Kuweka punguzo kwenye programu zinazolipishwa

Unaweza kuweka punguzo ili uuze programu unazolipisha kwa bei iliyopunguzwa. Watumiaji wanapoangalia programu yako kwenye Duka la Google Play, wataona bei yenye punguzo na bei ya awali - inafahamika kama uwekaji bei kwa kupiga mstari unaokata kati bei ya awali. 

Weka mipangilio ya punguzo

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Bei ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bei ya programu).
  2. Chagua kichupo cha Mapunguzo.
  3. Bofya Weka Punguzo.
  4. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili ulipatie punguzo lako jina, uweke tarehe ya kuanza na kumalizika kwa punguzo hilo. Jina la punguzo litaonekana tu kwenye Dashibodi ya Google Play na watumiaji hawataliona.
  5. Chagua nchi/maeneo yatakayolengwa na punguzo. Kwa chaguomsingi, maeneo yote yanayopatikana yatachaguliwa na punguzo litapatikana duniani kote. Ikiwa itahitajika, tumia visanduku vya kuteua ili uchague nchi mahususi ambamo utataka punguzo lako lipatikane.
  6. Bofya Badilisha bei yenye punguzo.
  7. Ili uuze programu yako kwa bei iliyopunguzwa: Weka bei yako yenye punguzo (katika sarafu chaguomsingi). Tutatumia bei ambayo utaweka kama msingi wa kukokotoa bei mahususi za soko.
    • Kumbuka: Unaweza kuweka 0 ikiwa ungependa programu yako ilipiwe $0 kwa muda na hatua hii itaweka bei kiotomatiki kuwa 0 pia katika nchi/maeneo mengine yote. Pata maelezo zaidi kuhusu mauzo ya $0 hapa chini.
  8. Bofya Hifadhi. Punguzo lako litaanza kulingana na tarehe ya kuanza uliyoweka katika hatua ya 4.

Mwongozo na masharti

Mwongozo na masharti haya yanabainisha jinsi mapunguzo ya programu zinazolipishwa yanavyofanya kazi ndani ya Dashibodi ya Google Play. Tafadhali wasiliana na timu yako ya kisheria ili uhakikishe vipengele vya ofa, kama vile muda wa ofa, vinatii sheria zinazotumika za ulinzi wa watumiaji wa eneo husika.

Bei na upatikanaji
  • Kwa sasa, unaweza kuweka mapunguzo kwenye programu zinazolipishwa pekee (sio kwenye usajili au bidhaa za ndani ya programu).
  • Ni lazima bei yenye punguzo ya programu yako iwakilishe angalau punguzo la 30% ya bei kamili (kwa kila nchi husika). Isipokuwa katika punguzo la $0, ni lazima bei zote zenye punguzo zifuate viwango vya bei vinavyokubalika.
  • Ili uweke au ubadilishe punguzo, ni lazima uchapishe programu yako.

Mambo muhimu kuhusu mapunguzo ya $0: Punguzo la $0 si la kudumu na si sawa na kutoa programu yako bila malipo, milele. Ukiweka ofa ya $0, haitaathiri uwezo wako wa kulipisha programu baadaye. Ukiweka ofa ya $0, programu yako haitaangaziwa kwenye Chati Maarufu za programu zinazolipishwa, wakati ofa inaendelea.

Mauzo ya $0 hayajumuishwi kwenye takwimu za ununuzi. Kwa hivyo, idadi ya wanunuzi kwenye ripoti zako inaweza kupungua wakati wa ofa. Hali hii itaathiri ripoti zifuatazo:

  • Ukurasa wa muhtasari wa Fedha: Jedwali la wanunuzi litapungua hadi 0.
  • Ripoti ya Wanunuzi ya Fedha: Utaona mabadiliko katika idadi ya wanunuzi wote, wanunuzi wa bidhaa mahususi na wanunuzi wanaorudi tena.
  • Ripoti ya Data ya watumiaji: Utaona mabadiliko katika idadi ya Wanunuzi na Wanunuzi wa Bidhaa Mahususi.
Kipindi
  • Kwa kila programu, ni sharti kuwe na siku 30 kati ya tarehe ya kumalizika kwa ofa moja na kuanza kwa ofa nyingine. Unaweza kubadilisha bei msingi ya programu wakati wowote.
  • Ofa inaweza kudumu kwa siku moja (muda wa chini zaidi) hadi siku nane (muda wa juu zaidi).

Violezo vya bei na mapunguzo

Kwa sababu kila ofa inatolewa kulingana na kila programu, ofa hazitatumika kwenye violezo vya bei.

Kama umeweka ofa kwa programu ambayo iko kwenye kiolezo, utahitaji kusimamisha ofa hiyo au usubiri hadi ofa ikamilike, kabla ya kufanya mabadiliko yoyote kwenye kiolezo.

Angalia na usasishe ofa

Kwenye Dashibodi ya Google Play, unaweza kufikia ofa za awali, ofa zijazo na ofa zinazoendelea.

Sasisha punguzo lijalo au linaloendelea
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Bei ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bei ya programu).
  2. Chagua kichupo cha Mapunguzo.
  3. Karibu na punguzo unalotaka kusasisha, chagua Badilisha punguzo.
    • Kubadilisha jina la punguzo: Unaweza kubadilisha jina la ofa wakati wowote. Kumbuka kuwa jina la punguzo litaonekana tu kwenye Dashibodi ya Google Play na watumiaji hawataliona.
    • Kusasisha tarehe ya kuanza au bei: Unaweza kusasisha tarehe ya kuanza au bei ya ofa zozote zijazo. Kama tayari ofa imeanza, huwezi kubadilisha bei na tarehe ya kuanza.
    • Kumaliza au kurejesha ofa: Kwenye kona ya juu kulia kwenye ukurasa wa ofa inayoendelea, chagua Simamisha au Endelea.
Kukagua mapunguzo ya awali
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Bei ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bei ya programu).
  2. Chagua kichupo cha Mapunguzo. Ikiwa kuna mapunguzo yoyote ya awali ya programu yako, litaorodheshwa hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5281896083819241677
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false