Kuweka taarifa za malipo

Unda wasifu wa malipo katika kituo cha malipo ili udhibiti na ufuatilie mauzo ya programu zako kwenye Dashibodi ya Google Play. Kagua orodha ya Maeneo ambako usajili wa wasanidi programu na wauzaji unaruhusiwa.
  1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya malipo (Weka kisha Taarifa za malipo).
  3. Bofya Weka taarifa za malipo. Hakikisha una maelezo ya biashara yako ili uweke mipangilio ya taarifa zako za malipo.
  4. Chini ya "Taarifa za malipo," bofya kishale cha chini kisha uchague Weka taarifa za malipo.
  5. Jina na anwani: 
    • Weka jina rasmi la biashara yako jinsi unavyotaka lionekane kwenye taarifa zako za malipo. Maelezo haya huonyeshwa kwa wateja wako na kwenye stakabadhi zako za malipo. 
    • Weka anwani yako halali ya biashara jinsi inavyoonekana kwenye hati rasmi. Ni muhimu tuwe na anwani sahihi ya mahali halisi biashara yako ilipo kwenye rekodi zetu. Hatukuruhusu kutumia anwani ya Sanduku la Posta. Baadaye, utahitaji kuhakikisha kuwa akaunti yako ya benki imesajiliwa katika nchi ile ile uliyoweka kwenye taarifa zako za malipo. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya akaunti ya benki.
  6. Anwani msingi: Weka jina la mwakilishi wa kampuni yako aliyeidhinishwa ambaye Google inaweza kuwasiliana naye ikiwa tuna maswali kuhusu akaunti yako ya malipo. Weka anwani ya barua pepe na nambari ya simu (si lazima).
  7. Weka maelezo yafuatayo ya umma ya biashara yako, au chagua kulinganisha maelezo ya akaunti ya umma ya muuzaji na maelezo ya akaunti ya malipo:
    • Weka tovuti yako ya biashara.
    • Chagua aina ya bidhaa unazouza.
    • Barua pepe yako ya huduma kwa wateja.
    • Jina la biashara au bidhaa ambalo litaonekana kwenye taarifa za kadi za mikopo za watumiaji wako.
      • Kidokezo: Ili kuwasaidia wateja kukumbuka walichonunua na kukusaidia kupunguza matukio ya urejeshaji pesa, tumia jina linalofaa kwenye taarifa ya kadi ya mikopo.
  8. Ukimaliza , bofya Wasilisha.
    Kidokezo: Huwezi kubadilisha nchi iliko biashara yako lakini unaweza kubadilisha taarifa zako za umma za muuzaji na za malipo baadaye.

Baada ya kuunda wasifu wa malipo, utaunganishwa kiotomatiki kwenye Dashibodi yako ya Google Play. Kumbuka: Kama ulikuwa umeunda wasifu wa malipo au akaunti ya kituo cha muuzaji, tayari imeunganishwa kwenye Dashibodi ya Google Play.

Ikiwa unahitaji usaidizi, wasiliana nasi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16456348249684441840
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false