila kiungo cha kipekee.

Muda wa kiungo cha kupakua umekwisha

Iwapo muda wa kutumia kiungo cha kupakua programu yako ya kushiriki ndani ya kampuni utakwisha, pakia APK au App Bundle sawa tena ili upokee kiungo kipya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3473926760429609500
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false