Sambaza matoleo ya programu katika nchi mahususi

Unaposambaza toleo la programu yako kwenye Toleo la umma, Jaribio la watumiaji wengi au Toleo la jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kulenga toleo lako katika kila kundi kwa watumiaji katika nchi mahususi.

Njia za kutumia mbinu ya kulenga nchi

Zifuatazo ni baadhi ya hali ambazo zinaweza kukusaidia kulenga nchi ambako utasambaza programu:

  • Ikiwa programu yako ina toleo la umma, unaweza kuanzisha toleo la jaribio la watumiaji wengi kwenye nchi mpya bila kupanua usambazaji wa toleo lako la umma kwenye nchi mpya.
  • Ikiwa programu yako ina toleo la jaribio la watumiaji wengi, unaweza kuanzisha toleo la umma kwenye nchi mahususi wakati unaendelea kufanya jaribio la watumiaji wengi kwenye nchi nyingine.
  • Ikiwa ungependa kufanya jaribio la watumiaji wengi kwa kiwango cha kimataifa wakati programu yako inapatikana katika baadhi ya nchi katika toleo la umma.
  • Ikiwa programu yako inapatikana kwenye toleo la umma na jaribio la watumiaji wengi kwenye nchi kadhaa lakini unataka timu zako za ndani ya shirika au za kuhakiki ubora wa programu kimataifa zifikie programu yako kwenye jaribio la watumiaji mahususi.

Ulengaji wa nchi hautumiki kwenye programu katika Toleo la jaribio la ndani. Unaweza kuweka watumiaji kutokea mahali popote kwenye jaribio la ndani. Ikiwa mtumiaji wa jaribio la ndani yupo katika nchi ambapo toleo la umma la programu yako, jaribio la watumiaji wengi au jaribio la watumiaji mahususi halipatikani, mtumiaji bado atapokea programu ya jaribio la ndani.

Wafikie watumiaji wanaofaa

Ili udhibiti nchi ambako matoleo yote ya programu yako yatapatikana, utahitaji kujua tofauti kati ya upatikanaji wa programu na kulenga nchi ambako utasambaza programu.

Upatikanaji wa programu

Upatikanaji wa programu unamaanisha kupatikana kwa programu yako katika toleo la umma. Wakati unachagua kuwa programu inapatikana katika nchi fulani, matoleo ya baadaye ya toleo la umma yatajumuisha nchi hiyo.

Ili udhibiti upatikanaji wa programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uchague programu ambapo unataka kudhibiti upatikanaji. 
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Toleo la umma .
  3. Chagua kichupo cha Nchi au maeneo.
  4. Bofya Weka nchi / maeneo au Ondoa nchi / maeneo na uchague nchi / maeneo unayotaka kuweka au kuondoa. Zingatia yafuatayo kwa ajili ya programu zinazolipishwa na usajili:
    • Ikiwa utaongeza nchi ambako programu inayolipishwa itapatikana, bei mpya zitaongezwa kiotomatiki. Ikihitajika, unaweza kubadilisha bei za nchini baadaye.
    • Ukiuza usajili, hakikisha unaweka bei za nchi / maeneo unayotaka kuweka. Pata maelezo zaidi kuhusu usajili.
  5. Thibitisha chaguo zako.

Kumbuka: Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kulenga usambazaji kwa hatua katika nchi mahususi, nenda kwenye chapisha masasisho ya programu kwa kutumia usambazaji kwa hatua.

Kulenga nchi ambako utasambaza programu yako

Mbali na upatikanaji wa programu ulioweka kwa ajili ya toleo la umma, unaweza kuweka mapendeleo kwenye nchi ambako unalenga kusambaza matoleo ya kujaribu. Kwa chaguomsingi, matoleo yako ya majaribio yanalingana na nchi ambako programu inapatikana, uliyoweka kwa ajili ya toleo la umma.

Masharti: Unaweza kuweka mapendeleo ya nchi ambako inapatikana kwa ajili ya vikundi vya kujaribu programu yako katika hali zifuatazo:

  • Programu yako haina App Bundle iliyopakiwa katika toleo la umma au
  • Programu yako ina App Bundle iliyopakiwa kwenye toleo la umma na angalau nchi moja inapatikana kwenye toleo la umma.

Ili ubadilishe upatikanaji wa matoleo ya kujaribu programu yako:

Inaweza kuzimwa iwapo mtumiaji hana ruhusa za kubadilisha.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uchague programu ambapo unataka kudhibiti upatikanaji wa majaribio.
  2. Nenda kwenye kikundi cha majaribio unachotaka kusasisha: 
    • Ukitaka kusasisha programu kwenye jaribio la watumiaji wengi, bofya Jaribio la watumiaji wengi (Jaribio > Jaribio la watumiaji wengi) na uchague kichupo cha Nchi / maeneo
    • Ukitaka kusasisha programu kwenye jaribio la watumiaji wengi, bofya Jaribio la watumiaji mahususi (Jaribio > Jaribio la watumiaji mahususi), bofya Dhibiti kikundi kando ya kikundi unachotaka kusasisha na uchague kichupo cha Nchi / maeneo.
  3. Upatikanaji katika nchi unasawazishwa na toleo la umma kwa chaguomsingi. Hali hii humaanisha kuwa mabadiliko yoyote unayofanya katika kipengele cha upatikanaji kwenye toleo la umma au usajili wa mapema yatafanyika pia kwenye toleo la kikundi cha majaribio. Ili ubadilishe hali hii, bofya Sawazisha nchi / maeneo. Usawazishaji utawashwa iwapo: Unaweza kuzimwa iwapo mtumiaji hana ruhusa za kubadilisha.
    • Kikundi chako hakina toleo lililosambazwa;
    • toleo lako la umma linalenga angalau nchi/eneo moja; au
    • kipindi cha kujisajili mapema kimeanza na kinalenga angalau nchi moja isiyobainishwa katika kundi la "Nchi Nyingine Ulimwenguni".
  4. Ikiwa kikundi chako hakijasawazishwa tena na toleo la umma, unaweza kubofya Badilisha nchi  na uchague nchi / maeneo unayotaka kuongeza au kuondoa.
  5. Thibitisha chaguo zako.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9996594745454899259
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false