Kutumia Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu

Kwa kutumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu, Google hudhibiti na kulinda ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu na kuutumia kuambatisha cheti kwenye APK za usambazaji zilizoboreshwa ambazo zimetengenezwa kutoka kwenye App Bundles zako. Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu huhifadhi ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu katika mfumo salama wa Google na hukupa chaguo la kupata toleo jipya ili kuimarisha usalama.

Ili utumie kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu, unapaswa kuwa mmiliki wa akaunti au mtumiaji aliye na ruhusa ya Kuchapisha matoleo ya umma, kutenga vifaa na kutumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu na unapaswa kukubali Sheria na Masharti ya Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu.

Jinsi kinavyofanya kazi

Unapotumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu, funguo zako huhifadhiwa kwenye mfumo sawa wa usalama ambao Google hutumia kuhifadhi funguo zake. Funguo hulindwa na Huduma ya Google ya Kudhibiti Funguo. Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu mfumo wa Google, soma Ripoti Rasmi ya Usalama wa Wingu la Google.

Programu za Android huambatishwa vyeti kwa kutumia ufunguo binafsi. Ili kuhakikisha kuwa masasisho ya programu yanaaminika, kila ufunguo binafsi una cheti husika cha umma ambacho hutumiwa na huduma na vifaa ili kuthibitisha kuwa sasisho la programu linatoka kwenye chanzo kimoja. Vifaa hukubali tu masasisho wakati vyeti vilivyoambatishwa vinalingana na vyeti vya programu zilizosakinishwa. Kwa kuiruhusu Google idhibiti ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu, inafanya mchakato huu uwe salama zaidi.

Kumbuka: Kwa programu zilizowekwa kabla ya Agosti 2021, bado unaweza kupakia APK na kudhibiti funguo zako badala ya kutumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu na kuchapisha kwa kutumia Android App Bundle. Hata hivyo, iwapo utapoteza ufunguo wako au utaathiriwa, hutaweza kusasisha programu yako bila kuchapisha programu mpya yenye jina jipya la kifurushi. Kwa programu hizi, Google Play inapendekeza utumie kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu na ubadilishe ili uchapishe kwa kutumia App Bundles.

Ufafanuzi wa funguo, vizalia vya programu na zana
Kipindi Maelezo
Ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu

Ufunguo ambao Google Play hutumia kuambatisha vyeti kwenye APK ambazo huwasilishwa katika kifaa cha mtumiaji. Unapotumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu, unaweza kupakia ufunguo uliopo wa kuambatisha cheti kwenye programu au uruhusu Google ikutengenezee ufunguo.

Hifadhi ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa faragha, lakini unaweza kushiriki cheti cha umma cha programu yako na watu wengine.

Ufunguo wa kupakia

Ufunguo unaotumia kuambatisha cheti kwenye App Bundle kabla ya kuipakia kwenye Google Play. Hifadhi ufunguo wako wa kupakia kwa faragha, lakini unaweza kuruhusu ufikiaji wa cheti cha umma cha programu yako kwa watu wengine. Kwa sababu za usalama, tunakushauri uwe na ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu na mwingine tofauti wa kupakia.

Kuna njia mbili za kutengeneza ufunguo wa kupakia:

  • Tumia ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu: Iwapo utairuhusu Google ikutengenezee ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu, ufunguo utakaotumia katika toleo lako la kwanza ndio utakuwa ufunguo wako wa kupakia.
  • Tumia ufunguo tofauti wa kupakia: Iwapo utaweka ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu, utapewa chaguo la kutengeneza ufunguo mpya wa kupakia ili kuimarisha usalama. Iwapo hutazalisha ufunguo wa kupakia, tumia ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu kama ufunguo wako wa kupakia ili kuambatisha cheti kwenye matoleo.
Cheti (.der au .pem)

Cheti kina ufunguo wa umma na maelezo ya ziada ya kutambulisha mmiliki wa ufunguo. Cheti cha ufunguo wa umma kinamruhusu mtu yeyote athibitishe aliyeambatisha cheti kwenye App Bundle au APK, na unaweza kuutumia pamoja na mtu yeyote kwa sababu haujumuishi ufunguo wako binafsi.

Ili usajili funguo zako kwa watoa huduma za API, unaweza kupakua cheti cha umma kwa ajili ya ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu na ufunguo wako wa kupakia kutoka kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu) katika Dashibodi ya Google Play. Unaweza kuruhusu ufikiaji wa cheti cha ufunguo wa umma kwa mtu yeyote. Hakijumuishi ufunguo wako binafsi.

Alama bainifu ya cheti

Kipengee kifupi na maalum kinachowakilisha cheti ambacho mara nyingi huombwa na watoa huduma za API pamoja na jina la kifurushi ili kusajili programu itumie huduma zao.

Unaweza kupata alama bainifu za MD5, SHA-1 na SHA-256 za vyeti vya kupakia na vya kuambatisha kwenye programu katika ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu) katika  Dashibodi ya Google Play. Alama nyingine bainifu zinaweza pia kukokotolewa kwa kupakua cheti halisi (.der) kwenye ukurasa mmoja.

Java keystore (.jks au keystore) Hazina ya vyeti vya usalama na funguo binafsi.
Zana ya Kusimba na kuhamisha Funguo Binafsi kwenye Google Play (PERK)

Zana ya kutuma funguo binafsi kutoka Java keystore na kuzisimba kwa njia fiche ili kuzituma kwenye Google Play.

Unapoweka ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ili utumiwe na Google, teua chaguo la kutuma na kupakia ufunguo wako (na cheti chake cha umma panapohitajika) na ufuate maelekezo ya kupakua na kutumia zana hii. Ukipenda, unaweza kupakua, kukagua na kutumia msimbo wa programu huria katika zana ya PEPK.

Mchakato wa kuambatisha cheti kwenye programu

Utafuata utaratibu huu:

  1. Ambatisha cheti kwenye App Bundle na uipakie katika Dashibodi ya Google Play.
  2. Google hutengeneza APK zilizoboreshwa kutoka App Bundle yako na kuziambatisha vyeti kwa kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.
  3. Google hutumia apksigner kuweka mihuri miwili kwenye faili ya maelezo ya programu yako (com.android.stamp.source na com.android.stamp.type) kisha kuambatisha vyeti kwenye APK kwa kutumia ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu. Mihuri iliyowekwa na apksigner huwezesha APK kuhusishwa na aliyeziambatisha vyeti.
  4. Google huwapa watumiaji APK zilizoambatishwa vyeti.

Weka mipangilio na udhibiti kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti Kwenye Programu

Iwapo programu yako bado haijaanza kutumia kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti Kwenye Programu, fuata maagizo hapa chini.

Hatua ya 1: Tengeneza ufunguo wa kupakia

  1. Kwa kufuata maagizo haya, tengeneza ufunguo wa kupakia.
  2. Ambatisha cheti kwenye App Bundle kwa kutumia ufunguo wa kupakia.

Hatua ya 2: Andaa toleo lako

  1. Fuata maagizo ya kuandaa na kusambaza toleo lako.
  2. Baada ya kuchagua kikundi lengwa, sehemu ya “Uadilifu wa programu” huonyesha hali ya kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu kwa programu yako.
  3. Ili uendelee ukitumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu uliotengenezwa na Google, pakia App Bundle yako. Pia, unaweza kuchagua Badilisha ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ili ufikie chaguo zifuatazo:
    • Tumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu uliotengenezwa na Google: Zaidi ya asilimia 90 ya programu mpya zinatumia funguo za kuambatisha cheti kwenye programu zilizotengenezwa na Google. Hatua ya kutumia ufunguo uliotengenezwa na Google hulinda dhidi ya kupotea au kuhatarishwa (ufunguo hauwezi kupakuliwa). Ukiteua chaguo hili, unaweza kupakua APK za usambazaji kwenye Kichunguzi cha App Bundle kilichoambatisha cheti kwa kutumia ufunguo uliotengenezwa na Google kwa ajili ya njia nyingine za usambazaji au utumie ufunguo tofauti kwa njia hizo.
    • Tumia ufunguo tofauti wa kuambatisha cheti kwenye programu: Hatua ya kuchagua ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu inakuruhusu utumie ufunguo sawa na ule uliotumiwa kuambatisha cheti kwenye programu nyingine katika akaunti yako ya msanidi programu au uhifadhi kwenye kifaa nakala ya ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ili kurahisisha mambo zaidi. Kwa mfano, huenda tayari ufunguo umechaguliwa kwa sababu programu imesakinishwa mapema kwenye baadhi ya vifaa. Hatua ya kuhifadhi nakala ya ufunguo wako nje ya seva za Google inaongeza hatari ikiwa ufunguo ulio kwenye kifaa utaathiriwa. Una chaguo zifuatazo za jinsi ya kutumia ufunguo tofauti:
  4. Kamilisha maagizo yaliyosalia ili kuandaa na kusambaza toleo lako.

Kumbuka: Unahitaji kukubali Sheria na Masharti na ujijumuishe katika mpango wa kuambatisha cheti kwenye programu ili uendelee.

Hatua ya 3: Sajili ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa watoa huduma za API

Iwapo programu yako inatumia API zozote, kwa kawaida unahitaji kusajili ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu nao kwa madhumuni ya uthibitishaji kwa kutumia alama bainifu ya cheti. Utapata cheti hicho hapa:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya “Ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu” kisha unakili alama bainifu (MD5, SHA-1 na SHA-256) za cheti chako cha kuambatisha kwenye programu.
    • Kama watoa huduma za API wanahitaji aina tofauti ya alama bainifu, unaweza pia kupakua cheti halisi katika muundo wa .der na kukigeuza ukitumia zana ya kubadilisha ambayo mtoa huduma wa API anataka.
Masharti ya ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu

Unapotumia ufunguo uliotengenezwa na Google, Google hutengeneza kiotomatiki ufunguo thabiti uliosimbwa kwa njia fiche wa RSA ulio na biti 4096. Ukichagua kupakia ufunguo wako mwenyewe wa kuambatisha cheti kwenye programu, lazima uwe ufunguo wa RSA ulio na biti 2048 au zaidi.

Maagizo kwa programu zilizowekwa kabla ya Agosti 2021

Hatua ya 1: Weka mipangilio ya kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).
  2. Iwapo hujafanya hivyo, soma Sheria na Masharti ya mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu kisha uchague Kubali.

Hatua ya 2: Tumia Google nakala ya ufunguo wako halisi na utengeneze ufunguo wa kupakia

  1. Bainisha ufunguo wako halisi wa kuambatisha cheti kwenye programu.
  2. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).
  3. Teua chaguo la kutuma na kupakia linalofaa zaidi mchakato wa toleo lako na upakie ufunguo uliopo wa kuambatisha cheti kwenye programu.

Hatua ya 3: Kuunda ufunguo wa kupakia (si lazima na tunapendekeza)

  1. Unda ufunguo wa kupakia na upakie cheti kwenye Google Play.
    • Unaweza pia kuendelea kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu kama ufunguo wako wa kupakia.
  2. Nakili alama bainifu (MD5, SHA-1 na SHA-256) ya cheti chako cha kuambatisha kwenye programu.
    • Kwa sababu za majaribio, huenda ukahitaji kusajili cheti cha ufunguo wako wa kupakia kwa watoa huduma za API ukitumia alama bainifu ya cheti na ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.

Hatua ya 4: Ambatisha cheti kwenye sasisho la programu yako inayofuata ukitumia ufunguo wa kupakia

Unapotoa masasisho ya programu yako, unahitaji kuambatisha vyeti kwa kutumia ufunguo wako wa kupakia.

  • Iwapo hukutengeneza ufunguo mpya wa kupakia: Endelea kutumia ufunguo wako halisi wa kuambatisha cheti kwenye programu ili uambatishe vyeti kwenye App Bundles kabla ya kuzipakia kwenye Google Play. Iwapo utapoteza ufunguo wako halisi wa kuambatisha cheti kwenye programu, unaweza kutengeneza ufunguo mpya wa kupakia na uusajili katika Google ili uendelee kusasisha programu yako.
  • Iwapo ulitengeneza ufunguo mpya wa kupakia: Tumia ufunguo wako mpya wa kupakia ili kuambatisha vyeti kwenye App Bundles kabla ya kuzipakia kwenye Google Play. Google hutumia ufunguo wa kupakia ili kuthibitisha utambulisho wako. Iwapo utapoteza ufunguo wako wa kupakia, unaweza kuwasiliana na kituo cha usaidizi ili uubadilishe.
Pata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu ili ujiandikishe kwenye kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti Kwenye Programu

Huenda ukataka kufanya hivyo ikiwa huwezi kuruhusu ufikiaji wa ufunguo wako uliopo. Kabla hujachagua kupata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu ili ujiandikishe, kumbuka kwamba:

  • Chaguo hili litahitaji matoleo mawili.
  • Utahitaji kupakia App Bundle na APK iliyoambatishwa cheti kwa kutumia ufunguo uliopitwa na wakati katika kila toleo. Google Play itatumia App Bundle zako kuzalisha APK zilizoambatishwa vyeti kwa kutumia ufunguo mpya wa vifaa vilivyo kwenye Android R* (Kiwango cha API cha 30) au toleo jipya zaidi. APK zako zilizopitwa na wakati zitatumika kwa matoleo ya zamani ya Android (hadi kiwango cha API cha 29).

*Iwapo programu yako inatumia sharedUserId, inapendekezwa utumie toleo jipya la ufunguo kwa usakinishaji na masasisho kwenye vifaa vinavyotumia Android T (kiwango cha API cha 33) au zaidi. Ili uweke mipangilio hii, tafadhali weka kiwango sahihi cha chini cha toleo la SDK kwenye mipangilio ya kifurushi.

Hatua ya 1: Pakia ufunguo wako mpya kisha uzalishe na upakie ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo

Ili ufunguo mpya uaminike kwenye vifaa vya Android, ni lazima upakie ufunguo mpya wa kuambatisha cheti kutoka kwenye hazina kisha uzalishe na upakie ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).
  2. Chagua kichupo cha Kuambatisha cheti kwenye programu.
  3. Bofya Onyesha chaguo za kina, kisha uchague Tumia ufunguo mpya wa kuambatisha cheti kwenye programu (hii inahitaji matoleo mawili yanayoendelea).
  4. Unaweza kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ulio sawa na ule wa programu nyingine kwenye akaunti yako ya msanidi programu au upakie ufunguo mpya wa kuambatisha cheti kwenye programu kutoka Android Studio, Java KeyStore au hazina nyingine.
  5. Kwa kufuata maagizo yaliyo kwenye skrini, pakua kisha utekeleze zana ya PEPK.
  6. Baada ya ZIP yako kuwa tayari, bofya Pakia ZIP iliyozalishwa kisha uipakie kwenye Dashibodi ya Google Play.
  7. Karibu na "5. Ruhusu ufunguo mpya uaminike kwenye vifaa vya Android kwa kupakia ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo," bofya Onyesha maagizo.
  8. Pakua APKSigner kisha uzalishe ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo kwa kutekeleza amri hii:
    • $ apksigner rotate --out /path/to/new/file --old-signer --ks old-signer-jks --set-rollback true --new-signer --ks new-signer-jks --set-rollback true
  9. Bofya Pakia faili ya ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo iliyozalishwa kisha upakie ithibati ya ruhusa ya kubadilisha ufunguo iliyozalishwa kwenye hatua ya 8.
  10. Bofya Hifadhi.

Tengeneza ufunguo wa kupakia na usasishe hifadhi za funguo

Ili kuimarisha usalama, tunapendekeza uambatishe cheti kwenye programu ukitumia ufunguo mpya wa kupakia badala ya ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu.

Unaweza kutengeneza ufunguo wa kupakia wakati unajijumuisha katika mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu au unaweza kutengeneza ufunguo wa kupakia baadaye kwa kutembelea ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).

Fuata utaratibu huu ili utengeneze ufunguo wa kupakia:

  1. Fuata maelekezo kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android. Hifadhi ufunguo wako mahali salama.
  2. Tuma cheti cha ufunguo wako wa kupakia katika muundo wa PEM. Badilisha vipengele vifuatavyo tulivyopigia mstari:
    • $ keytool -export -rfc -keystore upload-keystore.jks -alias upload -file upload_certificate.pem
  3. Ukiona kidokezo wakati wa mchakato wa kuchapisha, pakia cheti ili ukisajili kwenye Google.

Unapotumia ufunguo wa kupakia:

  • Ufunguo wako wa kupakia unasajiliwa tu na Google ili kuthibitisha utambulisho wa mtayarishi wa programu.
  • Cheti chako huondolewa kwenye APK zozote ulizopakia kabla ya kutumwa kwa watumiaji.
Masharti ya ufunguo wa kupakia
  • Ni lazima uwe ufunguo wa RSA ulio na biti 2048 au zaidi.
Kusasisha hifadi za funguo

Baada ya kutengeneza ufunguo wa kupakia, yafuatayo ni baadhi ya maeneo ambayo unaweza kuangalia na kusasisha:

  • Mashine za mfumo
  • Seva iliyofungwa iliyo mahali ulipo (ACL zinazotofautiana)
  • Mashine ya wingu (ACL zinazotofautiana)
  • Huduma maalum za kudhibiti siri
  • Hazina (Git)

Pata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu

Sehemu hii ina maagizo yanayohusiana na kupata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu. Ikiwa umepoteza ufunguo wako wa kupakia, huhitaji kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo; badala yake, rejelea Ufunguo wako wa kupakia umepotea au kuathiriwa? katika sehemu ya chini ya ukurasa huu.

Katika hali fulani, unaweza kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kufanya utume ombi la kupata toleo jipya la ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu:

  • Unahitaji ufunguo ulio na usimbaji fiche thabiti zaidi.
  • Ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu umeathiriwa.

Muhimu: Masasisho ya ufunguo yanatumika tu kwa programu zinazotumia App Bundle.

Kabla ya kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo katika Dashibodi ya Google Play, soma sehemu ya Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo hapa chini. Kisha unaweza kupanua sehemu zingine hapa chini ili upate maelezo zaidi kuhusu kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo.

Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo

Kabla ya kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo, ni muhimu uelewe mabadiliko ambayo huenda ukahitaji kufanya baada ya kupata toleo jipya la ufunguo.

  • Ikiwa unatumia ufunguo mmoja wa kuambatisha cheti kwenye programu nyingi ili uruhusu ufikiaji wa msimbo au data kati ya programu hizo, unahitaji kusasisha programu zako ili zitambue vyeti vyako vipya na vya zamani vya ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.
  • Ikiwa programu yako inatumia API, hakikisha kwamba umesajili vyeti vya ufunguo wako mpya na wa zamani wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa watoa huduma za API kabla ya kuchapisha sasisho ili kuhakikisha kuwa API zinaendelea kufanya kazi. Vyeti vinapatikana kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu) katika Dashibodi ya Google Play.  
  • Ikiwa mtumiaji wako yeyote atasakinisha masasisho ya programu yako kati ya kompyuta katika mtandao mmoja, ataweza tu kusakinisha masasisho ambayo yameambatishwa vyeti kwa kutumia ufunguo sawa na ule uliotumiwa kuambatisha cheti kwenye toleo la programu yako ambayo tayari amesakinisha. Ikiwa atashindwa kusasisha programu kwa sababu amesakinisha toleo la programu yako ambalo limeambatishwa ufunguo tofauti, atakuwa na chaguo la kuondoa na kusakinisha upya programu ili apate sasisho.
Tuma ombi la kusasisha ufunguo kwa ajili ya usakinishaji kwenye Android N (Kiwango cha API cha 24) na toleo jipya zaidi

Unaweza kupata toleo jipya la ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye kila programu kwa ajili ya usakinishaji katika Android N (Kiwango cha API cha 24 ) na toleo jipya zaidi mara moja kila mwaka.

Ikiwa umetuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo huu, ufunguo wako mpya utatumika kuambatisha cheti katika akaunti za programu zote zilizosakinishwa na masisho ya programu. Kwenye vifaa vinavyotumia  Android N (Kiwango cha API cha 24) hadi Android S (Kiwango cha API cha 32), Google Play Protect itahakikisha kuwa masasisho ya programu yameambatisha cheti kwa kutumia ufunguo wenye toleo jipya, isipokuwa ikiwa imezimwa na mtumiaji. Kwenye vifaa vinavyotumia Android T (Kiwango cha API cha 33) na toleo jipya zaidi, mfumo wa Android hutekeleza matumizi ya ufunguo wenye toleo jipya.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu (Toleo > Mipangilio > Kuambatisha cheti kwenye programu).
  2. Katika kadi ya “Pata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu”, chagua Tuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo.
  3. Teua chaguo ili upate toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa programu zote zilizosakinishwa katika Android N na toleo jipya zaidi.
  4. Ruhusu Google itengeneze ufunguo mpya wa kuambatisha cheti kwenye programu (inapendekezwa) au upakie ufunguo.
    • Baada ya kupata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu, ikiwa ulikuwa unatumia ufunguo mmoja kuambatisha cheti kwenye programu na kupakia, unaweza kuendelea kutumia ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu uliopitwa na wakati kama ufunguo wa kupakia au utengeneze ufunguo mpya wa kupakia.
  5. Chagua sababu ya kutuma ombi la kupata toleo jipya la ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.
  6. Ikiwa inahitajika, sajili ufunguo wako mpya wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa watoa huduma za API.

Kidokezo: Ikiwa unasambaza programu yako kwenye vituo vingi vya usambazaji na ungependa kuongeza uoanifu wa sasisho la programu kwa ajili ya watumiaji wako, unapaswa kupata toleo jipya la ufunguo wako kwenye kila mfumo wa usambazaji. Ili uweze kutumia toleo jipya la ufunguo la Google Play, tumia zana ya ApkSigner, iliyounganishwa naZana za Muundo wa Android SDK (sasisho la 33.0.1 na mapya zaidi):

$ apksigner sign --in ${INPUT_APK}

--out ${OUTPUT_APK}

--ks ${ORIGINAL_KEYSTORE}

--ks-key-alias ${ORIGINAL_KEY_ALIAS}

--next-signer --ks ${UPGRADED_KEYSTORE}

--ks-key-alias ${UPGRADED_KEY_ALIAS}

--lineage ${LINEAGE}

 Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi masasisho ya programu yanavyofanya kazi.

Mbinu bora

  • Iwapo pia unasambaza programu yako nje ya Google Play au unapanga kufanya hivyo baadaye na unataka kutumia ufunguo sawa wa kuambatisha cheti kwenye programu, una chaguo mbili: 
    • Ruhusu Google itengeneze ufunguo (inapendekezwa) kisha upakue APK ya jumla iliyoambatishwa cheti kwenye Kichunguzi cha App Bundle ili usambaze programu nje ya Google Play.
    • Au unaweza kutengeneza ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ambao unataka kutumia katika maduka yote ya programu, kisha utume nakala yake kwa Google unapoweka mipangilio ya kipengele cha Google Play cha Kuambatisha Cheti kwenye Programu.
  • Ili kulinda akaunti yako, washa kipengele cha Uthibitishaji wa hatua mbili katika akaunti zinazoweza kufikia Dashibodi yako ya Google Play.
  • Baada ya kuchapisha App Bundle katika kikundi lengwa, unaweza kutembelea Kichunguzi cha App Bundle  ili ufikie APK zinazoweza kusakinishwa ambazo Google imetengeneza kutoka kwenye App Bundle yako. Unaweza:
    • Kunakili na kutuma kiungo cha kuruhusu ufikiaji wa programu ndani ya kampuni ambacho kinakuruhusu ujaribu kwa mguso mmoja maudhui ambayo Google Play itachapisha kutoka kwenye App Bundle yako katika vifaa tofauti.
    • Kupakua APK ya jumla iliyoambatishwa cheti. APK hii moja imeambatishwa cheti kwa kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu unaohifadhiwa na Google na inaweza kusakinishwa kwenye kifaa chochote kinachotumia programu yako.
    • Kupakua faili ya ZIP yenye APK zote kwa ajili ya kifaa mahususi. APK hizi huambatishwa vyeti kwa kutumia ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu unaohifadhiwa na Google., na unaweza kusakinisha APK zilizo kwenye faili ya ZIP katika kifaa kwa kutumia amri ya adb install-multiple *.apk.
  • Ili kuimarisha usalama, tengeneza ufunguo mpya wa kupakia ambao haufanani na ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu.
  • Ikiwa unatumia API yoyote ya Google, huenda ukahitaji kusajili ufunguo wa kupakia na vyeti vya ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu katika Dashibodi ya Wingu la Google kwa ajili ya programu yako.
  • Ikiwa unatumia Viungo vya Programu ya Android, hakikisha kuwa unasasisha funguo kwenye Faili husika ya JSON ya Viungo vya Vipengee Dijitali katika tovuti yako.

Je, ufunguo wako wa kupakia umepotea au umeathiriwa?

Ikiwa umepoteza ufunguo wako binafsi wa kupakia au iwapo umeathiriwa, unaweza kutengeneza ufunguo mpya. Mmiliki wa akaunti yako ya msanidi programu anaweza kuanzisha mchakato wa kubadilisha ufunguo kwenye Dashibodi ya Google Play.

Baada ya timu yetu ya usaidizi kusajili ufunguo mpya wa kupakia, mmiliki wa akaunti na wasimamizi wote watapokea ujumbe kwenye Kikasha na barua pepe yenye maelezo zaidi. Kisha unaweza kusasisha funguo zako na kusajili ufunguo kwa watoa huduma za API.

Mmiliki wa akaunti anaweza pia kukatisha ombi la kubadilisha ufunguo kwenye Dashibodi ya Google Play.

Muhimu: Hatua ya kubadilisha ufunguo wako wa kupakia haiathiri ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu ambao Google Play hutumia kuambatisha vyeti upya kwenye APK kabla ya kuziwasilisha kwa watumiaji.

Toleo la 4 la Mpango wa Kuambatisha Cheti kwenye APK

Vifaa vya Android 11 na matoleo mapya zaidi hutumia Toleo jipya la 4 la mpango wa kuambatisha cheti kwenye APK. Mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu hutumia toleo la 4 la kuambatisha cheti katika programu zinazostahiki ili kuziwezesha kufikia vipengele vya usambazaji vilivyoboreshwa vinavyopatikana katika vifaa vipya. Msanidi programu hatakiwi kuchukua hatua yoyote na hakuna athari kutoka toleo la 4 la kusambaza cheti katika programu inayotarajiwa kwa mtumiaji.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13260482503301354742
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false