Angalia na udhibiti vifaa vinavyooana na programu yako

Baada ya kupakia angalau App Bundle moja kwenye Dashibodi ya Google Play, unaweza kuangalia orodha ya vifaa vilivyopo na ukague vinavyoweza kutumika kwenye programu yako. Ili kuhakikisha upatikanaji mpana zaidi wa programu yako, kagua orodha zako za vifaa vinavyotumika na vilivyotengwa mara kwa mara.

Nenda kwenye ukurasa wa Orodha ya vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa).

Kumbuka kuwa, orodha ya vifaa haitumiki katika programu zinazofunguka papo hapo.

Kuanza kutumia orodha ya vifaa

Kifungu hiki kina maelezo yote unayohitaji kujua ili uanze kutumia orodha ya vifaa.

Kubali Sheria na Masharti ya orodha ya vifaa

Unapofikia orodha ya vifaa kwa mara ya kwanza, ni lazima ukague na ukubali Sheria na Masharti. Lazima uwe mmiliki au mtumiaji wa akaunti mwenye ruhusa ya jumla ya "kudhibiti matoleo ya umma" ili ukubali sheria na masharti mapya. Mara tu unapokubali sheria na masharti mapya ya programu moja katika akaunti yako, utaweza kuendelea kutumia orodha ya vifaa kwenye programu zako zote.

Usipokubali Sheria na Masharti:

  • Hutaweza kufikia orodha ya vifaa.
  • Hutaweza kutenga vifaa ili visisambaze programu.

Elewa dhana za msingi

Maswali yaliyo hapa chini yanahusu dhana za msingi zinazohusu orodha na masharti ya vifaa. Bofya swali ili upanue na uone jibu au likunje.

Je, muundo wa kifaa ni nini? Je, kibadala cha kifaa ni nini?

Muundo wa kifaa ni dhana inayofafanuliwa na kampuni inayotengeneza vifaa vya asili (OEM). Ni jinsi Dashibodi ya Google Play inavyoelezea kifaa ili kubainisha sifa zake na kuunganisha miundo sawa ya vifaa vya Android vinavyotumika hivi sasa.

Muundo wa kifaa unajumuisha sifa mbili: chapa ya muuzaji na kifaa. Sifa zote mbili zimeainishwa na kampuni halisi iliyotengeneza kifaa (OEM).

  • Chapa ya muuzaji: android.os.Build.Brand. (Kumbuka kuwa chapa ni jinsi kifaa kinavyouzwa, na huenda ikawa na jina tofauti na la mtengenezaji.) Pata maelezo zaidi
  • Kifaa: android.os.Build.Device. Pata maelezo zaidi

Kwa mfano, google oriole ni muundo wa kifaa.

Pia, kila muundo wa kifaa una jina kwa ajili ya watumiaji, linalojulikana kuwa jina la chapa. Kwa mfano, jina la chapa ya google oriole ni Pixel 6.

Muundo wa kifaa una sifa za maunzi na programu tofauti, na muundo wa kifaa pekee hautoshi kubainisha sifa hizi kipekee. Kwa mfano, miundo ya vifaa mara nyingi huwa na vibadala vyenye matoleo ya Android, RAM, nafasi ya hifadhi

Kwa muhtasari, haya ni mambo muhimu zaidi ya kuzingatia kuhusu miundo ya vifaa:

  • Kifaa pekee hakijitoshelezi na kinaweza kutumiwa na watengenezaji wengi, hivyo hakipaswi kutumiwa bila chapa.
  • Si mara zote muundo wa kifaa hutosheleza kubainisha sifa za kifaa, kwa sababu vibadala vinaweza kuwepo.
  • Jina la chapa halitoshi kubainisha muundo wa kifaa, kwa kuwa mtengenezaji anaweza kutumia jina moja la chapa kwa michanganyiko tofauti ya {brand device}.

Kwenye Dashibodi ya Google Play, vifaa huonyeshwa kwenye fomu {brand device} (Jina la chapa), kwa mfano: “google oriole (Pixel 6)”, ili iwe rahisi kuunganisha jina linaloonekana kwa mtumiaji na sifa mahususi za kifaa.

Ni vifaa gani vinaonekana kwenye orodha? Ni lini vifaa vipya vitaonekana?

Vifaa huonekana kwenye orodha mara tu vinapotumiwa na kundi kubwa la watumiaji.

Orodha huonyesha vifaa vyote, vilivyothibitishwa na visivyothibitishwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa vifaa hapa chini.

Je, programu au mchezo wangu utapatikana kwenye kifaa kipya?

Kifaa chochote kipya kinapatikana kwa ajili ya kutoa huduma, hata kabla hakijaonekana kwenye orodha, ilimradi:

  • Inasimamiwa na taarifa za kifaa katika faili ya maelezo ya programu yako; na
  • Imejumuishwa kwenye Dashibodi ya Google Play.

Hali hii inamaanisha kuwa watumiaji wanaweza kusanikisha programu yako kwenye miundo ya vifaa ambayo haijathibitishwa isipokuwa ukichukua hatua kuzuia kitendo hiki. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa vifaa hapa chini.

Je, uthibitishaji wa vifaa ni nini? Je, vifaa ambavyo havijathibitishwa hushughulikiwa vipi kwenye Google Play?

Muundo wa kifaa uliothibitishwa ni ule ambao kampuni halisi iliyotengeneza kifaa (OEM) imethibitisha kuwa unaoana na Android kwa kupakia nakala yake ya matokeo ya jaribio la uoanifu wa Android kwa Google. Muundo wa kifaa usiothibitishwa ni ule ambao kampuni halisi iliyotengeneza kifaa (OEM) haijathibitisha kuwa unaoana na Android kwa kupakia nakala yake ya matokeo ya jaribio la uoanifu wa Android kwa Google. Kwa hivyo:

  • Vifaa ambavyo havijathibitishwa huenda visiwe salama.
  • Vifaa ambavyo havijathibitishwa huenda visipate masasisho ya mfumo au masasisho ya programu.
  • Programu na vipengele kwenye vifaa ambavyo havijathibitishwa huenda visifanye kazi vizuri.
  • Data kwenye vifaa ambavyo havijathibitishwa huenda haitahifadhiwa nakala kwa usalama.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu sifa na jinsi ambavyo vifaa vilivyothibitishwa na visivyothibitishwa hufanya kazi:

  • Uonekanaji katika orodha: Miundo ya vifaa visivyothibitishwa itaonekana katika orodha ya vifaa inapokuwa ba kundi kubwa la watumiaji. Ili uiangalie, unaweza kuchuja kwa hali ya uthibitishaji wa vifaa kwenye orodha ya vifaa. Miundo ya vifaa vilivyothibitishwa inaweza kuwa na vibadala visivyothibitishwa. Hali hii hutokea ikiwa vifaa vinaripoti kuwa muundo wa vifaa uliothibishwa, lakini havipitii ukaguzi wa Play Integrity API. Hali hii haionekani kwenye orodha ya vifaa.
  • Usambazaji: Huenda programu yako ikapatikana kwa ajili ya kusakinishwa kutoka Google Play kwenye miundo ya vifaa visivyothibitishwa isipokuwa ukichukua hatua ili kuzuia kitendo hiki. Tembelea sehemu ya Kudhibiti usambazaji wa programu yako kwenye vifaa ambavyo havitimizi masharti ya uadilifu wa kifaa iliyo hapa chini ili upate maelezo zaidi.
  • Vipimo vya Android vitals: Vifaa vilivyothibitishwa tu na vyenye uadilifu kamili huchangia vipimo vya ubora wa kiufundi kwenye Vipimo muhimu (Vitals) vinavyoweza kuathiri uwezo wa kutambulika na kutangazwa kwa programu yako kwenye Google Play.

Elewa ulengaji wa vifaa wa programu yako

Seti ya miundo ya vifaa ambayo watumiaji wanaweza kugundua na kusakinisha programu yako kwenye Google Play inajulikana kuwa vifaa vinavyolengwa. Vifaa vyako vinavyolengwa vinabainishwa na vitu viwili: taarifa ya faili yako ya maelezo na kanuni zako za kutenga dashibodi. Taarifa na kanuni hizi hutumika kwenye vifaa na programu katika viwango tofauti vya ukubwa.

Taarifa za faili ya maelezo fafanua vifaa ambavyo programu yako hutumia. Hufanya kazi katika kiwango cha kifaa mahususi. Kwa mfano, kuweka minSdk kwenye Android 9 kutahakikisha kuwa vifaa vinavyotumia Android 9+ tu ndio vinatimiza masharti ya programu yako. Ikiwa muundo wa vifaa una vibadala vingine kwenye Android 9 na matoleo ya chini zaidi, hivyo vibadala vya Android 9 vitakuwa vimetimiza masharti, lakini matoleo ya chini zaidi hayatatimiza masharti.

Unaweza kutumia utengaji wa dashibodi katika viwango viwili:

  1. Katika kiwango cha muundo wa kifaa: Katika hali hii, vifaa vyote vilivyo na muundo huu havijumuishwi.
  2. Katika kiwango cha kanuni: Utengaji kulingana na kanuni hutumika katika kiwango cha kifaa cha mtu binafsi, kama vile taarifa ya faili ya maelezo. Hii inamaanisha kuwa miundo ya baadhi ya vifaa huenda ikaonekana katika orodha kama vile havijajumuishwa kikamilifu.

Kumbuka: Utengaji hubatilisha vifaa vinavyotumika vilivyobainishwa kwenye faili ya maelezo ya programu yako.

Ili uangalie vifaa vyote vinavyopatikana na kuelewa mahali ilipo programu yako kwa ajili ya usambazaji katika Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Orodha ya vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa).
  2. Chagua vichupo vya Zote, Zinazotumika, Zilizotengwa, au Zinazolengwa.
  3. Ili upakue orodha ya vifaa ikiwa faili ya CSV, bofya Pakua orodha ya vifaa karibu na upande wa kulia wa ukurasa.

Ili kuelewa hali ya ulengaji wa muundo wa kifaa mahususi, angalia safu wima ya "Hali" katika kurasa za Orodha ya vifaa au Maelezo ya vifaa. Hatua hii inaonyesha hali ya ulengaji wa kifaa kwa App Bundle zote zinazotumika au APK zinazohusiana na programu yako. Unaweza kupanua sehemu iliyo hapa chini ili kuangalia hali mahususi zinazolengwa za miundo ya kifaa.

Hali zinazolengwa za miundo ya kifaa
  • Zinazotumika: Programu yako inapatikana kwa watumiaji wa kifaa hiki katika Google Play.
  • Zisizotumika kikamilifu: Programu yako inapatikana kwa baadhi ya vibadala vya muundo wa kifaa hiki lakini si vyote.
  • Zilizotengwa kwa kanuni: Programu yako haipatikani kwenye muundo huu wa kifaa. Utaona hali hii ikiwa una kanuni ya utengaji unaohusiana na muundo huu wa kifaa.
  • Zisizotengwa kikamilifu kwa kanuni: Programu yako inapatikana kwa baadhi ya vibadala vya muundo wa kifaa hiki lakini si vyote. Huenda ukaona hali hii ikiwa una kanuni ya utengaji kwenye RAM, ambayo inaweza kutofautiana kati ya vibadala vya muundo wa vifaa.
  • Zilizoendolewa na mtumiaji mwenyewe: Programu yako haipatikani katika muundo huu wa vifaa. Utaona hali hii tu ikiwa umeondoa mwenyewe muundo wa kifaa.
  • Isiyotumika: Programu yako haipatikani kwenye vifaa vyovyote vilivyo na muundo huu wa kifaa. Utaona hali hii ikiwa faili yako ya maelezo inahitaji kipengele au sifa (Kwa mfano, ukubwa wa skrini au kiwango cha SDK) haipatikani kwenye kifaa. Kwa mfano, baadhi ya vifaa huenda visiwe na kitambuzi cha dira. Kama utendaji msingi wa programu unahitaji matumizi ya kitambuzi cha dira, basi programu yako haiwezi kutumika kwenye vifaa hivyo.
    • Kumbuka: Utaona hali hii wakati vibadala vyote vinavyohusiana na muundo wa kifaa si oanifu. Ikiwa baadhi ya vibadala vinaweza kutumika, hali itaonyesha "Baadhi ya vibadala vinatumika."

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya muhimu ya kuzingatia kuhusu ulengaji wa kifaa:

  • Hali ya kutenga vifaa inadhibitiwa kulingana na kila programu.
  • Hali inayotumika kwenye kifaa huonyeshwa katika kiwango cha toleo kwa sababu imebainishwa kwenye faili yako ya maelezo. Kwa sababu unaweza kuwa na vifurushi mbalimbali vilivyochapishwa katika vikundi tofauti (toleo la umma, jaribio la watumiaji wengi na mahususi, jaribio la ndani), kwenye maelezo ya kifaa pia utaona hali ya kila toleo. Kwa mfano, kama toleo la beta la programu yako linahitaji vipengele zaidi kuliko toleo la umma, utaweza kuona kuwa kifaa kinatumia toleo la umma wala si toleo la beta.

Tafuta na uchuje orodha ya vifaa

Orodha ya vifaa itaonyesha miundo yote ya vifaa kwa kichupo ambacho umechagua (vifaa vyote, vifaa vinavyotumika na zaidi), vilivyopangwa kulingana na muundo wa kifaa.

Unaweza kuchanganua orodha ya vifaa kwa njia mbili:

  1. Tumia upau wa kutafutia katika sehemu ya juu ya ukurasa ili uchuje orodha ya miundo au tafuta miundo mahususi ya kifaa.
  2. Chuja orodha ya miundo ya vifaa kulingana na mtengenezaji, vifaa au sifa nyinginezo.

Angalia maelezo ya kifaa

Ili uelewe zaidi kuhusu miundo ya vifaa ikiwa ni pamoja na vibadala, unaweza kubofya kupitia ukurasa wa maelezo.

Ukurasa wa maelezo unakupa maelezo zaidi kuhusu sifa za kifaa na vibadala vya muundo mahususi wa kifaa. Unaweza kupanua sehemu iliyo hapa chini ili uangalie maelezo muhimu ya kifaa.

Maelezo ya kifaa
  • Muhtasari: Vipimo muhimu kwa ajili ya muundo wa kifaa hiki kwenye programu yako, na usambazaji wa muundo wa kifaa hiki kulingana toleo la Android na RAM ya programu yako. Maelezo haya yanaweza kukusaidia kubainisha mantiki sahihi ya kulenga kifaa hiki na matatizo ya utatuzi kwenye muundo wa kifaa.

    Sifa zinazofanana: Sifa ambazo ni sawa kwa vibadala vyote vya muundo huo wa kifaa.

    Sifa za vibadala: Sifa ambazo huenda zikatofautiana kwa matoleo au vibadala vya muundo wa kifaa. Unaweza kubainisha vibadala unavyopendelea kwa kuchagua sifa ambazo ni muhimu.

    Orodha ya vibadala: Orodha ya vibadala vyote vinavyofahamika kwa muundo huu wa kifaa, ikizingatia vichujio vyovyote ulivyotumia kwenye sifa za vibadala. Orodha ya vibadala inaonyesha tu vibadala vilivyothibitishwa.

    Vibadala maarufu zaidi: Kibadala cha muundo wa kifaa hiki ambacho kina programu nyingi zilizosakinishwa kutoka Google Play. Hii inajumuisha programu zote kwenye Google Play, na si mahususi kwa programu yako. Ikiwa muundo wa kifaa una vibadala mbalimbali, kibadala maarufu zaidi kinaweza kusaidia mahali pa kurejelea wakati wa kubainisha muundo wa kifaa wa kupata au kujaribu.

Usijumuishe programu yako katika usambazaji kwenye vifaa fulani

Unaweza kuweka sheria za kutojumuisha vifaa katika usambazaji wa programu yako kwenye Google Play. Vifaa visivyojumuishwa havitaweza kuona au kusakinisha programu yako kwenye Google Play.

Vidokezo

  • Kanuni za kutenga vifaa hazitumiki kwa wanaojaribu matoleo ya ndani
  • Hali ya kutojumuisha vifaa kulingana na ukaguzi wa uadilifu inadhibitiwa kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu). Temebelea ukurasa huu wa Kituo cha Usaidizi ili kupata maelezo ya jinsi ya kuwasha ukaguzi wa uadilifu wa ukurasa wa programu katika Google Play ili Google Play iweze kuhakikisha kwamba vifaa vimepita hatua ya ukaguzi wa uadilifu kabla ya kufanya ukurasa wa programu yako katika Google Play uonekane kwa watumiaji.

Unaweza kupanua na kukunja sehemu zilizo hapa chini ili uelewe chaguo tofauti za usimamizi wa usambazaji wa programu.

Dhibiti usambazaji wa programu yako kwenye miundo mahususi ya vifaa

Unapotenga mwenyewe vifaa ambavyo vina matatizo ya uoanifu yanayojulikana, unaweza kuwasaidia watumiaji wako wapate hali bora ya matumizi. Hii inajulikana kuwa uondoaji unaofanywa na mtumiaji.

Kabla hujatenga kifaa chochote, zingatia yafuatayo:

  • Ukifanya mabadiliko haya utatenga miundo mahususi ya vifaa ya programu yako yote. Huwezi kutenga App Bundle au APK mahususi.
  • Utenganishaji wa muundo wa kifaa unaathiri vibadala vyote vya kifaa ikiwa ni pamoja na vibadala vya baadaye. Ikiwa hamasa yako kwa ajili ya utenganishaji ni kuhakikisha programu yako haipatikani kwenye miundo ya vifaa vyenye sifa mahususi, zingatia kutumia utenganishaji unaozingatia kanuni badala yake.

Kutenga kifaa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Orodha ya vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa).
  2. Chagua muundo wa kifaa ambao ungependa kutenga kisha nenda kwenye ukurasa wa maelezo.
  3. Kwenye upande wa juu kulia mwa skrini yako, chagua Kutenga kifaa. Muundo wa kifaa uliochagua katika hatua ya 2, ikijumuisha vibadala vyote, sasa vitatengwa.
Dhibiti usambazaji wa programu yako kwa kutumia kanuni zinazolingana na sifa za kifaa

Kama unataka kutenga vifaa ukitumia viashirio vya utendaji, unaweza kuunda kanuni za kulenga kulingana na ukubwa wa RAM au Mfumo kwenye Chipu (SoC).

Kwa mfano, kama programu yako inahitaji hifadhi kubwa ya data, unaweza kuweka kanuni inayotenga vifaa vilivyo chini ya RAM ya MB 512.

Kabla ya kuweka mipangilio yoyote ya utenganishaji unaozingatia kanuni, zingatia yafuatayo:

  • Utenganishaji unaozingatia kanuni hutumika kwenye vifaa vipya vilivyoongezwa kwenye orodha na vinavyolingana na vigezo vya kutenga.
  • Kanuni za RAM zinatumika kwa vifaa vya Android 4.1 na zaidi (SDK 16+) na hazitumiki kwa APK za Wear OS. Kanuni za RAM zinatokana na jumla ya hifadhi inayopatikana kwenye kifaa (TotalMem), si hifadhi iliyo na chapa.

Weka sheria

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Orodha ya vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa).
  2. Chagua Kudhibiti masharti ya kutengajirani na upande wa kulia wa ukurasa. 
  3. Chagua RAM au Mfumo kwenye Chipu.
    • Ili kuongeza sheria kadhaa, chagua kitufe cha AU. Kiteuzi kingine kitaonekana.
    • Ili uondoe sheria, chagua aikoni ya 'ghairi' .
  4. Kagua orodha ya vifaa inayoonekana kwenye sehemu ya chini ya skrini yako.
  5. Baada ya sheria yako kulenga orodha inayofaa ya kifaa, hifadhi mabadiliko yako.

Dhibiti usambazaji wa programu yako kwenye vifaa vinavyooana na Android Go

Unaweza kutojumuisha programu yako isipatikane kwenye baadhi ya vifaa kulingana na uoanifu na Android (toleo la Go).

Maelezo ya Android (toleo la Go)

Android (toleo la Go) huboresha hali ya utumiaji wa Android kwenye vifaa vya msingi vinavyotumia Android 8.1 (Kiwango cha API cha 27) au cha juu zaidi yenye RAM isiyozidi GB 1. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuboresha programu zako kwa ajili ya vifaa vinavyotumia Android (toleo la Go).

Weka sheria za kutojumuisha vifaa kwa ajili ya Android (toleo la Go)

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Orodha ya vifaa (Toleo > Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa).
  2. Chagua kichupo cha Vifaa visivyojumuishwa .
  3. Karibu na chaguo la "Sheria za kutojumuisha," chagua Dhibiti sheria za kutojumuisha

  4. Karibu na chaguo la "Kutojumuisha Android Go,” chagua:
    • Utengaji wa Android Go
      • Usitenge vifaa vya Android Go: Huchaguliwa kwa chaguomsingi.
      • Tenga vifaa vya Android Go: Zuia vifaa vinavyotumia Android Oreo (toleo la Go) ili visisakinishe programu yako kwenye Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8456466298395751312
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false