Fuatilia ubora wa kiufundi wa programu yako ukitumia Android vitals

Tumia Android vitals ili ikusaidie kuelewa na kuboresha jinsi programu yako inavyotumia betri, uthabiti na utekelezaji wa programu yako na zaidi.

Chagua jinsi ya kufikia data ya programu yako

Kuna njia mbili unazoweza kutumia kufikia Android vitals: kupitia Dashibodi ya Google Play na kupitia Google Play Developer Reporting API.

API hutoa ufikiaji wa michakato ya kiotomatiki ya programu kwenye Android vitals kwa wasanidi programu wanaotaka kujumuisha data ya Android vitals na vikundi vingine vya data au kuijumuisha kwenye utaratibu wao wa kazi. Ili upate maelezo zaidi kuhusu utumiaji wa API kufikia Android vitals, nenda kwenye ukurasa wa Google Play Developer Reporting API.

Ili upate na ukague data ya Android vitals ya programu yako katika Dashibodi ya Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Ubora > Android vitals > Muhtasari.
  4. Chagua fungu la data ambalo ungependa kuangalia ukitumia kiteuzi cha kipindi upande wa juu kulia.

Muhimu: Ikiwa hakuna data inayopatikana, programu yako haina pointi za data za kutosha katika vichujio vilivyobainishwa ili kutambua matatizo yoyote katika programu yako.

Fuatilia takwimu za msingi za programu yako

Upande wa juu kwenye ukurasa wa Muhtasari, unaweza kuona takwimu za msingi za programu yako. Hivi ndivyo vipimo muhimu zaidi vya kiufundi na vinaathiri uwezo wa kutambulika wa programu yako kwenye Google Play. Takwimu za msingi zinajumuisha:

Google Play hubainisha upeo wa utendaji duni kwa vipimo hivi. Programu yako ikizidisha upeo huu, huenda isiweze kutambulika kwa urahisi kwenye Google Play. Wakati mwingine, huenda ukaonyeshwa onyo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ili kuweka matarajio ya watumiaji.

Unaweza kutumia sehemu ya "Hitilafu kuu" ili kutambua haraka maboresho ambayo programu yako inahitaji. Kuna aina mbili za hitilafu kuu:

  • Utendaji duni: Vipimo ambavyo vimezidi upeo wa utendaji duni
  • Hitilafu: Data kubadilika sana (kwa mfano, ongezeko kubwa la idadi ya ANR inayotambuliwa na watumiaji)

Ili upate arifa za barua pepe, tembelea Mipangilio > Arifa au ubofye Dhibiti arifa kwenye sehemu ya "Takwimu za msingi" (Ubora > Android vitals > Muhtasari). Kumbuka kuwa, kwa sasa arifa zinapatikana tu kasoro inapotokea.

Kagua takwimu zote

Karibu na sehemu ya katikati ya ukurasa wa Muhtasari, unaweza kuangalia data ya takwimu zote kulingana na ubora.

Kwenye jedwali, unaweza kukagua vipimo vyako vya muda wa sasa na uliopita. Unaweza pia kulinganisha programu yako na programu zingine kwenye Google Play.

Kuangalia vipimo vya kina

Ili upate maelezo ya ziada kuhusu kipimo, bofya sehemu ya Angalia maelezo () iliyo karibu nacho. Kwenye skrini inayofuata, unaweza kukagua:

  • Upeo wa utendaji duni
  • Vigezo vya aina
  • Ulinganishaji wa kina na programu zingine
    • Karibu na sehemu ya juu ya ukurasa, kwenye kadi ya kulinganisha na programu zingine, chagua Badilisha kikundi cha programu zingine ili ubadilishe kikundi cha programu zilizochaguliwa na mtumiaji. Baada ya kuunda kikundi cha programu zilizochaguliwa na mtumiaji, unaweza kuona jinsi programu yako inavyolinganishwa na programu zingine ambazo umechagua kwenye Google Play.
  • Kipimo kinavyovuma kadri muda unavyosonga
Changanua data kwa ukubwa

Ili kukusaidia kupanga, kugawa na kuchanganua data yako, vipimo vyako huainishwa kulingana na vigezo tofauti. Vipimo vyote vimeainishwa ifuatavyo:

  • Vizalia vya programu: Toleo la programu yako linalokabiliwa na hitilafu
  • Toleo la Android (SDK): Toleo la Mfumo wa Uendeshaji wa Android linaloripotiwa na kifaa cha mtumiaji
  • Umbo: Aina ya kifaa kinachotumiwa kuendesha programu yako (kwa mfano, Simu, Kompyuta Kibao, TV, Kifaa cha Kuvaliwa)
  • Muundo wa kifaa: Ufafanuzi wa kiwango cha juu kuhusu kifaa, ikijumuisha chapa ya kipekee na kitambulishi cha kifaa, kwa mfano, "Google oriole." Muundo mmoja wa kifaa unaweza kuwa na vibadala vilivyo na matoleo tofauti ya Android, RAM, hifadhi au Mfumo kwenye Chip (SoC).
  • Nchi/eneo: Mahali kilipokuwa kifaa cha mtumiaji wakati wa kuripoti hitilafu

Kidokezo: Ili uone uainishaji kulingana na vigezo mahususi vya maunzi ya kifaa au programu ya kifaa (kwa mfano, muundo wa kifaa au toleo la Android), bofya alama () karibu na kipengee husika kwenye jedwali.

Baadhi ya vipimo vina vigezo vya uainishaji vya ziada:

  • Jina la ombi la kudhibiti kuwaka kwa kifaa: Lebo zilizowekwa kiotomatiki wakati wa kutumia API ya PowerManager katika programu yako
  • Jina la hatua ya skrini kuwaka: Lebo zilizowekwa kiotomatiki wakati wa kutumia API ya AlarmManager katika programu yako
  • Jina la shughuli ya ANR: Jina kamili la aina ya shughuli ambapo ANR ilitokea (ikiwa lipo)
  • Aina ya ANR: Wakati ANR ilitokea (kwa mfano, wakati wa kutekeleza huduma ikiwa) (ikiwa ipo)

Unaweza kuangalia maelezo zaidi yanapopatikana (kwa mfano matukio ya kuacha kufanya kazi au vikundi vya ANR vinavyohusiana na uainishaji huo) kwa kubofya Angalia maelezo () iliyo karibu na kipengee husika.

Kidokezo: Unaweza kubadilisha ili uone vipimo mbalimbali vilivyo katika kategoria moja kwa kutumia kipengele cha kugeuza kilicho upande wa juu wa skrini, kisha uchuje ukurasa.

Vipimo na aina za data

Data ya Android vitals inapatikana kwa siku 90 zilizotangulia kwenye Dashibodi ya Google Play na kwa miaka mitatu kwenye Google Play Developer Reporting API.

Data hukusanywa kutoka kwa watumiaji ambao walijijumuisha kushiriki kiotomatiki data ya matumizi na uchunguzi kutoka kwenye kikundi kidogo cha vifaa vya Android na matoleo ya mfumo wa uendeshaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi watumiaji wa Android wanajijumuisha kushiriki data, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi wa Akaunti.

Android vitals husasishwa kila siku. Wakati mwingine data ya vifaa vya Android 10 au matoleo mapya zaidi huenda ikasasishwa kabla ya data ya vifaa vilivyo chini ya Android 10. Hili likitokea, utaona tu data ya Android 10 na matoleo mapya zaidi siku ambazo ni toleo hili tu linapatikana.

Kumbuka: Vipimo vya Android vitals havijumuishi matatizo ya kiufundi yanayotokea kwenye miundo ya vifaa ambayo haijathibitishwa au kwenye matoleo ya programu yako ambayo hayakusakinishwa kupitia Google Play.

Kunja Zote Panua Zote

Uthabiti

Vipimo vya idadi ya ANR

Vipimo vya idadi ya ANR vinaonyesha muhtasari wa ubora wa programu yako. Vipimo hivi huhesabiwa kwa kuzingatia idadi ya watumiaji wenye ANR ulio nao kisha kulinganisha idadi hiyo na matumizi ya programu yako. Huripotiwa kama asilimia ya watu wanaotumia programu kila siku, ambapo mtumiaji wa kila siku ni yule anayetumia programu yako kwa siku moja kwenye kifaa kimoja. Mtumiaji akitumia programu yako kwenye zaidi ya kifaa kimoja kwa siku moja, kila kifaa kitachangia idadi ya watumiaji wa programu kwa siku hiyo. Watumiaji kadhaa wakitumia kifaa kile kile kwa siku moja, itahesabiwa kama mtumiaji mmoja pekee.

Kuna vipimo vitatu vya idadi ya ANR:

  • Idadi ya ANR inayotambuliwa na mtumiaji: Asilimia ya watumiaji wa programu yako wa kila siku waliokumbana na angalau tukio moja la ANR lililotambuliwa na mtumiaji. Tukio la ANR lililotambuliwa na mtumiaji ni ANR yenye uwezekano mkubwa kuwa ilitambuliwa na mtumiaji. Kwa sasa, ni matukio ya ANR yenye alama ya 'input dispatching timed out' pekee yanahesabiwa. Kila wakati, kpimo hiki kitakuwa chini ya jumla ya idadi yako ya ANR kwa sababu kinasawazishwa na matumizi ya kila siku, lakini hakijumuishi ANR zote.
    Idadi ya ANR iliyotambuliwa na mtumiaji ni takwimu ya msingi, kumaanisha kuwa inaathiri uwezo wa programu yako kutambulika kwenye Google Play. Ni muhimu kwa sababu ANR inazokokota hutokea kila wakati mtumiaji anapotumia programu na hivyo kusababisha usumbufu mwingi.
  • Idadi ya ANR: Asilimia ya watu wanaotumia programu yako kila siku waliotatizika angalau mara moja kutokana na hitilafu ya ANR. Kipimo hiki kinajumuisha ANR ambazo hazijaainishwa kuwa hazijaripotiwa na watumiaji, lakini hatuwezi kutoa hakikisho kuwa ANR hizi haziwaathiri watumiaji.
  • Kiwango cha matukio ya ANR: Asilimia ya watumiaji wako wa kila siku ambao waliathiriwa na ANR angalau mara mbili. Kipimo hiki husaidia kuonyesha hitilafu zinazojirudia.

Kurekebisha tatizo

ANR zinazochangia idadi zako za ANR huripotiwa kwenye ukurasa wa ANR na Matukio ya Kuacha Kufanya Kazi. Kwenye ukurasa huu, unaweza kuchuja matukio ya ANR yanayotambuliwa na watumiaji.

Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android inatoa mwongozo wa jinsi ya kuchunguza na kurekebisha hitilafu za ANR.

Vipimo vya idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi

Vipimo vya idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi vinaonyesha muhtasari wa ubora wa programu yako. Vipimo hivi huhesabiwa kwa kuzingatia idadi ya watumiaji waliokabiliwa na hitilafu ya programu kuacha kufanya kazi kisha kulinganisha idadi hiyo na matumizi ya programu yako. Huripotiwa kama asilimia ya watumiaji wa kila siku, ambapo mtumiaji wa kila siku ni yule anayetumia programu yako kwa siku moja kwenye kifaa kimoja. Ikiwa mtumiaji ana zaidi ya kifaa kimoja, mtumiaji huyo atahesabiwa zaidi ya mara moja. Kwa mfano, watumiaji wawili wakitumia programu kwa siku mbili kila mmoja kwenye kifaa chake, idadi ya matumizi ya programu ya kila siku itakuwa nne.

Kuna vipimo vitatu vya idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi:

  • Idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi iliyotambuliwa na mtumiaji: Asilimia ya watu wanaotumia programu yako kila siku waliotatizika angalau mara moja kutokana na tukio la programu kuacha kufanya kazi lililotambuliwa na mtumiaji. Tukio la programu kuacha kufanya kazi ni tukio ambalo linaweza kuwa limetambuliwa na mtumiaji. Kwa mfano, hitilafu za kuacha kufanya kazi zinazotokea wakati programu yako inaonyesha shughuli au ikiwa inatekeleza huduma inayoonekana kwenye skrini. Kipimo hiki kitakuwa chini kila wakati kuliko idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi, kwa sababu kinasawazishwa na matumizi ya kila siku, lakini hakijumuishi hitilafu zote za kuacha kufanya kazi.
    Idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi inayotambuliwa na mtumiaji ni takwimu ya msingi, kumaanisha kuwa inaathiri upatikanaji wa programu yako kwenye Google Play. Ni muhimu kwa sababu matukio ya kuacha kufanya kazi yanayohesabiwa hutokea kila wakati mtumiaji anatumia programu na hukatiza matumizi. Hii ndiyo sababu unapaswa kuhakikisha kwamba programu yako haizidi upeo wa utendaji duni kwa kipimo hiki.
  • Idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi: Asilimia ya watu wanaotumia programu yako kila siku waliotatizika angalau mara moja kutokana na hitilafu ya programu kuacha kufanya kazi. Kipimo hiki kinajumuisha hitilafu za kuacha kufanya kazi ambazo haziainishwi kama zinazotambulika na mtumiaji, lakini hatuwezi kutoa hakikisho kuwa hitilafu hizi haziwaathiri watumiaji.

  • Kiwango cha matukio ya programu kuacha kufanya kazi: Asilimia ya watu wanaotumia programu yako kila siku waliotatizika angalau mara mbili kutokana na hitilafu ya programu kuacha kufanya kazi. Kipimo hiki husaidia kuonyesha hitilafu zinazojirudia.

Kurekebisha tatizo

Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android inatoa mwongozo kuhusu kuchunguza na kurekebisha hitilafu za programu kuacha kufanya kazi.

Muda wa kuanza na kupakia

Muda wa kuanza (muda hadi onyesho la kwanza)

Kwenye ukurasa wa Muda wa kuanza kupakia programu, unaweza kuona maelezo kuhusu wakati ambapo programu yako inaanza kupakia polepole kuanzia hali za mfumo za programu kupakia polepole kuanzia mwanzo, programu kupakia polepole wakati programu zingine zinapakia na programu kupakia polepole wakati programu zingine zimepakia. Muda wa kuanza kupakia hupima muda unaotumiwa na mtumiaji kuwasha programu yako, hadi wakati fremu za kwanza zitaonekana kwenye skrini. Mchakato huu pia unajulikana kama 'muda wa hadi onyesho la kwanza'.

Huenda programu yako isiwe tayari kwa mtumiaji kuanza kuitumia baada ya muda huu, kwa mfano, ikiwa programu yako ina skrini za ziada za kupakia.

Maelezo ya kukusanya data

  • Muda wa kupakia programu unarekodiwa tu wakati mtumiaji anaanzisha shughuli.
    • Kwa mfano: Kwa programu za kibodi, muda wa kupakia programu ni sawa na muda wa kupakia programu inayotumika kudhibiti Jam.
  • Ikiwa programu inapakia mara nyingi siku ile ile kwenye hali sawa ya mfumo, muda wa juu zaidi wa kupakia programu wa siku hiyo utarekodiwa.
  • Muda wa kupakia programu hufuatiliwa wakati fremu ya kwanza ya programu inapomaliza kupakia, hata kama si skrini ambayo mtumiaji anatumia.
    • Kwa mfano: Ikiwa programu inaanza na skrini ya utangulizi, muda wa kupakia utakuwa sawa na muda unaohitajika kuonyesha skrini ya utangulizi.

Maelezo muhimu

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi ambapo watumiaji waliathiriwa na tukio la programu kupakia polepole katika kila hali ya mfumo:
    • Programu kupakia polepole unapoifungua mara ya kwanza: Sekunde 5 au zaidi
    • Programu kufunguka polepole ikiwa tayari imepakiwa: Sekunde 2 au zaidi
    • Programu kufunguka polepole ikiwa tayari inatumika chinichini: Sekunde 1 au zaidi
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia 90/99: Asilimia 10/1 ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na tukio la programu yako kupakia polepole.

Kurekebisha tatizo

Iwapo programu yako ina idadi nyingi ya matukio ya programu kupakia polepole, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate suluhu zinazopendekezwa.

Utekelezaji

Utekelezaji wote

Kipimo cha kipindi cha kasi ya chini (FPS 30 au FPS 20) [michezo pekee]

Umuhimu wake

Kwa kutumia kipimo cha vipindi vyenye kasi ya chini unaweza kuelewa utendaji wa kasi ya picha ya mchezo wako, suala linaloathiri uwezo wa mchezo wako kuchezwa na watumiaji bila kukwama.

Kuelewa data ya programu yako

Kwenye ukurasa wa Vipindi vya kasi ya chini, utaona maelezo kuhusu asilimia ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na zaidi ya asilimia 25 ya fremu zinazotekelezwa kwa kasi ya chini kuliko kasi ya FPS 30 au FPS 20, kulingana na kasi ya msingi unayochagua. Unaweza pia kuona usambazaji wa vipindi kulingana na kasi ya picha ya mchezo wako. (Kasi ya picha ya kiwango cha kipindi hupimwa katika kiwango cha asilimia 75, kumaanisha kwamba asilimia 75 ya fremu zinafikia angalau kwa kasi hii ya picha.)

Michezo mingi kwenye Google Play inapaswa kulenga kasi ya FPS 30 au zaidi. Hii inawapa watumiaji hali nzuri ya utumiaji, bila kujali aina ya mchezo wanaocheza (ingawa watumiaji wengine watapendelea angalau kasi ya FPS 60, hasa kwenye vifaa vya bei zaidi). Fuatilia kipimo cha kipindi cha kasi ya chini (FPS 30) ili uhakikishe unafikia kiwango hiki. Kumbuka kwamba kipimo hiki kinajumuisha tu vipindi ambavyo zaidi ya asilimia 25 ya fremu hazina FPS 30, kwa hivyo zinaweka fursa ya kubadilishwa kwa kasi ya picha.

Ingawa kasi ya FPS 30 inatoa hali nzuri ya utumiaji, huenda kukawa na nyakati au aina za michezo ambayo ni sawa kupunguza kasi ya picha iwe chini ya kiwango hiki au watumiaji wanaweza kutaka kucheza mchezo wako kwenye simu ambazo haziwezi kutumia kasi ya FPS 30. Katika hali hizi, angalau asilimia 75 ya fremu katika kipindi bado zinapaswa kuonyeshwa kwa kasi ya FPS 20 au zaidi. Fuatilia kipimo cha kipindi cha kasi ya chini (FPS 20) ili uhakikishe unafikia kiwango hiki.

Android vitals huripoti vipindi vya kasi ya chini (FPS 30) na vipindi vya kasi ya chini (FPS 20) vya kila kifaa pamoja na kwenye vipindi na vifaa vyote. Tumia kipimo cha jumla ili uelewe hali yako ya jumla ya utumiaji, lakini zingatia pia utendaji wa kila kifaa. Wakati ukifika, Google Play itaanza kuwaelekeza watumiaji kuepuka michezo ambayo haiwezi kuonyeshwa kwa kasi ya FPS 20 kwenye simu zao.

Android Vitals huanza tu kufuatilia kasi ya picha baada ya mchezo wako kutekelezwa kwa dakika 1.

Maelezo ya kukusanya data

Kipimo cha vipindi vya kasi ya chini huhesabiwa na data iliyokusanywa katika SurfaceFlinger. Kwa maelezo ya kina zaidi, kasi ya picha ya kipindi mahususi inakadiriwa kulingana na muda unaotumika kati ya fremu zinazoonyeshwa kwenye mifumo inayomilikiwa na programu na inajumuisha fremu zinazotekelezwa na OpenGL, Vulkan, pamoja na Zana za kiolesura cha Android. Kipimo hiki kwa sasa kinapatikana tu kwa michezo.

Data ya kasi ya picha ya Vipindi vya kasi ya chini hukusanywa kwa vifaa vinavyotumia toleo la Android 9 au jipya zaidi.

Skrini ya dashibodi

  • Kasi wakilishi ya picha: Utendaji wa kasi ya picha ya mchezo wako kwenye vifaa vinavyotumia toleo la Android 9 au jipya zaidi, ilihesabiwa katika kiwango cha asilimia 75. Hii inamaanisha asilimia 75 ya vipindi vilikuwa na kasi hii ya picha au ya juu zaidi kwa asilimia 75 ya wakati.
  • Kiwango cha vipindi vyenye kasi ya chini baada ya muda: Ni kipindi cha wakati kinachoonyesha asilimia ya vipindi vilivyobainishwa kuwa Vipindi vyenye kasi ya chini.
  • Mgawanyo wa kasi ya picha: Ni histogramu inayoonyesha asilimia 75 ya matokeo ya kasi ya picha kwenye vipindi mbalimbali. Hii inamaanisha asilimia 75 ya fremu katika kipindi zilikuwa na kasi inayozidi kasi ya picha iliyotumika kwenye kipindi hicho cha muda.

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina idadi kubwa ya Vipindi vya kasi ya chini, nenda kwenye tovuti ya wasanidi programu wa Android upate suluhu zinazopendekezwa.

Utekelezaji wa zana za kiolesura cha Android

Fremu nyingi mno za kasi ya chini [programu pekee]

Kuelewa data ya programu yako

Kwenye ukurasa wa Fremu za kasi ya chini zilizokithiri, utaona maelezo kuhusu asilimia ya matumizi ya programu ya kila siku ambapo watumiaji walikumbana na zaidi ya asilimia 50 ya fremu ambazo hazikutimiza makataa ya kuonyesha picha kwenye kifaa. Shughuli za watumiaji kwenye programu yako zinatakiwa kutekelezwa kwa kasi ya picha kwa sekunde ya FPS 60 bila fremu zilizocheleweshwa au ambazo hazijajumuishwa.

Maelezo ya kukusanya data

Google hukusanya muda wa utekelezaji wa kila fremu iliyotekelezwa na programu yako unapotumia fremu ya Zana za Kiolesura. Fremu zinazotekelezwa kwa kutumia OpenGL au Vulkan moja kwa moja hazikusanywi.

Skrini ya dashibodi

Unapochagua safu mlalo, utaona data imechanganuliwa katika asilimia.

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na zaidi ya asilimia 50 ya fremu ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16. Kipindi cha kila siku kinarejelea siku ambayo programu yako ilitumika. Kwa mfano, ikiwa watumiaji wawili watatumia programu kwa siku mbili, itaonyesha vipindi vinne vya kila siku.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99 : Asilimia 90/99 ya fremu zote ilikuwa na muda wa utekelezaji usiozidi idadi iliyoonyeshwa. Idadi hii inalingana na fremu zote zilizokusanywa.

Unapobofya maelezo katika jedwali, utaona chati ya "Usambazaji wa muda wa utekelezaji wa kiolesura". Unapokagua chati, utataka kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya fremu za programu yako zinatekelezwa kwa milisekunde 16 au chini yake.

Data iliyo chini ya chati inaonyesha utendaji wa muda wa utekelezaji wa programu na inaweza kukusaidia kupata chanzo cha tatizo lolote kuhusu muda wa utekelezaji. Kwa mfano, ikiwa asilimia ya 'muda wa juu wa kusubiri majibu baada ya kuingiza data' iko juu, huenda utahitaji kuangalia msimbo wa programu yako ambao unashughulikia uingizaji wa data inayowekwa na mtumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu vipimo hivi, nenda kwenye makala ya kujaribu utendaji wa kiolesura.

  • Vsync ambazo hazikutekelezwa: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya matukio ya Vsync ambayo hayakutekelezwa ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Muda mrefu wa kusubiri majibu baada ya kuingiza data: Kwa fremu zote ambazo muda wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya matukio ya kuingiza data iliyochukua zaidi ya milisekunde 24 ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Mchakato wa kiolesura unaotekelezwa polepole: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya mara ambazo mchakato wa kiolesura ulichukua zaidi ya milisekunde 8 kukamilika ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Amri za kuonyesha zinazotekelezwa polepole: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, mara ambazo utumaji wa amri za kuonyesha kwenye GPU ulichukua zaidi ya milisekunde 12 ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Upakiaji wa polepole wa taswidoti: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya mara ambazo taswidoti ilichukua zaidi ya milisekunde 3.2 kupakia kwenye GPU ikigawanywa na idadi ya fremu.

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina idadi ya juu ya fremu zenye muda wa utekelezaji unaozidi milisekunde 16, nenda kwenye tovuti ya wasanidi programu wa Android upate suluhu zinazopendekezwa.

Fremu zilizochelewa mno kutekelezwa [programu pekee]

Kuelewa data ya programu yako

Kwenye ukurasa wa Fremu za kasi ya chini zilizokithiri, utaona maelezo kuhusu asilimia ya matumizi ya programu ya kila siku ambapo watumiaji walikumbana na zaidi ya asilimia 50 ya fremu ambazo hazikutimiza makataa ya kuonyesha picha kwenye kifaa. Shughuli za watumiaji kwenye programu yako zinatakiwa kutekelezwa kwa kasi ya picha kwa sekunde ya FPS 60 bila fremu zilizocheleweshwa au ambazo hazijajumuishwa.

Maelezo ya kukusanya data

Google hukusanya muda wa utekelezaji wa kila fremu iliyotekelezwa na programu yako unapotumia fremu ya Zana za Kiolesura. Fremu zinazotekelezwa kwa kutumia OpenGL au Vulkan moja kwa moja hazikusanywi.

Skrini ya dashibodi

Unapochagua safu mlalo, utaona data imechanganuliwa katika asilimia.

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na zaidi ya asilimia 50 ya fremu ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16. Kipindi cha kila siku kinarejelea siku ambayo programu yako ilitumika. Kwa mfano, ikiwa watumiaji wawili watatumia programu kwa siku mbili, itaonyesha vipindi vinne vya kila siku.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99 : Asilimia 90/99 ya fremu zote ilikuwa na muda wa utekelezaji usiozidi idadi iliyoonyeshwa. Idadi hii inalingana na fremu zote zilizokusanywa.

Unapobofya maelezo katika jedwali, utaona chati ya "Usambazaji wa muda wa utekelezaji wa kiolesura". Unapokagua chati, utataka kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya fremu za programu yako zinatekelezwa kwa milisekunde 16 au chini yake.

Data iliyo chini ya chati inaonyesha utendaji wa muda wa utekelezaji wa programu na inaweza kukusaidia kupata chanzo cha tatizo lolote kuhusu muda wa utekelezaji. Kwa mfano, ikiwa asilimia ya 'muda wa juu wa kusubiri majibu baada ya kuingiza data' iko juu, huenda utahitaji kuangalia msimbo wa programu yako ambao unashughulikia uingizaji wa data inayowekwa na mtumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu vipimo hivi, nenda kwenye makala ya kujaribu utendaji wa kiolesura.

  • Vsync ambazo hazikutekelezwa: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya matukio ya Vsync ambayo hayakutekelezwa ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Muda mrefu wa kusubiri majibu baada ya kuingiza data: Kwa fremu zote ambazo muda wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya matukio ya kuingiza data iliyochukua zaidi ya milisekunde 24 ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Mchakato wa kiolesura unaotekelezwa polepole: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya mara ambazo mchakato wa kiolesura ulichukua zaidi ya milisekunde 8 kukamilika ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Amri za kuonyesha zinazotekelezwa polepole: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, mara ambazo utumaji wa amri za kuonyesha kwenye GPU ulichukua zaidi ya milisekunde 12 ikigawanywa na idadi ya fremu.
  • Upakiaji wa polepole wa taswidoti: Kwa fremu zote ambazo muda wake wa kutekelezwa unazidi milisekunde 16, idadi ya mara ambazo taswidoti ilichukua zaidi ya milisekunde 3.2 kupakia kwenye GPU ikigawanywa na idadi ya fremu.

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina idadi ya juu ya fremu zenye muda wa utekelezaji unaozidi milisekunde 16, nenda kwenye tovuti ya wasanidi programu wa Android upate suluhu zinazopendekezwa.

Matumizi ya betri

Maombi marefu na yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa (chinichini)

Kurasa za maombi marefu na yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa na maombi marefu na yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa (chinichini) zinaonyesha matukio ya maombi yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa yaliyofanyika kwenye programu yako kupitia aina ya PowerManager. Maombi yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa huhakikisha kuwa CPU inatumika lakini mwangaza wa skrini na kibodi unaruhusiwa kuzima.

Maelezo ya kukusanya data

  • Kwa sababu za faragha, lebo za utambulishaji wa kudhibiti kuwaka kwa kifaa ambazo hazijakamilika hazitambulishwi.
  • Data kuhusu maombi yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa hukusanywa wakati kifaa hakichaji na skrini imezimwa.
  • Maombi marefu na yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa (chinichini) hukusanywa tu wakati programu inatumika chinichini.
  • Google hukokotoa muda wa juu wa maombi yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa kwa kila kipindi cha betri ili kuonyesha idadi ya vipindi vilivyoathiriwa na ombi la kudhibiti kuwaka kwa kifaa, lililodumu muda mrefu. Kwa mfano, ikiwa mtumiaji atatuma ombi la kudhibiti kuwaka kwa kifaa litakalodumu saa mbili, muda wa juu wa kudhibiti kuwaka kwa kifaa ambao Google itatumia utakuwa saa moja.
  • Kwa programu ambazo zinaweka sharedUserId katika faili ya maelezo: Utaona tu data ikiwa programu moja pekee ambayo ina sharedUserId sawa imesakinishwa.

Maelezo muhimu

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya matumizi ya chaji kabla ya kujazwa tena ambapo watumiaji waliathiriwa na angalau tukio moja la kudhibiti kuwaka kwa kifaa kwa zaidi ya saa moja.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99 : Asilimia 10/1 ya matumizi ya programu ya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na muda wa kudhibiti kuwaka kwa kifaa ambao haujakamilika uliozidi idadi iliyoonyeshwa.
  • Upeo wa utendaji duni: Iwapo programu yako inaonyesha kiwango cha matukio kilicho sawa na au zaidi ya upeo ulioonyeshwa, programu iko katika asilimia ya 25 ya chini ya programu maarufu 1,000 kwenye Google Play (kulingana na mara ambazo imesakinishwa).

Kurekebisha tatizo

Iwapo programu yako ina maombi mengi, marefu na yasiyo kamili ya kudhibiti kuwaka kwa kifaa, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate suluhu zinazopendekezwa.

Skrini kuwaka mara nyingi mno

Ukurasa wa Matukio mengi mno ya skrini kuwaka huonyesha matukio ya skrini kuwaka katika Kidhibiti cha Kengele yanayosababishwa na programu yako. Utaona data ya matukio ya skrini kuwaka ya aina za ELAPSED_REALTIME_WAKEUP au RTC_WAKEUP.

Maelezo ya kukusanya data

  • Kwa sababu za faragha, lebo za utambulishaji wa skrini kuwaka zimewekwa kwa namna isiyoweza kumtambulisha mtumiaji.
  • Matukio ya skrini kuwaka hukusanywa wakati kifaa hakichaji.
  • Ili kuonyesha kipimo cha kawaida, idadi ya mara za skrini kuwaka hulinganishwa na muda ambao kifaa kinatumia chaji ya betri. Google huhesabu idadi ya mara za skrini kuwaka kwa kila mtumiaji kwa kila saa ili kuonyesha ni watumiaji wangapi wameathiriwa na idadi ya juu ya matukio ya skrini kuwaka.
  • Kwa programu ambazo zinaweka sharedUserId katika faili ya maelezo: Utaona tu data ikiwa programu moja pekee ambayo ina sharedUserId sawa imesakinishwa.

Maelezo muhimu

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya matumizi ya chaji kabla ya kujazwa tena ambapo watumiaji waliathiriwa na zaidi ya matukio 10 ya skrini kuwaka kwa kila saa. Kipindi cha matumizi ya chaji kabla ya kujazwa tena ni ujumlisho wa ripoti zote za matumizi ya betri zilizopokelewa katika kipindi mahususi cha saa 24. Kwenye Android 10, ripoti ya matumizi ya betri inamaanisha muda kati ya matukio mawili ya kuchaji betri ikiwa chini ya asilimia 20 hadi zaidi ya asilimia 80 au kuanzia kiwango chochote hadi asilimia 100. Kwenye Android 11 na matoleo mapya zaidi, ripoti ya matumizi ya betri inamaanisha kipindi mahususi cha saa 24. Google hukusanya tu data hii wakati ambapo kifaa hakichaji.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99 : Asilimia 10/1 ya matumizi ya programu ya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na matukio ya skrini kuwaka kwa kila saa yanayozidi idadi iliyoonyeshwa.
  • Upeo wa utendaji duni: Iwapo programu yako inaonyesha kiwango cha matukio kilicho sawa na au zaidi ya upeo ulioonyeshwa, programu iko katika asilimia ya 25 ya chini ya programu maarufu 1,000 kwenye Google Play (kulingana na mara ambazo imesakinishwa).

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina matukio ya skrini kuwaka mara kwa mara, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate hatua zinazopendekezwa.

Matukio mengi mno ya utafutaji wa Wi-Fi (chinichini)

Ukurasa wa Matukio mengi mno ya utafutaji wa Wi-Fi (chinichini) huonyesha matukio ya utafutaji wa Wi-Fi yanayotokana na matumizi ya juu ya betri.

Maelezo ya kukusanya data

Data kuhusu matukio ya utafutaji wa Wi-Fi hukusanywa wakati kifaa hakichaji na programu inatumika chinichini.

Maelezo muhimu

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya matumizi ya chaji kabla ya kujazwa tena ambapo watumiaji walitafuta Wi-Fi zaidi ya mara 4 kwa kila saa.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99: Asilimia 10/1 ya matumizi ya programu ya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na matukio mengi ya utafutaji wa Wi-Fi chinichini uliozidi idadi iliyoonyeshwa.

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina idadi ya juu ya utafutaji wa Wi-Fi chinichini, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate suluhisho zinazopendekezwa.

Matukio mengi mno ya matumizi ya mtandao (chinichini)

Ukurasa wa Matukio mengi mno ya utumiaji wa mtandao huonyesha wakati idadi kubwa ya data ya mtandao inahusishwa na huduma ya chinichini. Wakati matumizi ya mtandao wako wa simu yanatendeka chinichini, watumiaji wako hawawezi kufikia vidhibiti ili kukomesha uhamishaji wa data kwa urahisi.

Maelezo ya kukusanya data

Data kuhusu matumizi ya mtandao wa simu hukusanywa wakati kifaa hakichaji na programu inatumika chinichini.

Maelezo muhimu

  • Vipindi vilivyoathiriwa: Asilimia ya vipindi vya matumizi ya chaji kabla ya kujazwa tena ambapo watumiaji waliathiriwa na matumizi ya mtandao kwa zaidi ya MB 50 chinichini kwa siku.
  • Idadi ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.
  • Asilimia ya 90/99: Asilimia 10/1 ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji waliathiriwa na matukio mengi mno ya utumiaji wa mtandao chinichini kuzidi idadi inayoonyeshwa.

Kurekebisha tatizo

Kama programu yako ina matukio ya juu ya matumizi ya mtandao wa simu chinichini, nenda kwenye Tovuti ya wasanidi programu wa Android ili upate suluhisho zinazopendekezwa.

Ruhusa

Kukataliwa kwa ruhusa

Kwenye ukurasa wa Kukataliwa kwa ruhusa, unaweza kuona asilimia ya vipindi vya ruhusa vya kila siku ambapo watumiaji walikataa ruhusa. Ruhusa ya kipindi cha kila siku inarejelea siku ambayo programu yako iliomba angalau ruhusa moja kutoka kwa mtumiaji.

Maelezo ya kukusanya data

Data kuhusu kukataa kutoa ruhusa hukusanywa wakati watumiaji wanajibu maombi ya ruhusa katika programu yako.

Maelezo muhimu

  • Kukataliwa kwa ruhusa: Asilimia ya ruhusa ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji walikataa kutoa ruhusa.
  • Usiulize tena: Asilimia ya ruhusa ya vipindi vya kila siku ambapo watumiaji walikataa kutoa ruhusa kwa kuteua chaguo la 'Usiulize tena'.
  • Jumla ya vipindi: Kadirio la idadi ya vipindi vilivyorekodiwa.

Kurekebisha tatizo

Ikiwa programu yako ina matukio mengi ya kukataliwa kwa ruhusa, nenda kwenye Tovuti ya Wasanidi programu wa Android ili upate suluhisho zinazopendekezwa.

Upeo wa utendaji duni kwa takwimu za msingi

Google Play imebainisha upeo wa utendaji duni wa takwimu za msingi za programu yako.

Programu yako ikizidisha upeo wa utendaji duni, huenda isipatikane kwa urahisi kwenye Google Play. Iwapo utendaji wa programu yako ni duni kwenye miundo mahususi ya vifaa, Google Play itawaelekeza watumiaji wa vifaa hivyo kwingine kwenye programu zinazowafaa zaidi. Wakati mwingine, huenda ukaonyeshwa onyo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ili kuweka matarajio ya watumiaji na kuweka chaguo la kutumia njia mbadala zenye ubora wa juu wa kiufundi.

Kawaida, Google Play huangalia data ya siku 28 zilizopita wakati wa kutathmini ubora wa programu yako, lakini inaweza kuchukua hatua mapema hitilafu zikiongezeka.

Kunja Zote Panua Zote

Uthabiti

Upeo wa Idadi ya matukio ya ANR yanayotambuliwa na Mtumiaji

Google Play imebainisha viwango vya upeo wa utendaji duni kwenye idadi ya matukio ya ANR yaliyotambuliwa na mtumiaji:

  • Utendaji duni wa jumla: Angalau asilimia 0.47 ya watumiaji wanaotumia programu yako kila siku wanakabiliwa na tukio la ANR lililotambuliwa na mtumiaji kwenye miundo yote ya vifaa.

  • Utendaji duni kwenye kila kifaa: Angalau asilimia 8 ya watumiaji wanaotumia programu yako kila siku wanakabiliwa na tukio la ANR lililotambuliwa na mtumiaji kwenye muundo fulani wa vifaa.

Ili kupunguza idadi ya ANR ya programu yako, rekebisha hitilafu za ANR zinazoripotiwa kwenye ukurasa wa ANR na Matukio ya Kuacha Kufanya Kazi. Idadi ya watumiaji waliotatizika ikiwa juu, idadi ya ANR ya programu yako inaongezeka kutokana wingi wa hitilafu.

Iwapo vigezo mahususi vya maunzi ya kifaa au programu vinachangia idadi ya ANR ya programu yako, Android vitals itakuarifu. Unaweza pia kuangalia ulinganishaji kwenye ukurasa wa Muhtasari wa ufikiaji na vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Muhtasari).

Upeo wa idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi yaliyotambuliwa na mtumiaji

Google Play imebainisha viwango vya upeo wa utendaji duni kwenye idadi ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi yaliyotambuliwa na mtumiaji:

  • Utendaji duni wa jumla: Angalau asilimia 1.09 ya watumiaji wanaotumia programu yako kila siku wanakabiliwa na tukio la programu kuacha kufanya kazi lililotambuliwa na mtumiaji kwenye miundo yote ya vifaa.

  • Utendaji duni katika kila kifaa: Angalau asilimia 8 ya watumiaji wanaotumia programu yako kila siku wanakabiliwa na tukio la programu kuacha kufanya kazi lililotambuliwa na mtumiaji kwenye muundo mmoja wa vifaa.

Ili kupunguza idadi ya matukio ya programu yako kuacha kufanya kazi, rekebisha hitilafu zinazoripotiwa kwenye ukurasa wa ANR na Matukio ya Kuacha Kufanya Kazi . Idadi ya watumiaji waliotatizika ikiwa juu, idadi ya matukio ya programu yako kuacha kufanya kazi inaongezeka kutokana wingi wa hitilafu.

Iwapo vigezo mahususi vya maunzi ya kifaa au programu vinachangia idadi ya matukio ya programu yako kuacha kufanya kazi, Android vitals itakuarifu. Unaweza pia kuangalia ulinganishaji kwenye ukurasa wa Muhtasari wa ufikiaji na vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Muhtasari).

Maudhui yanayohusiana

Gundua mbinu bora za kutumia Android vitals ili uboreshe utendaji na uthabiti wa programu yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1968655421729937193
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false