Toa masasisho ya programu kwa kutumia usambazaji kwa hatua

Unaweza kutoa sasisho la programu kwa umma na kikundi cha majaribio kupitia usambazaji kwa hatua. Kwa kutumia uchapishaji kwa hatua, sasisho lako hufikia asilimia fulani pekee ya watumiaji wako, unaweza kuongeza asilimia hiyo kadri muda unavyoenda.

Kusambaza kwa hatua kunaweza kutumiwa kwa masasisho ya programu pekee wala si wakati unapochapisha programu kwa mara ya kwanza.

Ustahiki wa watumiaji na ulengaji

  • Watumiaji wapya na waliopo wanaweza kupata masasisho kupitia mchakato wa kusambaza kwa hatua na huchaguliwa bila utaratibu wowote kwa kila uchapishaji wa toleo jipya.
  • Ukisitisha usambazaji wa toleo lako kisha uendelee, utakuwa unaathiri watumiaji walewale.
  • Unaposambaza kwa hatua toleo jipya kabla ya kukamilisha usambazaji kwa hatua wa toleo la awali, toleo jipya litatumia kikundi sawa cha watumiaji kama ilivyokuwa kwa toleo lililotangulia (kulingana na asilimia ya usambazaji kwa hatua).
  • Sasisho la programu yako litapatikana kwa asilimia ya watumiaji iliyo kwenye uchapishaji wako wa hatua, lakini huenda ikachukua muda mwingi kabla ya kikundi chote kupata sasisho hilo.
  • Watumiaji hawataarifiwa wakipokea toleo la programu yako katika usambazaji kwa hatua.
  • Ukichagua nchi mahususi ambapo utasambaza kwa hatua, sasisho litatumiwa tu na watu walio na akaunti za Google Play katika maeneo hayo.

Kuweka na kudumisha usambazaji kwa hatua

Chagua asilimia ya usambazaji kwa hatua

Unaposambaza toleo, unachagua asilimia ya watumiaji watakaopokea toleo hilo. Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye sehemu ya kutayarisha na kusambaza toleo.

Kumbuka, asilimia ya usambazaji kwa hatua ya programu yako haitaongezeka kiotomatiki. Ili ujumuishe asilimia kubwa ya watumiaji katika usambazaji wa programu yako kwa hatua, fuata maagizo yafuatayo.

Sambaza kwa hatua katika nchi mahususi

Unapotoa programu ukitumia usambazaji kwa hatua, unaweza kuanza na nchi chache.

  • Kulingana na mipangilio chaguo-msingi, upatikanaji wa nchi ambapo utachapisha kwa hatua utalingana na maeneo ambayo umeweka katika toleo la umma la programu yako.
  • Baada ya kuanzisha usambazaji kwa hatua, huwezi kuondoa nchi zozote.

Ili kuweka mipangilio ya kulenga nchi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Toleo la umma ikiwa ungependa kusasisha toleo la umma. Iwapo programu yako inafanyiwa majaribio, nenda kwenye ukurasa wa Jaribo la watumiaji wengi au Jaribio la watumiaji mahususi.
  2. Chagua kichupo cha Matoleo.
  3. Kwa toleo ambalo ungependa kusasisha, bofya Badilisha.
  4. Iwapo hungependa kufanya mabadiliko mengine yoyote katika toleo lako, huhitaji kufanya mabadiliko yoyote katika sehemu ya “Tayarisha” kwenye ukurasa wa Buni toleo la umma. Unaweza kubofya Kagua toleo katika sehemu ya chini ya skrini yako ili uende kwenye sehemu ya “Kagua na uchapishe”.
  5. Nenda kwenye sehemu ya "Kusambaza kwa hatua".
  6. Weka asilimia ya kusambaza.
  7. Kwenye sehemu ya “Upatikanaji katika nchi,” teua Chagua maeneo/nchi mahususi, teua kisanduku kilicho kando ya eneo/nchi yoyote ambako ungependa programu yako ipatikane kama sehemu ya mpango wako wa kusambaza kwa hatua. Chaguo za "Upatikanaji katika nchi" zinapatikana tu unaposasisha toleo la umma.
  8. Bofya Anza kusambaza katika toleo la umma.
Kuongeza asilimia yako ya usambazaji kwa hatua
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Toleo la umma ikiwa ungependa kusasisha toleo la umma. Iwapo programu yako inafanyiwa majaribio, nenda kwenye ukurasa wa Jaribo la watumiaji wengi au Jaribio la watumiaji mahususi.
  2. Chagua kichupo cha Matoleo.
  3. Chini ya toleo ambalo ungependa kusasisha, chagua Dhibiti usambazaji > Sasisha usambazaji.
  4. Sasisha asilimia ya usambazaji.
  5. Bofya Thibitisha sasisho.
Kusitisha usambazaji kwa hatua

Ukigundua tatizo, unaweza kusitisha usambazaji kwa hatua ili kusaidia kupunguza idadi ya watumiaji wanaopata tatizo kutokana na programu yako.

Ukisitisha usambazaji kwa hatua, hakuna watumiaji wa ziada watakaopokea toleo la programu yako lililotumika katika usambazaji kwa hatua. Watumiaji ambao tayari walipokea toleo la programu katika usambazaji kwa hatua watabaki na toleo hilo.

Kusitisha kwa kutumia tovuti ya Dashibodi ya Google Play

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Toleo la umma ikiwa ungependa kusasisha toleo la umma. Iwapo programu yako inafanyiwa majaribio, nenda kwenye ukurasa wa Jaribo la watumiaji wengi au Jaribio la watumiaji mahususi.
  2. Chagua kichupo cha Matoleo.
  3. Chini ya toleo ambalo ungependa kusitisha, chagua Dhibiti usambazaji > Sitisha usambazaji.
Kuendelea na usambazaji kwa hatua

Iwapo Android App Bundle iliyopo haina matatizo yoyote, unaweza kuendelea na usambazaji kwa hatua.

Kutumia tovuti ya Dashibodi ya Google Play

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Toleo la umma ikiwa ungependa kusasisha toleo la umma. Iwapo programu yako inafanyiwa majaribio, nenda kwenye ukurasa wa Jaribo la watumiaji wengi au Jaribio la watumiaji mahususi.
  2. Chagua kichupo cha Matoleo.
  3. Chini ya toleo ambalo ungependa kuendeleza, chagua Dhibiti usambazaji > Endelea kusambaza.
  4. Sasisha asilimia ya usambazaji.
  5. Bofya Thibitisha sasisho.

Kwa kutumia programu ya Dashibodi ya Google Play

  1. Fungua programu ya Dashibodi ya Google Play Programu ya Dashibodi.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye kadi ya "Matoleo yanayotumika," gusa toleo ambako ungependa kuendelea kuchapisha.
  4. Gusa Kusambaza kwa hatua > Endelea kusambaza > Endelea.

Kidokezo: Ukipata tatizo kwenye App Bundle iliyopo, sanidi na usambaze toleo jipya kwa kutumia App Bundle iliyorekebishwa.

Vidokezo vya kusambaza kwa hatua moja kwa moja

  • Ikiwa sasisho la programu yako linahitaji mabadiliko kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play, tunapendekeza usasishe ukurasa wa programu katika Google Play baada ya toleo lako kusambazwa kwa asilimia 100 ya watumiaji.
  • Wakati wa uchapishaji kwa hatua, ni vizuri kufuatilia kwa makini ripoti za kuacha kufanya kazi na maoni ya wateja. Wateja wanaopokea programu kupitia usambazaji wa hatua kwa hatua wanaweza kutoa maoni yao kwa umma kwenye Google Play. Pata maelezo zaidi kuhusu kuangalia ukadiriaji na maoni kupitia Dashibodi ya Google Play.

Maudhui yanayohusiana

  • Pata maelezo zaidi kuhusu kutoa masasisho taratibu kupitia usambazaji wa hatua kwa hatua kwenye Chuo cha Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16036747611390763019
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false