Kagua matoleo ya programu ukitumia kichunguzi cha App Bundle


Kuanzia Agosti 2021, programu mpya zitatakiwa kuchapishwa kwa kutumia Android App Bundle kwenye Google Play. Programu mpya zenye ukubwa wa zaidi ya MB 200 zinaweza kutumia Play Asset Delivery au Utumaji wa Vipengele vya Google Play.

Kuanzia tarehe 30 Juni 2023, Google Play haitaruhusu tena masasisho ya programu ya televisheni kwa kutumia APK. Masasisho yote ya programu ya televisheni lazima yachapishwe kwa kutumia Android App Bundle (AAB).

Ili upate maelezo zaidi, soma makala ya Mustakabali wa Android App Bundles umewadia, kwenye Blogu ya Wasanidi Programu wa Android.

Android App Bundle ndio muundo wa uchapishaji unaotumika kwenye Google Play. Hatua ya kuchapisha kwa kutumia App Bundles husaidia kupunguza ukubwa wa programu yako, kurahisisha matoleo na kuwezesha vipengele vya usambazaji wa kina.

Kwa kutumia kichunguzi cha App Bundle kwenye Dashibodi ya Google Play, unaweza kudhibiti kwa urahisi App Bundle na matoleo yako katika sehemu moja. Unaweza pia kufikia metadata, vipakuliwa na maarifa muhimu kuhusu vitu ambavyo Google Play hubuni kwa ajili ya Asset Delivery.

Jinsi App Bundle hufanya kazi na manufaa yake

Google Play hutumia App Bundle kubuni na kutuma APK ambazo zimeboreshwa katika kila usanidi wa kifaa, hali inayotoa programu bora kwa watumiaji. Hii inamaanisha kuwa unahitaji tu kubuni, kuweka sahihi na kupakia App Bundle moja ili utumie APK zilizoboreshwa katika aina mbalimbali za usanidi wa vifaa. Baadaye, Google Play itadhibiti na kuwasilisha APK za usambazaji wa programu kwa niaba yako.

Vipengele na manufaa ya App Bundle
  • Kuchapisha programu ndogo, kuwezesha usakinishaji wa haraka na kutumia nafasi ndogo kwenye diski, hali ambayo inaweza kupunguza matukio ya kuondoa programu.
  • Kurahisisha udhibiti wa matoleo, kuondoa ugumu wa kuchapisha na kudhibiti APK nyingi.
  • Unaweza kutumia huduma ya Utumaji wa Vipengele vya Google Play kuweka sehemu kwenye programu yako na kujumuisha sehemu za vipengele. Unaweza kutuma sehemu za vipengele kupitia njia mbalimbali:
    • Kutuma wakati wa kusakinisha: Sehemu za vipengele hutumwa wakati wa kusakinisha. Unaweza kuchagua kufanya hili ili utumie fursa ya kubuni miundo haraka au kutuma sehemu wakati wa kusakinisha. Kisha unaweza kuziondoa baadaye ili kuzuia kutumia nafasi kubwa kwenye diski yako. 
    • Kutuma kwa masharti: Sehemu za vipengele hutumwa wakati wa kusakinisha kulingana na masharti kama vile nchi ya mtumiaji, vipengele vya kifaa na kiwango cha chini zaidi cha toleo la SDK.
    • Kutuma panapohitajika: Sakinisha na uondoe sehemu za vipengele kadri inavyohitajika, badala ya kuzituma kwa watumiaji wote katika siku zote ambazo programu yako inatumika.
    • Huduma za papo hapo: Sehemu za vipengele zinaweza kufunguka papo hapo ili kuwapa watumiaji huduma za papo hapo kupitia viungo na kitufe cha Jaribu Sasa kwenye ukurasa wa programu katika Google Play, ambao hauhitaji mtumiaji kusakinisha programu yako kwanza.
  • Unaweza kutumia Play Asset Delivery kutuma vifurushi vikubwa vya vipengee. Unaweza kuwekea mapendeleo utumaji wa vifurushi vya vipengele kwa njia mbalimbali:
    • Kutuma wakati wa kusakinisha: Vifurushi vya vipengee hutumwa pamoja na programu ya kusakinishwa ("mapema") na hupatikana kwenye programu wakati wa kuzindua.
    • Kutuma haraka punde: Vifurushi vya vipengee hutumwa kiotomatiki baada ya programu kusakinishwa. Programu hii haihitaji kufunguliwa ili ianze kupakuliwa. Kipakuliwa pia hakizuii mtumiaji kufungua programu.
    • Kutuma panapohitajika: Vifurushi vya vipengee hupakuliwa vinapohitajika wakati programu inafanya kazi.
  • Iwapo programu yako ina kiteua lugha cha ndani ya programu, unaweza kutumia API ya lugha za ziada kuwaruhusu watumiaji kufikia na kupakua nyenzo za lugha za ziada wanapozihitaji.

Kutumia kichunguzi cha App Bundle

Unaweza kutumia kichunguzi cha App Bundle kukagua matoleo ya programu, kupakua vipengee na kupata maarifa kuhusu mambo ambayo Google Play hubuni kwa ajili ya utumaji. 

Ukurasa wa kichunguzi cha App bundle una kichujio cha toleo kwenye sehemu ya juu kulia mwa ukurasa, ambacho unaweza kutumia pamoja na vichupo vitatu hapa chini ili kukagua mipangilio na matoleo tofauti ya APK za usambazaji wa programu yako kwenye vifaa mbalimbali. Kichujio hiki cha toleo kinafanya kazi kama “Maktaba ya vizalia vya programu” kwenye toleo la zamani la Dashibodi ya Google Play.

Kichunguzi cha App bundle kina vichupo vitatu:

  • Maelezo: Kagua maelezo ya kina kwa kila toleo la programu yako.
  • Vipakuliwa: Tengeneza viungo vya kusakinisha kwa kila toleo la programu yako, pakua APK za vifaa mahususi za kujaribu au kusakinisha mapema kwenye vifaa, pakua APK ya jumla na udhibiti vipengee vingine vinavyohusiana na kila toleo.
  • Kutuma: Kagua vitu ambavyo Google Play hubuni kutoka kwenye App Bundle yako na hali ambazo vizalia vyote vya programu za usambazaji hutumwa.

Masharti ya msingi na mapendekezo

Kagua maelezo ya APK yako

Ili uone APK ambazo Google Play hutengeneza kutoka App Bundle yako:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo > Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Kwenye kichupo cha Vifaa, chagua kichujio cha toleo karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Kagua maelezo ya toleo.
    • Si lazima: Chini ya sehemu ya “Vifaa vya Android vinavyotumika,” unaweza kuchagua Angalia orodha ya vifaa ili uone na udhibiti vifaa ambavyo vinaoana na toleo hili la programu yako.

Shiriki kiungo cha kusakinisha

Ili ushiriki kiungo cha kusakinisha APK inayofaa kifaa mahususi ambayo Google Play hubuni kutoka kwenye App Bundle yako:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Chagua kichujio cha toleo kilicho karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Chagua kichupo cha Vipakuliwa.
  5. Ili kushiriki kiungo cha kusakinisha APK ya kifaa mahususi: Kwenye sehemu ya “Kiungo cha kushiriki programu ndani”, chagua Nakili kiungo kinachoweza kushirikiwa.
  6. Shiriki kiungo.
    • Kidokezo: Unaweza kuchagua Dhibiti ufikiaji ili utembelee ukurasa wa Kushiriki programu ndani na ushiriki kwa haraka viungo vya App Bundle na APK na timu yako. Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye Shiriki App Bundle na APK ndani.

Pakua APK za vifaa mahususi

Unaweza kupakua APK za vifaa mahususi na upakue APK za kusakinisha mapema kwenye vifaa mahususi ili ushiriki na Kampuni zinazotengeneza vifaa (OEM) ili kusakinisha mapema kwenye vifaa vyao (ziweze kusasishwa mara kwa mara kwenye Google Play).

Ili upakue APK za vifaa mahususi ambazo Google Play hutengeneza kutoka App Bundle yako:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo > Vifaa na matoleo > Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Chagua kichujio cha toleo kilicho karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Chagua kichupo cha Vipakuliwa.
  5. Kwenye jedwali la “APK za Vifaa Mahususi”, chagua aikoni ya kupakua karibu na APK ambayo ungependa kuhifadhi au kushiriki.

Pakua APK ya jumla iliyoambatishwa cheti

APK ya jumla iliyoambatishwa cheti ni APK moja inayoweza kusakinishwa ambayo imeambatishwa cheti kwa kutumia ufunguo sawa wa kuambatisha cheti kwenye programu unaotumiwa na huduma ya Google Play ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu wa programu yako. Unaweza kusambaza APK hii kwenye maduka ya programu na njia nyingine za usambazaji kama vile tovuti ili kila unaposambaza programu yako, iambatishwe cheti kwa kutumia ufunguo sawa.

Ili upakue APK ya jumla iliyoambatishwa cheti:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Chagua kichujio cha toleo kilicho karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Chagua kichupo cha Vipakuliwa.
  5. Kwenye jedwali la “Vipengee”, chagua aikoni ya kupakua karibu na faili ya "APK ya Jumla Iliyoambatishwa Cheti".

Pakua faili za vipengee na za kufumbua

Ili upakue faili za vipengee, faili za kufumbua na alama asili za utatuzi wa APK ambazo Google Play hutengeneza kutoka kwenye App Bundle yako:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Chagua kichujio cha toleo kilicho karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Chagua kichupo cha Vipakuliwa.
  5. Kwenye jedwali la “Vipengee”, chagua aikoni ya kupakua karibu na faili ambazo ungependa kuhifadhi kipengee.

Angalia maelezo ya kutuma ya sehemu ya vipengele na vifurushi vya vipengee

Ukitumia huduma ya Utumaji wa Vipengele vya Google Play kuweka mapendeleo kwenye utumaji wa sehemu za vipengele au Play Asset Delivery ili kuweka mapendeleo kwenye utumaji wa vifurushi vya vipengee, kichupo chako cha Kutuma kwenye ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle kitawekewa maelezo muhimu. Ili uone maelezo haya:

  1. Fungua ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Chagua kichujio cha toleo kilicho karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa.
  3. Kwenye jedwali la “Chagua toleo”, chagua kishale cha kulia kwenye toleo ambalo ungependa kuangalia.
  4. Chagua kichupo cha Kutuma.
  5. Angalia maelezo ya kutuma katika majedwali yanayopatikana, ambayo yanaorodhesha jina, hali za kutuma na ukubwa wa vipakuliwa:
    • Sehemu: Huonyesha maelezo ya sehemu za vipengele. Jedwali hili hupatikana kila wakati na huwa na sehemu ya msingi ya programu yako.
    • Vifurushi vya vipengee: Huonyesha maelezo ya vifurushi vya vipengee kwenye programu yako. Jedwali hili linapatikana tu iwapo kuna vifurushi vya vipengee vinavyohusishwa na programu yako.
  6. Bofya safu mlalo ya jedwali ili uangalie kila kitu ambacho Google hubuni kutoka kwenye App Bundle yako inayohusiana na sehemu mahususi za kipengele au vifurushi vya vipengee, ikiwa ni pamoja na:
    • Hali za kina za kutuma (iwapo zinatumika)
    • Maelezo kuhusu APK zozote zilizobuniwa zenye vipengele vingi
    • Maelezo kuhusu APK zozote zilizobuniwa za kujisimamia
      • Kumbuka: APK zenye vipengele kamili hujumuisha kila wakati sehemu ya msingi na sehemu zozote za vipengele au vifurushi vya vipengee vilivyotumwa wakati wa kusakinisha. APK zenye vipengele kamili zinajumuisha pia sehemu zozote zinazohitajika ambazo zinaweza kuunganishwa.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2579786783642496615
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false